Kufuatia vifo watu 14 wakiwemo waandishi 6, Rais toa maelekezo misafara ya viongozi

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Kwa heshima na taadhima namwomba Mhe. Rais SSH atoe maelekezo kuhusu misafara ya viongozi wa Serikali kupunguza au kuepusha ajali zisizo za lazima.

Hakuna ulazima wa Waziri, RC au DC kuwa na msururu wa magari na mrundikano wa waandishi wa habari kwene gari moja. Waandishi aidha waqe na private car au wajigawe kwenye gari chache zikizoko kwene msafara ikiwemo ya Mkuu wa msafara: Waziri, RC, DC au Mbunge.

Shughuli za ukaguzi wa miradi iliyoko mikoani, wilayani au kata ifanywe na Viongozi wa maeneo husika na watoe mrejesho kwa mamlaka zilizoko juu.

Maafisa habari wa Halmashauri za Wilaya na Majiji ya Mikoa wa-share info na media zote kwa simu au rununu.

Kuwe na idadi maalumu ya magari machache kwene msafara husika na Jeshi la Polisi lihusike kuhakikisha usalama wa msafara husika.

Ajali yoyote kwene msafara husika Mkuu wa Msafara awe Waziri. RC DC au MP awajibike.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom