Kufuatia ushindi wa Arsenal, Man United warudi mtaa wa sita

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Arsenal imeimarisha matumaini yao ya kutaka kuwa katika timu nne bora katika jedwali la Uingereza kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton.

Mabao hayo yalifungwa na Alexi Sanchez na Olivier Giroud.

Baada ya kipindi cha kwanza kilichokosa mchezo mzuri Sanchez aliwashangaza wengi baada ya kuwachenga walinzi wa Southampton na kisha kucheka na wavu.

Mchezaji wa ziada Giroud ambaye aliingia mahala pake Wellbeck aliimarisha ushindi huo kwa kufunga kwa kichwa muda mfupi baada ya kuingia uwanjani.

Southampton hawakufanya mashambulizi mengi katika safu ya ulinzi ya Arsenal.

Fursa yao kuu ilikuwa katika kipindi cha kwanza wakati Manolo Gabbiadini alipopiga mkwaju uliookolewa na Petr Cech.

Ushindi huo unamaanisha kwamba Arsenal inapanda juu ya Manchester United katika nafasi ya 5 ,alama tatu nyuma ya Manchester City.
 
1st to reply,,, watakuja maana walikaribishwa ugenini kwa mida sasa wamerud kwao pale pale
 
Man United tunachukua Uefa ndogo,Asenane fail to make top 4&Sanchez leave Asenane...Wenger kuendelea kuinoa Arsenal....
 
Yaani maisha ya mpira jamani nyie acheni tu. Yaani Arsenal na Man Utd ndiyo wa kugombea nafasi ya nne kana kwamba hajawahi kubeba kombe la ligi kuu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom