Kufukuza na kusimamisha kazi watumishi wa umma

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
2,397
1,011
Mwanajamii mwenzangu unadhani mtindo unaoendelea sasa hivi wa kuwawajibisha watumishi wa umma kwa kuwafukuza au kuwasimamisha kazi kutokana na uzembe au challenges zinazowakabili katika vituo vyao au kwa vyovyote vile inaongeza UTENDAJI WA WATUMISHI MAKAZINI AU UNAWAFANYA wafanye kazi kwa bidii au unafukiri nini
 
Mm sipendi kinachoendelea taaratibu za utumishi zifatwe kujieleza onyo then kusimamishwa naumia kweli
 
Sina objection yeyote kuhusu wafanyikazi wasio timiza wajibu wao kufukuzwa.Ni sawa kabisa,kama mfayanyikazi kafanya kosa linalostahili yeye kufukuzwa kazi afukuzwe tu,hii itaongeza nidhamu kazini kwa watumishi wengine.Hata hivyo ni lazima sheria za kazi zifuatwe na mfanyikazi asidhalilishwe katika hali yeyote ile.
Mwanajamii mwenzangu unadhani mtindo unaoendelea sasa hivi wa kuwawajibisha watumishi wa umma kwa kuwafukuza au kuwasimamisha kazi kutokana na uzembe au challenges zinazowakabili katika vituo vyao au kwa vyovyote vile inaongeza UTENDAJI WA WATUMISHI MAKAZINI AU UNAWAFANYA wafanye kazi kwa bidii au unafukiri nini
 
Na vyama vya wafanyakazi vipo kmya
Kuna ngazi za utumishi ambapo huruhusiwi tena kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi kwa kuwa nawe ni part ya menejimenti.
Nafasi zote za uteuzi huwezi kutetewa na chama cha wafanyakazi kwa kuwa sio tena mwanachama wao
 
Nimekua nikirudia kwamba kwajinsi serikali iliyopita ilivyokua inafanya kazi, atawafukuza au kuwasimamisha wote.

Yeye mwenyewe mapungufu mengi anayoshughulika nayo sasa hivi kwa kusimamisha watu kazi aliyaona wakati wa utawala uliopita lakini hakua na cha kufanya, hali kadhalika kuna viongozi/watendaji wengi ambao walitamani kufanya tofauti lakini mfumo iliwanyima hiyo nafasi.

Huenda hata angekamata madaraka mwingine, angemsimamisha mheshimiwa kama sio kukosoa utendaji wake.
 
Mwanajamii mwenzangu unadhani mtindo unaoendelea sasa hivi wa kuwawajibisha watumishi wa umma kwa kuwafukuza au kuwasimamisha kazi kutokana na uzembe au challenges zinazowakabili katika vituo vyao au kwa vyovyote vile inaongeza UTENDAJI WA WATUMISHI MAKAZINI AU UNAWAFANYA wafanye kazi kwa bidii au unafukiri nini
Kuna fidia nyingi sana zinakuja kutokana na timuatimua hii isiyofuata utaratibu na yote hii ni maandalizi ya kumharibia makomeo
 
Kuna ngazi za utumishi ambapo huruhusiwi tena kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi kwa kuwa nawe ni part ya menejimenti.
Nafasi zote za uteuzi huwezi kutetewa na chama cha wafanyakazi kwa kuwa sio tena mwanachama wao
Kwanza mm sioni kazi ya hivi vyama now nipo kazin 3yrs sijajiunga zaidi ya kupiga hela tu but naongelea watendaji wa kata na vijiji waliowekwa ndani jana kwa kosa la wakala kupandisha bei ya pembejeo za kilimo tofauti na bei elekezi
 
Ww ulitaka wafanyweje? Au uliipenda ile ya kumhamisha kutoka idara flan kwenda idara nyingne?
Hivi nyinyi watu mnataka nn?
 
