Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

ngusillo, Ingekuwa kweli Kama wasingemfukuza. Angetoka mwenyewe. Ni rahisi kurudi

Sent using Jamii Forums mobile app

Nakuhakilishia hii ni michezo ya kizazi cha CCM kilichoshindwa na kukosa maarifa. Kikundi hiki haramu kinawalazimisha wananchi wasio na hatia kuendelea kuteketea kwa maradhi, ukosefu wa elimu sahihi, ujinga na umaskini.

Mimi nimeapa kuipigania kweli mpaka nitakapoona hakuna watoto wanaokufa kwa maradhi yaliyosahauliwa na nchi za wenzetu. Nitakaa kimpa pale nitakapoona hakuna udhalimu na wizi wa waziwazi.

Pale nitalapoona mwananchi wa Tanzania anaweza kumchagua kiongozi anayemtaka. Pale mwananchi atakapoandika katiba anayoitaka na wawakilishi kutunga sheria zinazomsaidia mwananchi.

CCM imetugeuza sisi wananchi kama mifugo yao au kwa haraka Magufuli ameamua kuifanya nchi itumbukizwe kwenye maangamizi ya lazima.

Nawaonea sana huruma watanzania hasa mnaoshabikia maangamizi badala ya kulia, kuomboleza na kujuta.
 
Hawa n zaid ya misukule
Ingekuwa huyo amefukuzwa upinzani na hasa Chadema humu vijana wa ccm wangechaniana nguo wakiisakama Chadema kama chama kisicho na demokrasia.

Sasa kwa kuwa ni huko kwao na kwa kuwa kafukuzwa kwa kutishia nafasi ya mfalme wao ktk azma yake ya kuendelea kuhodhi kiti chake, wanadai eti ni kwa kukiuka maadili.. maadili gani, hawasemi.!!! Ni unafiki ulioje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nidhamu au uoga kule n kusifu na kuabudiana tu hakuna namna
Ni uamuzi makini sana kusafisha nyumba mapema, kwani hawa mngewaacha mwishoni kabisa karibia na uchaguzi wangewaletea yale ya mwaka 2015, na matokeo yake wanachama wangegawanyika na kupunguza ushindi wa CCM halikadhalika CCM kujipa tabu kuisaka dola.

Ndio maana wapinzani wamelaani sana Kinana, hasa Membe kutolewa mapema, kwani turufu yao ilikua ajikatae uchaguzi ukikaribia.

Sasa Membe kabla hajafanya hivyo amewahiwa. Kiukweli CCM muendelee kuhakikisha masalia yote ya 2015 ya makundi yanakwisha au kumalizwa nguvu kabisa.

Nidhamu ndani ya chama kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu ni muhimu sana.

Mwisho kabisa CCM hongereni kwa kuonyesha kwamba ni taasisi imara haiyumbishwi na majina ya wale wanaojifanya bila wao CCM haipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Tundu Lissu ambaye alijibatiza kuwa mwandishi wa orodha ya mafisadi lakini baadae kuongoza kampeni ya usafishaji.Baada ya Bernard Membe kufurushwa CCM kajitenga naye, hataki kusema lolote kwani anajua watu watakumbushia kauli zake za zamani dhidi ya Membe.

Hata hivyo,Tundu Lissu pamoja na wafuasi wengine Chadema wanajua alipangalo Mbowe halipanguliki zaidi ya wao kulitekeleza.

Kwa hulka ya Mbowe hawezi kumkataa mtu maarufu anayekuja na hela kisa akina Lissu watanununa, amri ni moja tu 'shuka kwenye treni wengine wapande'.

Mbwa akimwona chatu hujipeleka mwenyewe huku akilia kumezwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wewe bibi,CDM imekufanya nini?
Hivi kweli una muda wa kuijali familia yako?
Hivi kweli una muda wa kufanya majukumu yako ya kikazi?
Hivi kweli ulipotibiwa Mirembe ulipona?
Hivi kweli hata mumeo unamtaja jina mara nyingi kama CHADEMA,Mbowe na Lissu?
Hivi kweli leo utaenda kanisani na kushiriki ibada pamoja na ushirikina wako wote asubuhi asubuhi hii!?
 
