Kufuatia mazingira mabaya ya biashara, Moil yafunga biashara Tanzania yahamia uganda na Congo

Inasikitisha kuona watanzania na wachanhiaji wengi hawana details/facts.. wanaongea blah blah tu. Kama hatujui tukae kimya Jaman .
Vichwa empty kabisa... tufuatilie mambo ndugu zangu
 
Kwann usimtakie kila la heri huko anapoenda kutengeneza ajira mpya? Ni vigezo gani unatumia kusema ni wakwepa kodi? Inawezekana kwa sasa soko lipo vizuri huko anapoenda. Wewe unajua mshauri wake wa biashara kamshauri nn juu ya future ya biashara yake? Usitoe tu conclusion unless Una uhakika na usemacho. Wakati unacoment usiwaze kukomoa upinzani, angalia uhalisia wa jambo lenyewe. Mjukuu wako anaweza kuja kuwa muajiriwa wa hii kampuni huko mbeleni. Hujui haya maisha yatapeleka wapi kizazi chako. Ila kama Una uhakika ni wakepa kodi sawa.
Umesema kweli mkuu. "Usifungue kinywa unless unachokitoa kina lengo la kujenga"nauheshimu sana huu ujumbe.. Tatizo letu tunapenda kupiga soga na maneno ya jioni hovyo.
 
Lake Oil/Gas nao wamehamia Congo. Mwezi jana niliongozana na malori yao yenye usajli wa namba za Congo. Naona wamehamishia majeshi yao(isomeke biashara) huko Congo.
Malori mengi mbona yamehamishiwa Zambia na Congo, masikini ndo wanaosoma namba,matajiri wana exposure wao ni kuhamisha mitaji tu.Wanaangalia nchi yenye fursa.
 
Ukichunguza zaidi utakuta hayo ndo miongoni mwa yale makampuni ya mafuta ambayo yalikuwa yanakwepa kodi kwa njia ya on transit!!!.
Ukichunguza zaidi utakuta hayo ndo miongoni mwa yale makampuni ya mafuta ambayo yalikuwa yanakwepa kodi kwa njia ya on transit!!!.

hizi ndo fikira za haraka za kata product, ujinga huuu ndo unaenda kuiua Tanzania, mnachotaka kudefend ni kwamba hakuna mazingira mabaya Tanzania? kwenye uchumi kuna kitu tunaita Multiplier effect, hii haiwezi kumuacha mtu salama, usidhan uko safe brother, utaguswa tu na ninavyojua asilimia kubwa ya watu huwa wanaamini wakifikiwa, seeing is believing ndo nature yetu, anyways, kwa wale wenye macho makubwa na akili kubwa wanaona na kujua kwamba hali ya nchi is too alarming.
 
Moody's wame rate nchi yetu kama B-, we are pushing to junk now, tafsiri yake ni kubwa in economics space, tutegemee zero investors now kwenye nchi, kama Mazingira mazuri unadhan kwanni potential investors wanayeyuka? can someone think? tutulie.
 
3-620x308.jpg

Mmiliki wa Kampuni ya mafuta ya Moil, Shanif Mansoor

KAMPUNI ya mafuta ya Moil, inadaiwa kuwa imeanza kuondoa biashara zake za uuzaji wa mafuta nchini na kuzihamishia katika nchi za Uganda na Congo kwa kile kinachotajwa kuwa kwa sasa Tanzania mazingira ya uwekezaji sio mazuri.

Moil inatajwa kumilikiwa na mbunge wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza, Shanif Mansoor (CCM) na Altaf Mansoor (Dogo), ambao wanamiliki vituo vya mafuta kadhaa hapa nchini.

Taarifa za ndani kutoka katika kampuni hiyo zinaeleza kuwa wamiliki wa kampuni hiyo wamelazimika kuondoa biashara nchini kutokana na mazingira ya kiuwekezaji kwa sasa nchini siyo rafiki.

Chanzo hicho cha ndani kutoka katika kampuni hiyo kinameueleza mtandao huu kuwa, kwa sasa tayari magari makubwa ya mafuta ya kampuni hiyo yamebadilishwa usajili wa namba za Tanzania na sasa zimesajiliwa kwa usajili wa nchi za Uganda na DR Congo.

“Wakurugenzi wao wanasema Tanzania sasa hivi biashara siyo nzuri na ufanyaji wake umekuwa mgumu na faida hakuna hivyo wamelazimika kuanza kuondoa biashara zao na kuzihamishia katika nchi za Uganda na DR Congo,” kilisema chanzo hicho.

Pia chanzo hicho kimebainisha kwamba uongozi wa kampuni hiyo ulikuwa umeanza kuondoa biashara zake nchini kwa muda mrefu lakini kwa gari hizo kumi za usafirishaji mafuta, usajili wa namba zake ulianza Februari 27 mwaka huu.

Kampuni ya Moil, ambayo ina vituo vya mafuta vitatu jijini Mwanza, inadaiwa kwa sasa gari inayosambaza mafuta kwenda jijini humo ni moja tofauti na awali zaidi ya gari kubwa za mafuta kuanzia 10 zilikuwa zikisambaza kwenye vituo hivyo.

Aidha chanzo hicho kimeendelea kudai kuwa pamoja na wanahisa wengine kushinikiza kuondolewa kwa biashara zao nchini pia mbunge wa sasa wa jimbo la Kwimba amekuwa akidai kuwa hana mpango wa kugombea tena ubunge mwaka 2020.

Kutoendelea kwa Mansoor katika nafasi hiyo pia kunadaiwa kuchangia kuhamishwa kwa Biashara za kampuni hiyo kwenda nchi hizo.

Mmoja wa wakurugenzi hao, Shanif Mansoor alipotafutwa kwa njia ya simu zaidi ya mara nne kwa nyakati tofauti ili kuzungumzia suala hilo, simu yake ya mkononi iliita bila majibu.
Ukiwa na pesa unapata mashabiki hata kwa matatizo yako. Alipoanzisha biashara hatukufahamishwa, anaondoka tunafahamishwa. Kuna nini cha maana? Mbona wauza alovera wameacha? Mbona mahindi yameshuka bei? Ni mazingira ya biashara? Afike salama badala ya kutafuta advocates wa biashara ya mafuta.
 
Wawekezaji wameshindwa kwenda na speed yetu kali ya kukua kwa uchumi
 
Congo kwenye mavita Luna mazingira mazuri ya biashara kuliko tz? Tz Luna zaidi ya vita. Ile ripoti kuhusu hali ya furaha duniani ni ya kweli kabisa. Nchi yangu kwa sasa hoooooovyooooo kabisa.
 
Umesema kweli mkuu. "Usifungue kinywa unless unachokitoa kina lengo la kujenga"nauheshimu sana huu ujumbe.. Tatizo letu tunapenda kupiga soga na maneno ya jioni hovyo.
Very true. Usifungue kinywa unless..... umefupisha vizuri kabisa.
 
Hamna binadamu wa ajabu
Kama mTanzania ............Kuna mijitu inashangilia kufungwa au kufilisika kwa biashara binafsi......Hakuna nchi yetote ile unayoijua ambayo imeweza kupiga hatua kiuchumi bila involvement ya sekta binafsi........Na nchi za wenzetu wako sensitive sana na sekta binafsi maana huku mapato makubwa na ajira hupatikana............Serikali haiwezi na ninasisitiza haitaweza kufanikiwa bila sekta binafsi hata siku moja............Hata nchi za Kikomunisti kama China na Russia sekta binafsi ndo zimechochea maendeleo waliyo nayo.....................Sasa mijitu hii inayo comment ujinga kama huu ndo hiyo hiyo inalia lia Jamii Forum kila siku kwamba ajira hakuna..........Sasa mnafikiri Serikali itajenga peke yake viwanda na Economic facilities za kuajiri watu wote bila Private sectors or businesses................
 
Back
Top Bottom