I
Kuna fidia nyingi sana zinakuja kutokana na timuatimua hii isiyofuata utaratibu na yote hii ni maandalizi ya kumharibia makomeo[/QUOalaaaaa inawezekana au lasivyo WATUMISHI wataishia hela maskini wanatia huruma sana wanavyokamatwa na polisi
 
Ww ulitaka wafanyweje? Au uliipenda ile ya kumhamisha kutoka idara flan kwenda idara nyingne?
Hivi nyinyi watu mnataka nn?
Hujaelewa soma tena ndugu then uje uniulize swali nikujibu kisomi si kisiasa kama ulivyokaririshwa na wenzako
 
Nimekua nikirudia kwamba kwajinsi serikali iliyopita ilivyokua inafanya kazi, atawafukuza au kuwasimamisha wote.

Yeye mwenyewe mapungufu mengi anayoshughulika nayo sasa hivi kwa kusimamisha watu kazi aliyaona wakati wa utawala uliopita lakini hakua na cha kufanya, hali kadhalika kuna viongozi/watendaji wengi ambao walitamani kufanya tofauti lakini mfumo iliwanyima hiyo nafasi.

Huenda hata angekamata madaraka mwingine, angemsimamisha mheshimiwa kama sio kukosoa utendaji wake.
Kabsaa coz umebase kumfukuza kazi au kumsimamisha lakin changamoto za kazi hutatui watendaji wa kata na vijiji hawana ofisi wala nyumba za kuishi na mengineyo ni bora wakawasikiliza na wao kabla ya kumtimua kazi
 
Tufike mahala tusijitoe faham. MTU kapewa dhamana kisha kaliibia taifa nawe unalalamika kwa mtu huyo kufukuzwa!!! Ama kweli kizazi cha nyoka. Hizo taratibu unazotaka ivi ziko juu ya mamlaka ya rais? Huyo mtu hiyo nafasi hakuifanyia interview Bali aliteuliwa na aliyemteuwa kamtengua uteuzi wake. Then your coming na hii kitu ili uonekane mtetezi wa wezi au unataka kutuambia kuwa mtu akikutwa kaliibia taifa aachwe?! Tena wanabahati sheria bado inawafanya wakisimamishwa waendelee kulipwa , mie nataka mswada wa kuibadiri hiyo sheria. Mtumishi wa umma akigundulika kuliibia taifa pale afutwe kazi,vyeti vyake vichanwe,na afilisiwe kabisa. Hii ndio suruhu la mtumishi kutumia cheo kuiba.
 
Kama wewe ni mzembe, kama wewe ni mungumtu kwenye ofisi na kitengo chako cha umma kwa awamu hii "utatoka tuu" maana hakuna namna nyingine sasa. Mimi ni mtumishi wa umma, naunga mkono kumweka pembeni mtumishi mzembe, mbadhirifu na asiyezingatia maadili ya kazi.
Ila nashauri usimamishaji na ufukuzaji huu ufuate sheria sababu serikali itakuja kulipa fidia kutokana na kukurupuka kwa viongozi katika kufukuza na kuwekana ndani bila sababu dhahiri.
 
JK mlimuita dhaifu na kila majina ya kumbeza JPM anafanya kweli mnalalamika.
Rais mpaka anachukua hatua ya kufukuza kazi mtumishi mjue kapata ushauri wa kutosha na kajiridhisha sasa baadhi yetu humu tunajifanya tunajua sheria,taratibu na kanuni za utumishi kuliko taasisi ya rais.

Mnataka afanyaje.
 
Mikataba yote duniani inaweka wazi matokeo ya kutotimiza wajibu kwa mwenye kuingia mkataba, na huwa inasainiwa baada ya kueleweka, so kama unafanya kazi kwa uadilifu, unawasiwasi gani? Na yule asiyetimiza majukumu, kwa nini asichukuliwe hatua stahiki? Sheria zipo ndo maana wanazitumia!
 
Acheni kufanya kazi kwa mazoea siyo kulalama kila mara. Kwanza wapelekwe mahakamani kabisa
 
Back
Top Bottom