Kufukuzwa kwa Halima Mdee na Wenzake 18 na mkanganyiko wa Ubunge wao

Singo Batan

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
292
191
Mei 11,2022 CHADEMA imeandika historia ya kuwavua uanachama, Wanachama wao 19 ambao wengi ni waandamizi na wamewahi kuwa viongozi wakubwa katika chama hicho. Baadhi ya Makosa makubwa yaliyosababisha wavuliwe uanachama ni pamoja na;
1. KUGHUSHI NYARAKA ZA CHAMA
2. KUGHUSHI SAINI YA KATIBU MKUU WA CHAMA
3. KUTENGENEZA ORODHA ISIYO HALALI YA WABUNGE WA VITI MAALUM KUTOKA CHAMA HICHO.
4. KUGHUSHI MUHURI WA CHAMA.

Tujikumbushe baadhi ya taratibu zinazowapa uhalali wabunge wa viti maalum kuteuliwa kuwa wabunge.
1. Orodha ya majina ya wanaopendekezwa kuwa wabunge wa viti maalumu huandaliwa na na kila chama cha siasa kinanachogombea nafasi za urais na ubunge katika Uchaguzi Mkuu, hii ni kwa mujibu wa ibara ya 66(1) na ibara ya 78 ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977.

2. Orodha hii huwasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi siku 30 kabla ya Uchaguzi Mkuu, CHADEMA ni miongoni mwa vyama vilivyotii jambo hili la kisheria.

3. Majina ya Wanawake wagombea waliopendekezwa na vyama vya siasa yatakuwa katika mpangilio kwa kuzingatia kipaumbele (order of preference) hii ni kwamujibu wa kifungu cha 86A(4) cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Itakumbukwa kwamba, CHADEMA iliilalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa umma kuhusu kughushi majina ya kina Halima Mdee, na sasa CHADEMA hiyo hiyo imewahukumu wabunge hao kwa kughushi nyaraka.

Kwa hiki kilichotokea Tume ya Uchaguzi haikustahili kulaumiwa hata kidogo, CHADEMA walipotea kwenye njia zao wenyewe na kama ushahidi umewaweka hatiani wabunge hao 19, chama kinatakiwa kukanusha yale kiliyoyasema awali kuhusu uteuzi wa Wabunge kwamba wametokana na Spika wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kwa namna nyingine, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilikuwa sahihi kabisa kupeleka majina ya wabunge wateule kwa Spika wa Bunge la JMT kwasababu kilipelekewa nyaraka zenye uthibitisho wa chama. Na siyo jukumu la Tume kuverify uhalali wa nyaraka hizo bali chama chenyewe ndio kinapaswa kujiridhisha.

Hukumu hii ya kuwafukuza Wabunge 19 haiondoi uhalali wa nyaraka zilizowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambapo sheria inawataka CHADEMA kuwasilisha Orodha siku 30 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Swali hapa ni je, Ni ipi Orodha ya Bw. Mnyika (KM-CDM) iliyowasilishwa Tume kwa uzingativu wa sheria tajwa?

Pia, tunaweza kujiuliza ikiwa wamefukuzwa wabunge pekee 19, je orodha yao inayolalamikiwa kughushiwa ina wateule 19 pekee?

Na kama imezidi hao wengine uhalali wa uanachama wao uko wapi ikiwa wenzao kwenye kundi moja wamefukuzwa?
Kwa Mtazamo wangu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bunge la JMT wamechafuliwa kwa makosa ya kutozingatia sheria kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

Ingefaa wajitafakari na kujipanga upya kwa hatua zinazofuata kuliko kurudia makosa yaleyale.
 
Then
images - 2022-05-12T071001.267.jpeg

Now
moto-pic-data.jpg

Tomorrow? Mahakamani? Tusubiri..
 
Mimi sijui lolote kuhusiana na jinsi wabunge wa viti maalumu wanavyopatikana,naomba kujua hiyo orodha ya wateule wa CHADEMA ilipelekwa na nani?au ni nani anapaswa kuiwasilisha huko tume ya uchagzi?
Nchi hii ni ngumu haswaa! Hata aliyekuwa anaminiwa na wanyonge alikuwa tapeli pia!
Eti wanyonge wangu msiwabughudhi huku wenye uelewa akiwafanyia UHUNI.
 
Mzee Mdee alivyokuwa anang’aka hadi misuli ya fuvu inamtoka huwezi kuamini ilikuwa uongo.!
 
Back
Top Bottom