Nicholaus Kilunga
JF-Expert Member
- Feb 15, 2014
- 1,188
- 570
Ningepata Nafasi yakumshauri mtu ninayemuheshimu leo hii kabla ya giza halijaingia, ningeanza na Rafiki yangu wa siku nyingi Mbobezi wa sheria, na Mwalimu wangu Prof, Palamagamba Kabudi.
Ningemwambia aitazame sana nafasi ya uteuzi wake aliyoteuliwa ya ubunge, kama sehemu ya jaribu katika maisha yake. Prof, Kabudi kuteuliwa kwako kuingia kwenye bunge bubu na kiziwi, bunge kipofu na dhaifu lenye kufuata matakwa ya kiimla ya mtu mmoja dhaifu, ni jaribu moja zito sana kwako na ni lazima ulishinde kwakuiangalia tena nafasi yako, umahiri, heshima na tajiriba uliyojijengea kwa wanazuoni wa Tanzania na Jamii nzima ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.
Labda rafikio na mwanazuoni mwenzako Prof. Kitila Mkumbo na Mzee wetu Joseph Butimu watakuwa wameteta na wewe jambo kuhusu hili jaribu kwako.
Huu utakuwa ni mpango tuu wakuzika vilio vya katiba mpya iloyosheheni maoni ya wananchi.
Nimehuzunika na nimekuonea huruma mno Prof. Kabudi. Legacy yako baba utaweza kuitunza??
Davido Ambrosihni Jr