Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,602
- 5,569
Sheria ya mtandao haiwahusu "WANAMTANDAO"Leo asubuhi, nimesoma humu JamiiForums Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka TAKUKURU ikikanusha taarifa za upotoshaji zilizoandikwa na magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE zikiwahusisha Maafisa mbalimbali wa TAKUKURU na tuhuma za kupokea rushwa. Kutokana na uzito wa Taarifa husika za kukanusha, taarifa hiyo imesainiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.
TAKUKURU ni moja ya Taasisi nyeti za kiserikali. Kimajukumu, TAKUKURU ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wakati nchi ikiwa kwenye vita kubwa ya kutokomeza rushwa nchini, tuhuma dhidi ya wenye jukumu la kutokomeza rushwa si tuhuma ndogo. Ni tuhuma kubwa na zinazopaswa kufanyiwa kazi haraka-kama ilivyotolewa Taarifa ya kukanusha. Uchunguzi zaidi pia unapaswa kufanyika juu ya tuhuma hizo, hasa kwa aliyezitoa ili kujua lengo na nia ya upotoshaji wake.
Ujumbe wa jumla wa Taarifa ya TAKUKURU ni kuwa tuhuma za FAHARI YETU na TANZANITE si za kweli na za kupotosha. Ndiyo kusema, magazeti hayo yameandika habari zisizo za kweli na za kupotosha ambazo zinaweza kusababisha sintofahamu kwenye jamii. Kinachofuata hapo, kwa mujibu wa Sheria, kuwashughulikia wasemauongo na wapotoshaji hao. Katika muktadha huu, magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE yashughulikiwe na kudhibitiwa ipasavyo.
Roporopo huweza kuleta madhara makubwa!
Laiti kama kungeliandikwa na wengine... kama si maagizo
Ni vigumu sana magazeti hayo kufungiwa au mmiliki wayo kuchukuliwa hatua kwa jambo dogo kama hilo kwani ameshafanya makubwa kuliko hilo na hakukuwa hata na kemeo. Hili linamaanisha kwamba ANATUMWA NA ANATIMIZA WAJIBU WAKE KWA BWANA ZAKE. Ukiyakumbuka ya kina Mbilinyi na Mramba utajua kila chenye mwanzo huwa hakiukosi mwisho...Leo asubuhi, nimesoma humu JamiiForums Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka TAKUKURU ikikanusha taarifa za upotoshaji zilizoandikwa na magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE zikiwahusisha Maafisa mbalimbali wa TAKUKURU na tuhuma za kupokea rushwa. Kutokana na uzito wa Taarifa husika za kukanusha, taarifa hiyo imesainiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.
TAKUKURU ni moja ya Taasisi nyeti za kiserikali. Kimajukumu, TAKUKURU ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wakati nchi ikiwa kwenye vita kubwa ya kutokomeza rushwa nchini, tuhuma dhidi ya wenye jukumu la kutokomeza rushwa si tuhuma ndogo. Ni tuhuma kubwa na zinazopaswa kufanyiwa kazi haraka-kama ilivyotolewa Taarifa ya kukanusha. Uchunguzi zaidi pia unapaswa kufanyika juu ya tuhuma hizo, hasa kwa aliyezitoa ili kujua lengo na nia ya upotoshaji wake.
Ujumbe wa jumla wa Taarifa ya TAKUKURU ni kuwa tuhuma za FAHARI YETU na TANZANITE si za kweli na za kupotosha. Ndiyo kusema, magazeti hayo yameandika habari zisizo za kweli na za kupotosha ambazo zinaweza kusababisha sintofahamu kwenye jamii. Kinachofuata hapo, kwa mujibu wa Sheria, kuwashughulikia wasemauongo na wapotoshaji hao. Katika muktadha huu, magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE yashughulikiwe na kudhibitiwa ipasavyo.
Roporopo huweza kuleta madhara makubwa!
Wanaopanda miiba leo wasitarajie kuvuna maparachichi hakika watavuna kilekile walichokipanda...
Kwa sasa mwenye vijigazeti hivyo ni vigumu kupelekwa sheriani....
Itakuwa rahisi kwa tembo kupenya kwenye tundu la sindano kuliko....
Ametumwa...