mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,760
- 35,205
Habari za watu kufa na kuzikwa na baadae kupatikana wakiwa hai ni za kushangaza mnooo.
Yaani mtu amekufa kwa kuugua au ajali au ghafla tuu, hospitalini wanahakikisha amekufa na wanatoa cheti cha kifo na mwili mnakadhiwa, mnaenda kuzika na viongozi wa serikali za mtaa, viongozi wa dini na familia wanashiriki na kusema Mungu amempenda zaidi.
Imagine wafiwa wanaomboleza na kusahau kisha baada ya muda marehemu anapatikana yupo hai katika hali tata. Hili jambo ni la kutisha na kushangaza sana na ni jambo linalodhihirisha uwepo watu wengi wanaodhaniwa wamekufa lakini inawezekana kabisa wapo kama walivyopatikana hawa.
Waandishi wa habari nadhani huu ni muda muafaka wa kulifanyia hili jambo habari za uchunguzi wa kina. Uchunguzi ambao utasaidia kujua haswa ni nini kinatokea hadi binadamu anaonekana amekufa, tena kitabibu kabisa mahospitalini, anazikwa na kisha anapatika akiwa hai.
Hizi habari zinagusa uhai wa mwanadamu lakini bahati mbaya hazipewi airtime kivileee na medias rasmi wala zile za udaku wala hazifanyiwi uchunguzi utakaoisaidia jamii mbeleni. Badala yake habari Zinazokik ni zile za Connections (ngono) na hapa ndio utagundua nguvu gani imeshikilia mitandao ya kijamii
Mungu atusaidie kumtafuta yeye na nguvu zake