Kufufua misekule ama wafu na kuwaweka mbele ya kanisa ili watoe ushuhuda wa huko kuzimu. Hakuwezi kuwafanya watu watubu na kuwa wema

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,640
4,426
Ni neno la Mungu pekee ndilo linaweza kumfanya mtu akawa kiumbe kipya. Biblia inasema hivi:-

29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu. LUKA 16.

Musa na Manabii ina maanisha maandiko matakatifu@"Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe. LUKA 24:27.

Hivyo injili yoyote ambayo inajengwa katika mashuhuda ya kuzimu, haipo kwa jinsi ya Kristo bali yule adui ambaye silaha yake kubwa ni kutia HOFU katika nyoyo za WAUMINI ili awatawale apendavyo. Yesu alimfufua Lazaro kutoka katika kaburi ambalo alikuwa amezikwa na kuoza kwa mda wa siku nne, lakini hakuna mahali alimweka Lazaro mbele kutoa ushuhuda wa kuzimu ili YESU ajipatie wafuasi wengi. Zaidi tunaona Yesu akiwaambia, wamfungue Lazaro Sanda na, wamwache aende zake. Na wakuu wa dini ya Kiyahudi walichukizwa sana kwa kitendo cha Yesu kumfufua Lazaro, wakaweka njama kumuua Yesu na Lazaro pia. [Yohana 11:46-57; 12:10].

Yesu alifanya mengi sana ya kustajabisha; na Mtume Yohana anasema kuwa, "Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini;[Yohana 12:37]. Leo mtu anafanya kamujiza kamoja tu, basi inakuwa matangazo katika vyombo vya habari, na mwenye kufanyiwa mujiza anapewa MAIKI na kuanza kutangaza hivi na vile. Si bure kuna kitu nyuma ya pazia.......

Lakini Bwana Yesu alipotenda mujiza hasa wa kufufua wafu, hasa pale alipomfufua binti wa miaka 12, binti wa mkuu wa Sinagogi; Biblia inasema hivi, " Akawaonya sana [wazazi wake], mtu asijue habari ile [ya kufufua]; Marko 5:43. Na kabla ya kumfufua huyo binti aliwafukuza watu waliokuwa katika maombolezo watoke katika nyumba hiyo, na akabakiwa na wazazi wake, pamoja na Petro, Yakobo na Yohana, kisha ndipo akafanya muujiza wa kufufua. Ni dhahiri Yesu hakutaka sifa kutoka kwa wanadamu bali daima alifanya kila jambo kwa kumpendeza BABA yake[yaani Mungu].

Wengi wa watenda miujiza wa leo, ni wapiga dili, wapo kibiashara zaidi; hutafuta sifa kwa matendo hayo wayafanyayo ili wavutie watu na kujaza majengo yao makubwa na kupata maslahi. Kwa njia hiyo huvuna pesa nyingi na kuwa matajiri na kuanza kutambiana katika MEDIA. Hao ni Mafarisayo wa kileo; Yesu alishawanena toka zamani.

4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. 5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, 7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. [Mathayo 23].

Mafarisayo wa leo hawaitwi RABI, bali wanapenda kuitwa BABA au DADY.Hupenda viti vya mbele kwa kila hafla, na katika makanisa utawakuta wako katika viti vya mbele, tena viti vyao vinapendeza na vipo wakfu kwajili yao tu. Na wakiwa hapo mbele ufanya vioja vingi ili watazamwe na watu katika TELEVISION nk. Na huwabebesha waumini mizigo mizito ya ZAKA, MATOLEO, KUPANDA MBEGU, MALIMBUKO, CHUMVI ZA UPAKO, MAJI YA UPAKO, MAFUTA YA UPAKO, VITAMBAA VYA UPAKO na mengine mengi yafananayo na hayo. Lakini wao, wake zao na watoto wao hawagusi hata kwa kidole chao cha mwisho. Wao hunenepa kwa kujawa na wingi wa sadaka, na mtu awaye yote akiwapinga katika matoleo humwandalia vita. Na mahubiri yao ni AMANI AMANI tu, maana hawataki bugudha katika ULAJI wao. Walishatabiriwa kitambo:-

Bwana asema hivi katika habari za manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote ASIYETIA KITU VINYWANI MWAO, WAO HUMWANDALIA VITA. [Mika 3:5]

Na wafuasi wao kwa kuwa hawana mda wa kusoma NENO bali wanao mda wa kuongozwa na wachungaji sampuli hii, daima huwa kondoo waliopotea na kuangamia. Biblia inasema hivi:-

Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.[Yeremia 50:6].

Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia.[Isaya 9:16]

Hukumu ya wachugaji hawa itakuwa kubwa sana.

“Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea UHARIBIFU usiokawia.Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.Na katika kutamani WATAJIPATIA FAIDA KWENU KWA MANENO YALIYOTUNGWA; ambao HUKUMU YAO TANGU ZAMANI HAIKAWII, WALA UVUNJIFU WAO HAUSINZII. [2 Petro 2:1-3]”

" Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.[Yeremia 25:34]

Tokeni kati yao kwa kumgeukia Kristo aliye mchungaji mkuu wa kweli.
 
Waraka wako huu nadhifu, wanatakiwa kuusoma pia kina askofu Gwajima, Mzee wa upako, Mbunge Rwakatare Getrude na wengineo wenye mahubiri yenye kufanana na matendo yaliyotajwa kwenye uzi huu.

Wewe siyo wa kwanza 'kuzindua' akili za masikini wabaoendelea kukandamizwa kiuchumi kila uchao na haya makanisa yanayoota kama uyoga yenye malengo ya kujitengenezea utajiri kwa sababu ya ujinga wa watu.

Shida zao na maradhi yao wameyapeleka kuyakabidhi kwa wachungaji, waliowalisha kwa hila 'bhangi' za kiimani na kuwatia 'chaka' wasielewe njia za kutoka na kujinasua, bali imani na furaha zao zote waneziwekeza kwa hao chui wararuao waliojivisha ngozi ya kondoo.
 
Waraka wako huu nadhifu, wanatakiwa kuusoma pia kina askofu Gwajima, Mzee wa upako, Mbunge Rwakatare Getrude na wengineo wenye mahubiri yenye kufanana na matendo yaliyotajwa kwenye uzi huu.

Wewe siyo wa kwanza 'kuzindua' akili za masikini wabaoendelea kukandamizwa kiuchumi kila uchao na haya makanisa yanayoota kama uyoga yenye malengo ya kujitengenezea utajiri kwa sababu ya ujinga wa watu.

Shida zao na maradhi yao wameyapeleka kuyakabidhi kwa wachungaji, waliowalisha kwa hila 'bhangi' za kiimani na kuwatia 'chaka' wasielewe njia za kutoka na kujinasua, bali imani na furaha zao zote waneziwekeza kwa hao chui wararuao waliojivisha ngozi ya kondoo.
Wakiona huu waraka walai nitakuwa adui wao awapendi wakosolewe kwa chochote
 
TAG na makanisa yote ya kilokole yanatumia sana huu mtindo na upo
Kaka TAG inaendeshwa na katiba hairuhusiwi hiyo mavitu kabisaaaa ,tena unafukuzwa asubuhi ,hapa ni kuhubiri injili ya kristo na uokovu ,sadaka inahubiliwa ila sio zaidi ya 20% ya mahubiri ,haiendeshwi na utashi wa mtu mmoja
 
Hakuna misukule au wafu wanaofufuliwa na hao matapeli. Hao wanaodaiwa kuwa misukule au wafu wanakubali kutumiwa na hao matapeli wanaojifanya ni manabii uchwara kwa sababu ya njaa.

Mwisho let love be our religion.
 
Kaka TAG inaendeshwa na katiba hairuhusiwi hiyo mavitu kabisaaaa ,tena unafukuzwa asubuhi ,hapa ni kuhubiri injili ya kristo na uokovu ,sadaka inahubiliwa ila sio zaidi ya 20% ya mahubiri ,haiendeshwi na utashi wa mtu mmoja
TAG hii aliyeiacha marehemu moses kulola au nyingine ndugu
 
Back
Top Bottom