Kufukuza wabunge uanachama wa vyama kunakiuka Katiba ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufukuza wabunge uanachama wa vyama kunakiuka Katiba ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungi, Aug 15, 2011.

 1. Sungi

  Sungi Senior Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vyama vya siasa Tanzania vimekuwa vikifukuza wanachama wao wa ngazi mbalimbali pale viongozi hawa wanapokaidi au kwenda kinyume na itikadi ya chama husika. Lakini nadhani swali la msingi hapa ni kwamba, hawa viongozi, hasa wabunge, wanakuwa wamechaguliwa na wananchi na pengine sio tu na wanachama wa vyama wanavyotoka. Utaratibu huu wa kufukuza uachama viongozi, eti kwa kwenda kinyume na itikadi ya vyama unaendelea kudidimiza democrasia na kuwafanya viongozi wawe watumwa kwa vyama vya siasa na ukiritimba na "wakubwa" wa vyama kwa kuhamisha nguvu ya wananchi kuchagua viongozi wanaowafaa. Hii ni sababu nyingine, katiba yetu mpya iwe na vipengere vya "right to recall" kurudisha nguvu ya kuwaondoa wabunge ambao wananchi hawaridhiki na utendaji wao wa kazi. Kutoa haki ya wagombea huru (binafsi) kuweza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pia itasaidia kuwapa wabunge uwezo wa kutetea maslahi ya wananchi wao bila ya kuwa na woga wa kufukuzwa chamani na hatimaye kupoteza nafasi zao za uongozi na hasa bungeni.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kama hujui SIASA bora ukae pembeni kuliko kujaribu ku justify vitu kutokana na unavyofikiria. Hakuna mtu ambaye anachaguliwa na watu pasipo chama kumsimamisha. Na Chama kinatawaliwa na itikadi na sera hivyo vyama viwili vyenye itikadi moja haviwezi kugombea uongozi, lazima kuwepo na tofauti baina ya vyama hivi lakini kwa Ujinga wetu sisi hasa watanzania tuloletewa hii demokrasia tunafikiri kwamba Uchaguzi huchaguliwa MTU sio chama na hata kudai Wagombea Binafsi.. haiwezekani kuwa na wagombea wawili ikiwa wote wanasimamia kitu kimoja.

  Ili kuondoa mlolongo wa watu wengi kugombea nafasi moja ndio maana demokrasia inaanza kutazama CHAMA chenye itikadi, sera na ilani ambazo lazima zitofautiane na chama kingine..kisha ndipo anachuliwa mtu mmoja kusimama kutetea kwa niaba ya chama hicho..Kwa mgombea binafsi ni lazima pia awe mpinzani wa kiitikadi, sera na ilani za vyama au watu waliojiandikisha kugombea kitaifa. Ndio maana hatuwezi kuwa na wagombea wawili toka chama kimoja sehemu moja hata kama wote wanapendwa sana kuliko wagombea wa vyama vingine. Kifupi ni lazima kuwepo tofauti ya kitikadi, kisera na kiilani baina ya wagombea wawili laa sivyo tungeona CCM wakisimamisha wagombea wawili au wote toka sehemu moja (kama tungekuwa tunachagua watu na sii vyama).

  Na mwisho mkuu wangu, swala sio kufukuzwa kwake bali ni yeye kutokubali kufuata kanuni za chama. Acha hili la kuchaguliwa na wananchi mtu anaweza kuwa kasomea kabisa elimu fulani na akanyang'anywa utumishi wake wakati hatuwezi kuindoa ile elimu kichwani mwa mhusika..Hata hao viongozi wa dini MaPadre na Masheikh wanaweza kuondolewa ktk uongozi wa dini kwa kuvuliwa mamlaka ya kuongoza. Hivyo swala sio kuvulia Uanachama bali usajili wa mhusika yeyote unatokana na kadi ya chama na unaponyang'anywa hiyo kadi ni kwa sababu umekiuka kanuni zake ktk ngazi ya uongozi...

  Kadi ni ya chama sio ya Mbunge wala Diwani hivyo zipo kanuni zinazokutaka wewe kama kiongozi uzifuate na kusimamia, kinyume cha hapo itakuwa ni kujaza watu kama ushabiki wa vyama vya Mpira..Na hata huko tunaona migogoro kibao ya viongozi wa mpira wakiuza ushindi kisha wanakataa kujiengua uongozi.. hatua zinazofuata hunyang'anywa uanachama hata kama wamechaguliwa na wananchi kwa sababu hawakuchaguliwa kwenda kuiuza timu. Lengo la kuwa na timu ya mpira ni kutafuta ushindi ambao ndio unawawezesha kuboreka kibiashara.
   
 3. Sungi

  Sungi Senior Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hujaelewa hoja, "system" inayotumika kupata viongozi yenyewe imeoza na ndio chimbuko ya kuhamisha nguvu ya wananchi kuchagua viongozi wao na badala yake chama ambacho pengine kinaweka mbele maslahi ya kisiasa ya kuchaguliwa kuingia madarakani "by any means necessary" na maslahi ya umma wa watanzania nyuma.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nakuelewa vizuri na sii kweli system imeoza isipokuwa sisi ndio hatufahamu..Chama ndicho huteua mtu ambaye husimama kwa niaba ya chama kuwakilisha wananchi bungeni..hakuna system iliyokuwa bora kama hiyo laa sivyo unataka kurudisha system ya Nyerere kuchagua - Jembe/Nyumba au Ukuta toka wagombea wa chama kimoja..Maslahi ya chama hutoa UONGOZI ili maslahi ya wananchi yapate MWAKILISHI, haiwezi kuwa kinyume..
   
 5. 2

  2015 Senior Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama mgombea anaona itokadi yake ni tofauti na ya chama halazimishwi kukaa, ni wajibu wake yeye kutafuta au kuanzisha chama chenye itikadi anayoitaka na sio kwenda kwenye chama ambacho unajua fika itikadi yake na yako ni tofauti halafu unajifanya unataka kuipinga.
   
 6. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Chama kwanza mengine baadaye.
   
 7. dhahabuinang'aa

  dhahabuinang'aa Senior Member

  #7
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu kama hujui siasa unakaa pembeni bwana.
   
 8. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Asikae pembeni bali aulize ili aelimishwe!
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  haya yamekuja baada ya kasheshe la Chadema na madiwani wakaidi............................vyama vya siasa vyote vina walakini mkubwa wa kidemokrasia...............haiwezekani mtu achaguliwe na tarafa halafu viongozi wa kitaifa wa chama chake wamvue madaraka na uanachama kwa kuwasikiliza au kutowasikilia wao.....................democracy in tz is and has always been a big joke.........................wagombea wote wa ubunge ni watalii kwenye majimbo yao.......................wao kimsingi ni wakaazi wa Dar........
   
 10. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  <br />
  Kwa hiyo akifanya madudu, esp yale ya kununuliwa na magamba, waangaliwe tu?
  Wake up please!
   
 11. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #11
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,451
  Likes Received: 2,502
  Trophy Points: 280
  Cra crap crap
   
Loading...