Kufuatia Kifo Cha Mpauko Nimejikuta Katika Tafakuri

T11

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
3,045
2,000
Wakuu Salaam, Nijielekeze moja kwa moja kwenye mada husika. Jamii Forums ni jukwaa pana na pendwa sana hapa nchini tangu kuanzishwa kwake, sifa moja inayopelekea kupendwa kwake ni hali ya kuficha majina ambayo inawapa Uhuru watu wengi sana wa kutoa maoni yao ikiwemo kuelezea maisha yao binafsi jambo ambalo sio rahisi kulifanya kwa watu ana kwa ana au katika mitandao inayoweka wazi wasifu wa mtu.

Nimeanza kuutembelea huu mtandao miaka mingi kabla sijajiunga rasmi 2017, hapa niwatoe watu ile dhana kwamba ID mpya ni member mpya.

Nimekuwa na desturi ya kufuata mtiririko wa hoja na mada zinazokuwa zikitolewa humu nikagundua hii ni jamii kama jamii unayoishi nayo mtaani kwa maana ina sifa zote kama jamii halisi.

Sasa watu wanasahau hili, mtu akitoa shida zake huishia kukejeliwa utafikiri mbali na maisha ya humu kuna maisha mengine halisi

Hapana, watu wa humu ndio hao hao wa mtaani,ndio hao hao tunaishi nao, ndio hao hao wenye maisha mazuri, elimu nzuri, familia nzuri, wacha Mungu n.k.

Lakini ndio hao hao wenye matatizo, shida, talaka, manyanyaso, kufukuzwa kazi, wagonjwa n.k

Ili uamini jamii ni ile ile utagundua trends za maisha ya mtaani ndio hizo hizo za humu

Kuna wakati mtaani habari ilikuwa siasa na upinzani mkali, kuna wakati ilikuwa masuala ya Freemason kuna wakati ikawa hali mbaya za kiuchumi

Vivyo hivyo mtiririko ni huo huo humu, ikawa siasa, ikawa Freemason, ikawa nyuzi za humu zenye soko ni mambo ya willing powers, ikawa ukosoaji wa Mungu na Uumbaji, ikawa stori za kina The Bold, Mara Ujasiriamali na ghafla upepo ukageukia watu kutoa nyongo zao sasa(kutoa ya moyoni juu ya maisha yao)

Ni suala tu mmoja akifanya ikaonekana inawezekana Basi kila mtu atafanya

Tukiacha nyuzi za mambo yote tujikite kwenye hili la 'kutoa nyongo' nime-experience kitu cha kunifikirisha sana

Hapo mwanzo ilionekana mtandao huu ni wa wenye hela, wasomi nk, hii ilisababishwa na msingi wa uanzishwaji wake na watumiaji wake wa mwanzo kabla ya smartphone. Pengine ni Kweli hapo mwanzo walioweza kumudu kuingia humu ni watu wa aina hiyo lakini mabadiliko ya teknolojia yakapelekea jamii nzima mchanganyiko kuweza kuingia Jf.

Lakini bado fikra yangu ilibaki palepale kwamba huu mtandao angalau ni wa watu hata kama hawana hela lakini angalau wana elimu ya kiwango Fulani. Na wakati mwingine nilifikiri Mimi ni mmoja wa malofa wachache humu

Lakini jinsi siku zinavyokwenda nakuja kugundua kuna watu wana maisha magumu na yenye mateso mengi sana, kuna watu wanahitaji faraja, kuna watu kuingia humu ni kutafuta faraja tu ndio maana wakati mwingine tunajibizana vibaya sana, najifunza kuvumilia majibu mabaya maana huwezi jua anayekujibu yuko katika hali gani kwa wakati huo.

Niseme tu kwamba katika watu wanaoumia sana kusikia kuna member amefariki Basi ni Mimi, hasa wale ambao wanakuwa wameshasema kabla

Huwa nawaza mengi sana, binafsi japo sina mpango wa kujiua, siumwi kwa sasa wala sina shida yoyote ukiacha za kiuchumi lakini natamani sana siku nikifa humu mjue

Nimegundua kuna watu wanafariki humu bila taarifa, sasa sijui itakuwaje.

Yote kwa yote tuepuke kujibu majibu ya fedheha kwa watu wanaotoa nyongo zao humu maana mnawaongezea mateso. Tukumbuke jamii unayoishi nayo huko mtaani ndio hii hii iliyopo humu, je huko kwenu mtu anaweza kukueleza matatizo yake ukamdhihaki?

Kama huwezi kwanini umdhihaki mtu wa humu?

Au nyuzi za kina Kidukulilo ndio zinafanya tuone watu wote hawako serious na maandishi yao?

Anyway sipendi kulaumu mtu pengine tutabadilishwa na matukio yanayoendelea na sasa tutaamini katika shida za watu

Nimesoma nyuzi za watu wote waliofariki kwa kujiua ama kufariki kawaida, naumia sana sana sanaa, sijui kwanini? Saa zingine nafungua nyuzi zao, natazama username zao nawaza mengi sana

Alamsik!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MR KUO

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,229
2,000
Mkuu unaumia Nini??

Kufa Ni lazama kwa kila kiumbe.

Ila umeeleza ukweli jf imevamiwa na malofa WAPUMBAVU na mauseles wengi Sana ambao wametoka Facebook na Instagram..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: T11

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,313
2,000
Tafuteni pesa acheni kuhisi kuwa yupo mtu ama tajiri wa kukupa pesa kama msaada kama mchungji, shehe, padre wameshindwa kumsaidia mtu humu ndani Ni shida sana kupata msaada ni kama bahati

Sent using Jamii Forums mobile app
 

T11

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
3,045
2,000
Kwanza mfano mmoja tu wa Mpauko hakuwa akihitaji pesa tu na pesa alizohitaji sio za kupewa alihitaji apewe ndoano avue mwenyewe samaki

Lakini pia pengine hujasoma nyuzi nyingi, kuna wengine walikuja kusema humu wapate relief tu wala sio pesa
Tafuteni pesa acheni kuhisi kuwa yupo mtu ama tajiri wa kukupa pesa kama msaada kama mchungji, shehe, padre wameshindwa kumsaidia mtu humu ndani Ni shida sana kupata msaada ni kama bahati

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom