Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Kufuatia mkutano mkuu wa CCM uliyoisha leo imedhihirisha baada ya kupata upinzani mkali katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 CCM imeamua kuleta mabadiliko makubwa ndani ya chama. Kwa muda wa miaka 20 CCM iliyopotea mwelekeo ikafikia hatua CCM ikiwa chama cha wafanyabiashara ambao walikuwa wakiweka mbele maslahi yao mbele, tukumbuke wakati CCM ikiasisiwa mwaka 1977 lengo la chama hicho kilikuwa kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi lakini kwa muda mrefu ilikuwa vigumu kwa wakulima na wafanyakazi kupata nafasi kugombea uongozi wowote katika chama hicho.
Nikirudi kwenye vyama vya upinzani nikianza na chama cha Chadema kwa kuangalia chama hiki bado hakijawa tayari kuaminiwa kupewa madaraka, chama Chadema toka uchaguzi mkuu uliyoisha hakija kaa chini na wanachama wake kutathimini matokeo ya uchaguzi mkuu na kupanga mikakati ya kukijenga chama kwa ajili ya kujitayarisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao badala yake viongozi wake wamebaki kulumbana na serikali iliyopo madarakani imbayo imeipa changamoto moto kubwa kwa CCM kujipanga na kurekebisha kasoro zake, tatizo lingine ni chama hiki kuendelea kupokea wanachama wanaotemwa na wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali kutoka CCM ni hii isipoangaliwa kwa chama cha Chadema kitakuwa kichaka cha wanasiasa wote wanaotemwa CCM kwa makosa mbalimbali, kitu kingine ni ukosefu wa demokrasia ndani ya Chadema tumeona chaguzi mbalimbali ya chama hiki ikifanyika bila kuwa demokrasia ya kweli kwa. mfano kuwa na Mwenyekiti wa Chama kwa muda wa miaka mingi bila kutoa nafasi ya kidemokrasia katika kupata mwenyekiti huyo.
Na kitendo cha aibu kwa chama cha Chadema pamoja na kupata ruzuku kubwa serikalini imeshindwa hata kujenga ofisi ya makao makuu na hata kulipia ofisi za chama hicho mikoani. Na kumalizia kitendo ama dhambi ya kumfanya aliyekuwa Katibu Mkuu W. Slaa kuondoka kwenye chama hicho kitaendelea kukisumbua chama hicho.
Kwa mgogoro unaoendelea katika chama cha CUF tutegemee chama hicho kumeguka mara Mbili CUF bara CUF visiwani.