Kufuatia Umuhimu wa Maandamano ya UKUTA: Nimehamasika, Nitashiriki, Tujitokeze kwa Wingi! Ila...!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,463
113,532
Wanabodi,

Haki ya kuandamana, kukusanyika, kuhudhuria mikutano, kushiriki kwenye shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii, ni miongoni mwa haki za msingi za binaadamu zilizot
olewa na katiba yetu, hivyo hakuna mtu awaye yote, wala mamlaka yoyote yenye uwezo au mtu yoyote uwezo, hata Rais wa JMT, hana mamlaka wala uwezo wa kuziondoa haki hizo, unless kama mtu huyo ni dikiteta kwa kujiweka juu ya katiba!.

Hivyo baada ya kutafakari kwa kina umuhimu wa maandamano haya na mikutano ya UKUTA nchi nzima hapo September mosi, nimeamua kwa dhati ya moyo wangu, nitashiriki kikamilifu katika maandamano hayo na mikutano hiyo, bila kikwazo chochote, na kwa tangazo hili, natoa wito, kwa wale Watanzania wengine wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, bila kujali vyama vyetu, tujitokeze kwa wingi, kuyaunga mkono maandamano na mikutano hiyo.

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia vyama vingi inayoendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, na hakuna chombo chochote kilicho juu ya katiba, hivyo hata rais wa JMT, yuko chini ya katiba, aliapa kuilinda kuitii na kuitekeleza katiba ya JMT, hivyo jambo lolote litakalofanywa na rais ni lazima liwe kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais hana mamlaka ya kufanya jambo lolote nje ya katiba ya JMT!. Hivyo kama kuna jambo lolote, rais amelisema, amelitenda au amepanga kulitenda, kwa mujibu wa katiba, hilo ni jambo halali na lazima tulitii!.

Ila pia rais ni binadamu na sio malaika, hivyo kuna wakati anaweza kukosea kibinaadamu, hivyo iwapo kuna jambo lolote ambalo rais amelipanga, amelisema, amelitenda, ambalo linakwenda kinyume cha katiba ya JMT, jambo hilo ni haramu!, kwa vile kauli ya rais ni sheria, rais akifanya jambo lolote kinyume cha katiba, mamlaka pekee kwa mujibu wa katiba, yenye uwezo wa kuitafsiri katiba, sheria, taratibu na kanuni, sio maandamano, wala mikutano ya siasa bali ni Mahakama Kuu ya Tanzania!. Kuandamana na kuhudhuria mikutano ni kuonyesha ushirikiana na mshikamano tuu kuhusu hoja ya msingi, na hakuwezi kuzuia uvunjwaji wa katiba!, njia halali ya kuzuia uvunjwaji wa katiba, unaofanywa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kupitia Mahakama Kuu, na ikithibitishwa rais wa JMT amevunja katiba, then anapaswa kuondolewa kwa mujibu wa ibara ya 56A ya katiba ya JMT.

Vyama vya siasa, navyo vipo kwa mujibu wa katiba, na vinaongozwa kwa sheria, taratibu na kanuni, hivyo jambo lolote ambalo vyama vimepanga kulifanya yakiwemo hayo maandamano ya UKUTA, lazima litekelezwe kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, hivyo ni mihimu sana, vyama, vikawaandaa wanachama, wafuasi wao, na washabiki wao kutii sheria bila shuruti!.

Kama katiba ilivyoelekeza na sheria inavyosema, kila sheria, pia inazo kanuni zake za utekelezaji wa sheria hizo, hivyo haki hiyo ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa, imetolewa kikatiba na kisheria na kutungiwa kanuni za utekelezaji!, hivyo nawasihi sana viongozi wa vyama, kuhakikisha wamefuata sheria, taratibu na kanuni za kufanya maandamano, na mikutano, ikiwemo kupatikana kwa vibali vya kufanya maandamano hayo na mikutano hiyo, ili maandamano hayo na mikutano hiyo iwe ni halali, sisi raia wema tunaopende kufuata sheria bila shuruti, tujitokeze kwa wingi tukiwa vifua mbele kuyaunga mkono maandamano hayo na kuandamana.

Japo haki ni stahiki, inapaswa kutolewa, na isipotolewa, haiombwi bali hudaiwa, na hailetwi kwenye kisahani cha chai, bali hupiganiwa!, na sometimes hugharimiwa kwa gharama ya machozi, jasho na damu, lakini ikitokea kwa sababu zozote zile za msingi, maandamano hayo yakanyimwa vibali ama kwa sababu za kiusalama, ama kwa taarifa za kiintelijensia, then kuandamana bila vibali au kuhudhuria mkutano wa kisiasa usio na kibali, ni uvunjani wa sheria!.

Hili likitokea, natoa wito kwa Watanzania wenzangu, kamwe tusikubali kuswagwa na wanasiasa wowote, kufanya vitendo vyovyote kinyume cha sheria, taratibu na kanuni, hivyo tusithubutu kushiriki maandamano na kuhudhuria mikutano yoyote isiyo na vibali! ni kinyume cha sheria!.

Hoja ya UKUTA ni hoja nzuri, tuiunge mkono kwa dhati, ila lazima utekelezaji wake uwe ni kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na tufuate sheria, bila shuruti.

Pasco.

