Kufunga kula kila baada ya muda fulani katika wiki hurefusha maisha na kuzuia magonjwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Watafiti nchini Marekani wamebaini kwamba kutokula kwa masaa 16-18 au kufunga kula kila baada ya muda fulani katika wiki hurefusha maisha na kuzuia magonjwa.

Katika makala iliyoandikwa katika jarida la “New England Medicine”, imebainishwa kwamba kula ndani ya masaa 6-8 katika siku na masaa yaliyobaki 16-18 kukaa mbali na chakula hukinga mwili kutokana na magonjwa tofauti, ikiwa ni pamoja na kupunguza shinikizo la damu na kurefusha maisha.

Katika makala hiyo imesisitizwa kwamba kufunga kula ni moja ya njia zinazowezapendekezwa katika tiba ya kiribatumbo, kisukari na magonjwa ya moyo, katika hilo inapendekezwa kufunga siku 2 kwa wiki au “kula kiasi kidogo kila siku”

Utafiti uliofanywa kwa kutumia binadamu na wanyama umeonyesha kwamba kufunga kila baada ya muda maalumu huweza michakato katika mwili “metabolism” kuhuishwa upya kitu ambacho hufanya afya ya seli za mwili kuboreka.
 
Amesema mtume Muhammad . Fungeni mtapata afya . Hadiith sahihi. Huyo ndo daktari wa madaktari . Ukibisha andamana magu akuvunje mguu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema utadhan kama ni muujiza wakati wayahudi walifunga miaka 1000 kabla ya mtume kuzaliwa
Ni wayahudi au ni wana wa israel?manake wana wa Israel walikua Na taurat ambayo ni kitabu cha mungu ila wayahudi sijui kitabu chao ni kipi
 
Kila myahudi ni Mwana wa Israel ila sio kila mwana wa Israel ni myahudi...it is the immutable law of unidentity....wayahudi ni mojawapo kwenye makabila 12 ya waisrael...Jews and benjaminites ni makabila mawili pendwa ambayo hayakuasi na tulipata wafalme wengi hata yesu alikuja kuzaliwa humo.
 
Kwa hiyo torati inawahusu?
 
Ni kweli kufunga kula ni tiba sahihi sana. Lkn pia watu tuachane na matumizi ya sukari. Sukari haina faida yoyote katika mwili wa binadamu. Watoto tusiwaharibu kwa kuwapa sukari ili wazoee tangu utotoni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom