Kufuatia kibano cha DC (Igunga): Wabunge wa CHADEMA wakamatwa

Hii ndio faida ya kuwapa vijana pombe na bangi. Sasa ndio watanzania watajua kuwa hawa CDM ni wapenda fujo. Kama kila jambo mtalitatua kwa fujo basi hii nchi mkipewa itawaka moto.
 
Inaonekana DC alichelewa kufunguan kesi so ikabidi ihakachuliwe na kuwekwa IR ileile kweli magamba kazini
 
watanzania tukiyaachia haya mambo kirahisi kwa ushabiki wa kisiasa yatatufikisha kusiko
 
Jizungumzie wewe binafsi coz wengi bado wana imani na CDM
CHADEMA wasivyopenda hijab! Nadhani nayo ilichangia kwa kiasi kikubwa hilo sakata! Hawa wahuni wamepoteza imani hata ile ndogo tuliyokuwa nayo juu yao!
 
07igu.jpg


Duu, jimama anatia huruma!

Huyu mama kama ana watoto na wapo hapa JF sijui hii aibu wanajisikiaje?
 
CHADEMA wasivyopenda hijab! Nadhani nayo ilichangia kwa kiasi kikubwa hilo sakata! Hawa wahuni wamepoteza imani hata ile ndogo tuliyokuwa nayo juu yao!
<br />
<br />
acha kutukana kama muhuni.
 
Kiukweli tuache majungu, DC alichemka na kwa jinsi ile inatilia shaka usalama wa viongozi wetu iwaje aende katika mkutano ambao ulikwa katika ratiba bila ulinzi! Yaani kwa jinsi alivyokwidwa ni kama mhuni fulani kumbe ni kiongozi!
Vilevile kama alifanyiwa ubaya asingweza kwenda kwenye mkutano wa CDM ambao ulikuwa unataka kuanza, hii ni ishara kuwa hakukuwa na vurugu na yeye mwenyewe DC alikuwa radhi kuongea na Dr Slaa baada ya sokomoko hilo. Nachelea kusema ya Dc yasije kuwa kama ya mizengo Pinda kusema uongo.
Kuna haja ya serikali kujipanga badala ya kukurupuka katika baadhi ya kesi kulinda heshima yake.
 
Jamani acheni kudanganya umma.hakuna mbunge aliyekamatwa na police. Chadema 2mepanga mapinduzi makubwa igunga kwa kutumia kanuni na sheria za nchi. Now tunajiandaa kumkamata jk endapo atatumia magari na vifaa vya ikulu (serikali) katika shughuri za kisiasa na kichama.
 
Hii ndio faida ya kuwapa vijana pombe na bangi. Sasa ndio watanzania watajua kuwa hawa CDM ni wapenda fujo. Kama kila jambo mtalitatua kwa fujo basi hii nchi mkipewa itawaka moto.

Hakika jinsi unavyosema upo sahihi kadiri ya mfumo wako wa ubongo ambao umeathirika. Hujasema kama vijana walifanya nini hasa na kwa nini walifanya hivyo. Tukio hilo linaonyesha ukweli wa upande mmoja kuwa DC alifika katika maeneo ambako kuna mkutano wa CDM. DC anafanya mkutano wa ndani na hapo hapo ana fomu za wasimamizi (eti katumwa azipeleke kwa msimamizi). Hata kama mtu unataka kumtetetea DC unapata wakati mgumu kwa sababu yapo maswali mengi ambayo anapaswa kuyajibu kama haya:
1. Ni mkutano wa aina gani aliokuwa akiufanya na ulihusu nini?
2. Huo mkutano wa DC na watendaji kwanini ulifanyika siku ambyo CDM nao wanafanya mkutano wao?
3. Hizo fomu za wasimamizi alipewa yeye kama nani?
4. Hao waliompa fomu alikutana nao wapi na katika mazingira gani?
5. Je, uwepo wake katika eneo hilo ambalo CDM walikuwa wakifanya mkutano ilikuwa na maana gani?

DC tunakupa pole sana lakini hata hivyo mtu aliyedhalilishwa kwa sababu amekutwa katika mazingira ya namna hiyo sidhani kama anastahili kupewa pole maana ni sawa na kumpa pole mtu alipigwa baada ya kukamatwa katika ugoni.
 
CHADEMA wasivyopenda hijab! Nadhani nayo ilichangia kwa kiasi kikubwa hilo sakata! Hawa wahuni wamepoteza imani hata ile ndogo tuliyokuwa nayo juu yao!
&lt;br /&gt;
Ndugu yangu kweli maji ya shingo! Naona sasa unaomba msaada wa udini. Tunaagalia chama kipi kina uzalendo wa kweli na si dini ndugu yangu mtz mwenzangu. Ndiyo maana hatuizungumzii CUF hapa. Kwa mimi hujanipata.
 
CHADEMA wasivyopenda hijab! Nadhani nayo ilichangia kwa kiasi kikubwa hilo sakata! Hawa wahuni wamepoteza imani hata ile ndogo tuliyokuwa nayo juu yao!

Acha unafiki wewe!Ni tangu lini wewe umewahi kuwa na imani na CHADEMA?we endelea kubaki na chama chako cha wapemba muijenge Pemba yenu full stop
 
Tuwe wakweli chadema ni wavunjaji wa sheria, hapa wamefanya kosa kubwa kuchukua sheria mkononi na kumdharirisha mteule wa rais ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani

1. Mwigulu kufumaniwa na mke wa mwanachama mwenzake tena kada maarufu siyo kosa!
2. Yule mgombea wenu aliyempiga mtama ocd wa wilaya na RPC wake kusema ni mambo binafsi siyo kosa kisheria?
3. Kichekesho zaidi DC sasa amekuwa mesenja wa kupeleka barua za wasimamizi.
Safari hii hali mbaya, mtasema hata yale yaliyoko matumboni mwenu.
 
D9cuFP+2PEisAAAAAElFTkSuQmCC


Hivi huyu kiwadhifa si mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya? Iwaje aondoke bila wajumbe wa kamati yake? Hapana kuna kitu kimejificha na ndo hicho kilichomfanya aombe msamaha. Kulalamika polisi ni kuficha aibu.
 
Hii ndio faida ya kuwapa vijana pombe na bangi. Sasa ndio watanzania watajua kuwa hawa CDM ni wapenda fujo. Kama kila jambo mtalitatua kwa fujo basi hii nchi mkipewa itawaka moto.
&lt;br /&gt;

Kama pombe na bangi vitatoa ujinga na umaskini huu uliokithiri wa mlo 1 kwa siku, kukosa dawa mahospitalini, mgawo wa umeme n.k, basi ndugu yangu WACHA WATU WAPOMBEKE! Ukiona huna point, si lazima uchangie. lF YOU HAVE NOTHING TO DO, DON'T DO IT HERE,
 
Haki na amani, vinaendana sana. Kila mtu atimize wajibu wake ktk eneo lake ili kuendana na weledi. Mwanasiasa afanye siasa,mtawala atawale,tume ishughulikie uchaguzi kuakikisha unakuwa HURU na wa HAKI,polisi watimize majukumu yao kiueledi kama itegemewavyo. Inatia shaka Dc kukutwa na fomu zinazohusu tume ya uchaguzi na kudai kuwa alikuwa anasaidia tuu! Nani alimtuma kazi isiyo yake? Ni swala la wakati yote yatakuwa wazi sikumoja, hizi ni ishala tu zinazo ongezeka kwa kasi, ni dhanivyo mimi ni wazi kuwa wakati umekaribia sana wa yote kuwa wazi na mabadiliko ya kweli kutimia.
 
Hili la kujichukulia sheria mkononi limekaa vibaya; hawa waheshimiwa wangekuwa waungwana wakamwomba radhi Mama Kimario!
 
Thats true hapo kuna ubabaishaji na kutaka kukichafua chama chetu CHADEMA kinachotusaidia kujua maovu ya serikeli inayoongozwa na chama kisichomakini na kisicho na huruma kwa wananchi wake ambacho wabunge wake wanahitaji kuongezewa posho wakati kima cha chini cha mwananchi mfanyakazi wa kawaida hakifiki laki mbili kwa mwezi.CHADEMA fanyeni kazi tupo wananchi wenye uchungu na nchi yetu tunawasupport.
 
Back
Top Bottom