Rejea:
Ushauri wa Bure Kwa Chadema: Japo Ni Haki, Lakini Chonde Chonde ...
 
Wanabodi,

Haki ya kuandamana, kukusanyika, kuhudhuria mikutano, kushiriki kwenye shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii, ni miongoni mwa haki za msingi za binaadamu zilizo kwenye katiba yetu, hivyo hakuna mtu awaye yote, mwenye uwezo wa kuziondoa haki hizo, unless kama mtu huyo yuko juu ya katiba!.

Hivyo baada ya kutafakari kwa kina umuhimu wa Maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima hapo September mosi, nimeamua nitashiriki kikamilifu katika maandamano hayo na mikutano hiyo, bila kikwazo chochote, na kwa tangazo hili, natoa wito, kwa wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, tujitokeze kwa wingi, kuyaunga mkono maandamano na mikutano hiyo.

Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa kufuata katiba, sheria na kanuni, na hakuna chombo chochote kilicho juu ya katiba, hivyo hata rais wa JMT, yuko chini ya katiba, aliapa kuilinda kuitii na kuitekeleza katiba ya JMT, hivyo jambo lolote litakalofanywa na rais ni lazima liwe kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais hana mamlaka ya kufanya jambo lolote nje ya katiba ya JMT!. Hivyo kama kuna jambo lolote, rais amelisema, amelitenda au amepanga kulitenda, kwa mujibu wa katiba, hilo ni jambo halali na lazima tulitii!.

Ila pia rais ni binadamu na sio malaika, hivyo kuna wakati anaweza kukosea kibinaadamu, hivyo iwapo kuna jambo lolote ambalo rais amelisema, amelitenda, ama amepanga kulitenda ambalo linakwenda kinyume cha katiba ya JMT, mamlaka pekee kwa mujibu wa katiba, yenye uwezo wa kutafsiri sheria, sio maandamano, wala mikutano ya siasa bali ni Mahakama Kuu ya Tanzania!. Kuandamana na kuhudhuria mikutano ni kuonyesha ushirikiana na mshikamano tuu kuhusu hoja ya msingi, na hakuwezi kuzuia uvunjwaji wa katiba!.

Vyama vya siasa, navyo vipo kwa mujibu wa katiba, na vinaongozwa kwa sheria, taratibu na kanuni, hivyo jambo lolote ambalo vyama vimepanga kulifanya yakiwemo hayo maandamano ya UKUTA, lazima litekelezwe kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, hivyo ni mihimu sana, vyama, vikawaandaa wanachama, washabiki na wafuasi wake kutii sheria bila shuruti!.

Kama katiba ilivyoelekeza na sheria inavyosema, kila sheria, pia inazo kanuni zake za utekelezaji wa sheria hizo, hivyo haki hiyo ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa, imetolewa kisheria na katiba na kutungiwa kanuni za utekelezaji!, hivyo nawasihi viongozi wa vyama, kuhakikisha wamefuata sheria, taratibu na kanuni za kufanya maandamano, na mikutano, ikiwemo kupatikana kwa vibali vya kufanya maandamanano hayo na mikutano hiyo, ili maandamano hayo na mikutano hiyo iwe ni halali, sisi raia wema tunaopende kufuata sheria bila shuruti, tujitokeze vifua mbele kuandamana na kuyaunga mkono!.

Japo haki haiombwi, bali hudaiwa, na hailetwi kwenye kisahani cha chai, bali hupiganiwa!, lakini ikitokea kwa sababu zozote zile za msingi, maandamano hayo yakanyimwa vibali ama kwa sababu za kiusalama, ama kwa taarifa za kiintelijensia, then kuandamana bila vibali au kuhudhuria mkutano wa kisiasiasa usio na kibali, ni uvunjani wa sheria!.

Hili likitokea, natoa wito kwa Watanzania wenzangu, kamwe tusikubali kuswagwa na wanasiasa wowote, kufanya vitendo vyovyote kinyume cha sheria, taratibu na kanuni, hivyo tusithubutu kushiriki maandamanano na kuhudhuria mikutano yoyote isiyo na vibali! ni kinyume cha sheria!.

Hoja ya UKUTA ni hoja nzuri, tuinge mkono kwa dhati, ila lazima utekelezaji wake uwe ni kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na tufuate sheria, bila shuruti.

Pasco.

Rejea:
Ushauri wa Bure Kwa Chadema: Japo Ni Haki, Lakini Chonde Chonde ...
Wewe ni Paskali au ni Pasco? Yule wa Mwanza mwandishi wa habari? Kama ni yeye msimuamini tafadhali.
 
Serikali yetu imeshasema awamu hii wamebadilisha utaratibu, watafwata wale Viongozi hivyo Mbowe, Lisu &Co. mjiandae!

Pasco wakati mwingine inakuwa ni vigumu kukuelewa ila leo nimekuelewa kwa ufupi sana nkuambie hakuna mkutano wowote au maandamano yatayofanyika bila kupata kibali cha polisi na polisi ambao watazuia maandamano na mikutano bila sababu za msingi wataenda kujibu mashtaka hayo mahakamani naelewa nguvu ya polisi inayotaka kutumiwa kwa siku hiyo. Maandalizi yote operesheni #UKUTA yataendelea kama ratiba ilivyopangwa nchini nzima .
 
Back
Top Bottom