Wakudadavuwa, Ajira hakuna,sekta ya kilimo ipo hoi,mikopo kwa wanachuo shida,diplomasia ya nje,ipo hovyo,ufisadi mtupu NIDA,
Lakini nyie mnamzungumzia Mbowe tu! Mbowe hana serikali,hana hazina,hana msjeshi!CCM vyote hivyo mnavyo tangu 1961!lakini mpaka leo hatuwezi kuzalisha sukari,na mafuta ya kula ya kutosha!

Kiwanda cha paleto mafinga kiliwashinda,nendeni mkaone "beberu" mmarekani anachofanya, Ametumia akili kidogo tu,anamhudumia mkulima kuanzia pembejeo,elimu,na mkulima analipwa hapo hapo!
Kwenye korosho, mkapereka jeshi,matokeo yake!fuckups ! tupu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Bernard Membe akizungumza na mtendaji wa Londo alijinasibu kuwa ule waraka wa makatibu wakuu wastaafu (Kinana na Makamba) umetafsiriwa (kautafsiri) na umesambazwa (kausambaza) kwa mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao Tanzania. Aliamini kwa kufanya hivyo basi amepeleka ujumbe kuwa Tanzania 'imekwama'.

Kama 'jasusi mbobezi'' na ''mwanadiplomasia'' hili lilikuwa ni tusi dhidi ya nchi na dhidi ya Mabalozi husika kwani hata kama nia ilikuwa ni kuleta mgogoro basi waliacha kwani ilishajulikana kuwa wanafanyia kazi ''fitina zilizofitinika'' waliamua kujitenga nazo na kujitenga naye (Membe).

Ikumbukwe miaka michache iliyopita Balozi ya EU alifurushwa nchini na kilichotokea EU waligundua kuwa balozi wao ''kachemka'' na wameteua mwingine na mambo yanasonga kama yalivyopangwa.

Ni dhahiri hii ni aibu nyingine kwa Membe kidiplomasia na kijasusi.
 
Mbona unaweweseka na kuanza ramli chonganishi mapema?
Tulia dawa iwaingie taratibu msije kuoverdose mkasingizia daktari.

Membe ameshikilia kile anachoamini mwache.Mambo ya mabalozi na diplomasia unaijua wewe?Tulia hivyohivyo Membe ana lake jambo ambalo mimi na wewe huenda hatujalijua na huwezi jua analingia nini.
Ccm mnalingia polisi,mahakama,NEC je,Membe analingia nini?Mimi na wewe hatujui ila muda ndo refa bora zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_20200208_130009.jpg


Hili ni swali tu ndugu zangu , maana mtu huyu aliingia kwenye 5 bora za wagombea Urais wa CCM kwenye kinyang'anyiro cha 2015 , na kwa hatua aliyofika bila shaka wapo waliomuunga mkono .

Je bado wapo , ni akina nani na bado wanazo nguvu za ushawishi ?
 
Membe kafukuzwa kama Mbwa aisee, inawezekana wamefanya assessment wakaona jamaa Hana lolote cha kuwafanya ..... Wakaona wamsukumizie huko huko Kwa Zitto ili wawe na one way battle , na sio kuwa na joint batlles ambazo hazina maana , mpigane ndani na nje tena jamaa wakaona isiwe taabu tumuunganishe Tu , na walivyo wajanja wamefanya divide and rule , wakamtosa alone , membe naye alivyo boya akaropoka Nina watu serikalini , CCM na usalama , wenzake watakuwa monitored sana
 
Kila MTU ameshuhudia kufukuzwa kwa membe ndani ya ccm ,na waliomfukuza wanadai amekosa maadili ndani ya chama ,lakin kwa upande wake anadai kisa anataka kusiamama na mwenyekiti kwenye kura za maoni, sasa hapa sina shaka ndan ya ccm kuna makundi mawili yanayotaka mwenyekiti asipingwe na MTU ambapo kutopingwa na MTU ni utamaduni wao waliojiwekea lakin katiba ya chama inaruhusu MTU kuchukua form na kusimama na mtangulizi wake na hili kundi ni ccm wapya na kuna kundi linalotaka mwenyekiti apate mpinzani na hili kundi ni ccm asilia na ni wengi sana kuliko wapya ,sasa swali langu ni je kwakuwa membe kakatwa mapema tu ,lakini ikatokea mwana ccm mwingine akajitosa wazwaz kupambana na mwenyekiti wake kabla ya miez michache kufikia uchaguz itakuaje? Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom