Kufuatia kauli ya WHO na maono ya Rais Magufuli kuhusu kuizoea Corona naomba shule na vyuo vifunguliwe

commm

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,674
1,903
Iko hivi: Endapo ligi luu Tanzania bara ikarejea na mechi kuchezwa katika viwanja mbali mbali hapa nchini, basi ni vyema pia vyuo na shule zifunguliwe na maisha yaendelee.

Maana ukiachana na sehemu za viwanja vya mpira ambapo watu wanakusanyika kwa wingi pamoja na shule na vyuo.

Sehemu nyingine au kada nyingine maisha yanaendelea kama kawaida.

Hata watoto wenyewe walioambiwa wabaki nyumbani ili kuepukana na Corona, wapo mtaani tu kazi yao ni kuzurura hawana hata huo muda wa kujisomea.

Labda kwa watoto wa kishua ambao maisha yao yanawaruhusu kuishi maisha ya lockdown.

Nawasilisha.
 
Wewe una mawazo mfu kama baadhi ya wateule wa jiwe wanavyolazimisha walimu baadhi ya mikoa waende mashuleni kufundisha huku wakijuwa wanawaingiza kwenye hatari ya kupata maambukizi na hatimaye kueneza COVID 19 kwa watoto na raia wengne wasiokuwa na maambikizi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wewe pia una akili mfu ,maana ungeona maisha ya mitaani huku ,wala usingeandika hivi unavyoandika hapa

Maana hao watoto ambao wameambiwa wakae nyumbani ili kujikinga na korona wapo busy kuzurura tu

Labda wewe utakua unaishi mitaa ya kishua
 
Hata wewe pia una akili mfu ,maana ungeona maisha ya mitaani huku ,wala usingeandika hivi unavyoandika hapa

Maana hao watoto ambao wameambiwa wakae nyumbani ili kujikinga na korona wapo busy kuzurura tu

Labda wewe utakua unaishi mitaa ya kishua
Wewe kama huwezi kuwaamlisha wanao au wadogo zako wakae ndani na wanaendelea kuzulula mtaani shauri yako.
Huenda uliwalea hivyo, chakufanya komaa na wanao/wadogo zako kuwaomba wazizulule wakae ndani kama watalaamu wa afya walivyoelekeza...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurugenzi wa WHO amesema covic si yakuisha kesho, wala lockdown haisaidii kwa zile nchi ambazo tayari corona imeingia.

Rais Magufuli pia alishaona mbali kuwa hili gonjwa haliondoki tutakuwa nalo tu huku tukisaidiwa na Mungu.

Ni dhairi shughuli za kijamii zifunguliwe na tuzidi kupatiwa njia za kisayansi na kiroho kujihadhari na ugonjwa huu.

Naiomba serikali kupitia Wizara ya Elimu kutoa tamko la kufungua mashule, kama Uingereza ilivyoamua kufanya.

Asanteni.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom