Kufukuzwa kwa Halima Mdee na Wenzake 18 na mkanganyiko wa Ubunge wao

Mei 11,2022 CHADEMA imeandika historia ya kuwavua uanachama, Wanachama wao 19 ambao wengi ni waandamizi na wamewahi kuwa viongozi wakubwa katika chama hicho. Baadhi ya Makosa makubwa yaliyosababisha wavuliwe uanachama ni pamoja na;
1. KUGHUSHI NYARAKA ZA CHAMA
2. KUGHUSHI SAINI YA KATIBU MKUU WA CHAMA
3. KUTENGENEZA ORODHA ISIYO HALALI YA WABUNGE WA VITI MAALUM KUTOKA CHAMA HICHO.
4. KUGHUSHI MUHURI WA CHAMA.

Tujikumbushe baadhi ya taratibu zinazowapa uhalali wabunge wa viti maalum kuteuliwa kuwa wabunge.
1. Orodha ya majina ya wanaopendekezwa kuwa wabunge wa viti maalumu huandaliwa na na kila chama cha siasa kinanachogombea nafasi za urais na ubunge katika Uchaguzi Mkuu, hii ni kwa mujibu wa ibara ya 66(1) na ibara ya 78 ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977.

2. Orodha hii huwasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi siku 30 kabla ya Uchaguzi Mkuu, CHADEMA ni miongoni mwa vyama vilivyotii jambo hili la kisheria.

3. Majina ya Wanawake wagombea waliopendekezwa na vyama vya siasa yatakuwa katika mpangilio kwa kuzingatia kipaumbele (order of preference) hii ni kwamujibu wa kifungu cha 86A(4) cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Itakumbukwa kwamba, CHADEMA iliilalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa umma kuhusu kughushi majina ya kina Halima Mdee, na sasa CHADEMA hiyo hiyo imewahukumu wabunge hao kwa kughushi nyaraka.

Kwa hiki kilichotokea Tume ya Uchaguzi haikustahili kulaumiwa hata kidogo, CHADEMA walipotea kwenye njia zao wenyewe na kama ushahidi umewaweka hatiani wabunge hao 19, chama kinatakiwa kukanusha yale kiliyoyasema awali kuhusu uteuzi wa Wabunge kwamba wametokana na Spika wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kwa namna nyingine, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilikuwa sahihi kabisa kupeleka majina ya wabunge wateule kwa Spika wa Bunge la JMT kwasababu kilipelekewa nyaraka zenye uthibitisho wa chama. Na siyo jukumu la Tume kuverify uhalali wa nyaraka hizo bali chama chenyewe ndio kinapaswa kujiridhisha.

Hukumu hii ya kuwafukuza Wabunge 19 haiondoi uhalali wa nyaraka zilizowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambapo sheria inawataka CHADEMA kuwasilisha Orodha siku 30 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Swali hapa ni je, Ni ipi Orodha ya Bw. Mnyika (KM-CDM) iliyowasilishwa Tume kwa uzingativu wa sheria tajwa?

Pia, tunaweza kujiuliza ikiwa wamefukuzwa wabunge pekee 19, je orodha yao inayolalamikiwa kughushiwa ina wateule 19 pekee?

Na kama imezidi hao wengine uhalali wa uanachama wao uko wapi ikiwa wenzao kwenye kundi moja wamefukuzwa?
Kwa Mtazamo wangu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bunge la JMT wamechafuliwa kwa makosa ya kutozingatia sheria kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

Ingefaa wajitafakari na kujipanga upya kwa hatua zinazofuata kuliko kurudia makosa yaleyale.
Waende wakadai hao zao Mahakamani ikiwa ni pamoja na kudai fidia kutoka CHADEMA kwa kuchafuliwa katika jamii kuhusiana na madai ya KUGHUSHI nyaraka na mhuri. Hii ni scandalous na udhalilishaji kwa Wabunge hao 19. Binafsi naona CHADEMA watakuwa na kesi ya kujibu kwani ni wao, CHADEMA, ndio watakuwa na kazi ya kuihakikishia Mahakama kuwa watuhumiwa walifanya forgery ya aina fulani. The onus will be on CHADEMA side.
 
Heading ya Stori haiendani na Content. Hujazungumzia kabisa mkanganyiko wa Ubunge wao. Nadhani ulipaswa kuandika tu CDM WALIONBE RADHI BUNGE NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
 
1. Kama hao wabunge 19 wa Chadema walighushi saini ya katibu mkuu wa chama, kughushi mhuri wa chama na kuandaa na kupeleka orodha ya majina bungeni na ushahidi usio kuwa na shaka upo bayana basi wawasiliane na DPP wafunguliwe kesi maana ni makosa ya jinai sio nidhamu pekee
2. Kama kwa kujua bunge lilipokea majina kutoka kwa mwakilishi yeyote wa Chadema kinyume na utaratibu na kuhalalisha ubatili basi katibu wa bunge, spika, naibu spika na kamati husika ambayo kwa vyovyote vile ni sharti majina hayo yaitie kwao kabla ya kutangazwa hadharani na mhimili huo basi wanapaswa kuwajibishwa kwa spika na naibu wake kuondolewa kwenye nafasi za uongozi na wale wengine kama katibu wa bunge ambaye ndiye mtendaji mkuu na mwakilishi wa serikali pamaja na kamati husika wanapaswa kufunguliwa mashitaka maana wametenda makosa ya jinai
3. Kama kuna ushahidi kwamba majina ya wabunge wa viti maalum pendekezwa ni sharti yapelekwe na katibu mkuu lakini kwa mazingira ya kesi husika aliyepeleka hana mamlaka ya chama chake basi alipokea hati hizo anatakiwa kushitakiwa pia kwa kuvunja sheria kwa makusudi kwa maslahi binafsi
4. Je, kanuni za bunge zimevunjwa kutokana na maamuzi ya chama cha Chadema kuwafukuzwa wanachama wao? Maana kila kosa linapotendwa huwa kuna muda maalumu wa kuwasilisha lalamiko husika?
5. Kama chama cha Chadema kiliwakataa wabunge 19 waliokuwa wakiwakilisha CDM kwa sababu mbili za kutotambua uteuzi wao na matokeo ya mwaka 2020, je kuwaengua hao watapendekeza wengine waende bungeni kwa uhalali upi unaotokana na kura iliyopigwa wakaikubali?
6. Takribani mwaka mzima sasa wale wabunge wanahudhuria bungeni na kwa mjibu wa sheria chama kinachowakilishwa kinasitahili kupata ruzuku kwa uzingatia asilimia ya uwakilishi, je, Chadema watakuwa na uhalali upi wakipeleka tena wabunge kisha wakakubali kupokea ruzuku waliyoisusia tangu uchaguzi ufanyike mwaka 2020 hadi sasa?
7. Endapo Chadema watadai limbikizo la ruzuku tangu mwaka 2020 hadi sasa itakuwa ni wizi na wanastahili na wenyewe kushitakiwa au kufutwa
8. Kama kuna viongozi wa CCM waliwasimika hao wabunge ndani ya bunge kwa maslahi binafsi, wanatakiwa kushtakiwa kwa mjibu wa sheria
Akili kubwa sana .... Udadisi wa kina kabisa. Shukran!
 
Heading ya Stori haiendani na Content. Hujazungumzia kabisa mkanganyiko wa Ubunge wao. Nadhani ulipaswa kuandika tu CDM WALIONBE RADHI BUNGE NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
hahahhaa Nguruka wa Morogoro
Mwisho wa hoja huwa ni mwanzo wa hoja nyingine natumai kuona andiko lako litakalojikita moja kwa moja katika content!
 
Hivi hakuna wa kulifungulia kesi Jambo hili watu tutazoea kuchezea sheria za Nchi na kuzifanya tunavyotaka
 
Waende wakadai hao zao Mahakamani ikiwa ni pamoja na kudai fidia kutoka CHADEMA kwa kuchafuliwa katika jamii kuhusiana na madai ya KUGHUSHI nyaraka na mhuri. Hii ni scandalous na udhalilishaji kwa Wabunge hao 19. Binafsi naona CHADEMA watakuwa na kesi ya kujibu kwani ni wao, CHADEMA, ndio watakuwa na kazi ya kuihakikishia Mahakama kuwa watuhumiwa walifanya forgery ya aina fulani. The onus will be on CHADEMA side.
Kama vile walinisikia! Si unaona walivyo wapiga CHADEMA goli la kisigino!? Tungoje tuone hii ngom!!a au filamu (kadri utakavyo penda), itakavyo kwenda!
 
Nimetafakari sana na kuona kwamba kumbe kile kitendo cha kuealaumu akina Mdee tunafanya makosa makubwa sana sana,kwani system yote ya CHADEMA ukianzia na Chairman wote ni Wapiga deal tu.Watanzania tujipange Upya tuachane na wanafiki na wanaokopesha AKILI.

Baada ya kutafakari ukaona uanzishie uzi haya mawazo yako.
 
Nimetafakari sana na kuona kwamba kumbe kile kitendo cha kuealaumu akina Mdee tunafanya makosa makubwa sana sana,kwani system yote ya CHADEMA ukianzia na Chairman wote ni Wapiga deal tu.Watanzania tujipange Upya tuachane na wanafiki na wanaokopesha AKILI.
Kwakuwa ni mwana umoja kama SII mwanachukua chako mapema🙄
 
Let the Movie continue 👴🏽View attachment 2251476
20220602_102729.jpg
TACH]
 
Back
Top Bottom