BUSH BIN LADEN
JF-Expert Member
- Mar 16, 2019
- 7,607
- 17,072
Ilikuwa jana 2/4/2020 ambapo zilizuka taarifa za maambukizi ya Covid19 kwenye meli vita ya kubeba ndege ya jeshi la Marekani USS Theodore Roosevelt iliyoko Pacific.
Taarifa hizi zilitolewa na kamanda wa meli hiyo Kapteni Brett Crozier katika barua aliyoiandika akilishutumu jeshi la wana maji la nchi hiyo kutofanya vya kutosha kuwalinda na kuwaokoa wanajeshi wake wanaokufa wakati hawako vitani.
Banda ya barua yake iliyoandikwa 30/03/2020 kuvuja kwa vyombo cya habari, Thomas Modly anayekaimu uongozi wa jeshi la wanamaji ameamua kumtoa kazini kwa madai kwamba barua ya kapteni Crozier ilijenga picha miongoni mwa wengi kwamba jeshi na serikali ya nchi hiyo haifanyi chochote kuwalinda askari wake.
Hii imezua sintofahamu miongoni mwa wamarekani na mataifa mengine kuhusu uhuru wa maoni na kuweka uwazi taarifa zinazohusu janga hili la Corona.
Marekani na nchi nyingi za magharibi zimekuwa zikiilaumu China kuhusu kutotoa taarifa za kina kuhusu corona na kutowajibika hali iliyosababisha gonjwa hili kuenea sana Ila pia wameilaumu serikali ya China ilipomchukulia hatua za kinidhamu daktari wa China alietoa taarifa za mwanzoni kabisa kuhusu corona.
Swali la kujiuliza ni vipi Marekani waliona kitendo alichofanyiwa daktari wa China hakikuwa sahihi ila wao walichomfanyia kamanda wao ni sahihi.
Za kuambiwa changanya na za kwako, kitu kuwa sahihi au kinyume chake muda mwingine inategemea na hali sio uhalisia.
Naomba kuwasilisha