Kufumaniwa DC Igunga akipanga mipango ya wizi wa kura; walinzi wetu wapo likizo au dharau dharau?

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
233
Ni siku chahce zimepita tangia DC wa Igunga Mama F. Kimario kukamatwa na wafuasi wa CDM akihujumu na kuendesha mkutano wa kikampeni kukisaidia chama tawala kinyume cha sheria za nchi na kinnyume na kanuni za kazi zake na maadili. DC huyu alikutwa akifanya hivyo akitumia wadhifa wake na mali za serikali kwenye muda wa serikali. Sio mara ya kwanza viongozi wa andamizi wa serikali kufanya hivi. Wengi wanatumia madaraka serikali , mali na muda wa walipa kodi kuhakikisha chama tawala kinabaki madarakani kwa gharama zozote zile. Mambo haya ni uvunjifu wa maadili na sheria za nchi zinazomkataza mtumishi wa serikali kukisaidia chama cha siasa kwa kutumia cheo chake, mali na ofisi za serikali kwa namna yeyote ile. Kama Tanzania ingekuwa inafuata sheria leo hii wengi wangekosa kazi kwa kosa hili.

Vyama vya upinzani ambavyo ni waathirika wakubwa wa hujuma hizi wamekuwa wakipiga kelele na kulalamika tume ya uchaguzi, msajili wa vyama , polisi na hata bungeni ila wahusika kwa miaka takribani 18 wamekuwa kimya, kwani wanaolalamikiwa wanafaidika na matumizi haya mabaya ya madaraka, kwani viongozi hawa wamewekwa ili kulinda chama kilichopo madaraka hasa wakati wa uchaguzi.

Hatari hii inazidi kukua na watumiaji wa vyombo vya umma bado jawajaweza kusoma ishara za nyakati. Zamani wananchi walikuwa wanaheshimu, amini viongozi wa serikali natumaini mpaka leo bado heshima ipo ila tu pale viongozi hawa watakapokuwa wanatimiza wajibu wao. Tanzania inatakiwa ijue bila kujali chama gani kitaongoza dola, kuwa sie sio kisiwa. Elimu inaongezeka sana, kuna ongezeko kubwa sana la shule za msingi mpaka vyuo ukilinganisha na idadi ya watu wameongezeka sana. Pamoja na wakwamba elimu inayotolewa sio bora ina inamfanya mwananchi kumjua adui yake ni nani.

Madhara ya viongozi wanaotakiwa kufuata na kuwa mfano kuvunja sheria ndio imetumbukiza nchi nyingi kwenye machafuko, kwani viongozi hawa wanajipa U-Miungu watu wanaamini kuwa hawawezi kuguswa na sheria. Wananchi wanaona siku hadi na wanachoka. Kama ilivyokuwa kwa kibaka kuanza kuchomwa au majambazi kupigwa mawe. haya yalianza baada ya wananchi kuamini hakuna haki polisi hivyo kila mmoja ajichukulie sheria mkononi, na haya yalienziwa na serikali chovu pale ilipokubali kuwa marehemu aliuwawa baada ya wananchi wenye hasira kali kumdhania mwizi au jambazi. Hapa swala la sheria lilioneka halina maana kupigiwa kelele mpaka vibaka walipochanganywa na wema wote kuitwa vibaka.

Hatari ya kutokufanya kazi kwa misingi ya sheria za haki, hupelekea hali tete ya usalama wa nchi wananchi na mali zao, kwani watu wakichoka kusubiria haki huinyakua haki.

Pamoja na magazeti na baadhi ya watu kuona kitendo alichofanyiwa Mkuu wa Wilaya wa igunga ni kizuri au kibaya, tukumbuke kuwa haya yote ni matokea ya sheria kuchezewa na wanaotakiwa kuzilinda. Nasikitika sana Mkuu wa wilaya kutumiwa na CCM bila yeye kujua anachokifanya ni hatari kwa maisha yake na anawaongoza. Kama sio busara iliyotumika kumwokoa baada ya wananchi kujua alikuwa nataka kuwadhulumu haki yao ya kidemokrasia leo yangekuwa mengine wala si haya tunayosikia sasa.

Wito kila mwenye dhamana afanye kazi yake kwa mujibu wa sheria. Wananchi wanamadai ya kweli na uchungu dhahiri. Umasikini ni bomu ambalo halitakiwi kuchezewa. Tayari wananchi wamekata tamaa na aina yeyote ya dhuluma wako tayri na lolote. Tusiichezee amani kwa kofia za utawala au cheo. Kama kila mtu asivyompenda kibaka, jamabazi na anatamani hawa watu wesiwepo kwenye uso wa dunia ndivyo wanaopenda demokrasia ya kweli wasivyoweza kukubaliana na matendo ya DC F Kimario kwa lugha zote. DC Kimario ni mfano wa Ma DC wengi wasio jua nini maadili ya kazi zao na kwamba wao ni viongozi wa wananchi wote. DC Kimario amedhihirisha Tanzania hahitaji hizi nafasi za ukuu wa wilaya kwani hauna kazi zaidi ya kuwa makada wa CCM.

Ndugu watanzania tusijifiche kwenye kivuli chochote kile, lazima wanavunja sheria washughulikiwe, na lazima DC ashughulikiwe kwa mujibu wa hseria na maadili ya kazi yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom