Kufuatia Kanusho la TAKUKURU, magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE yashughulikiwe ipasavyo!

Nje ya mada:

Nilichojifunza JF siku hizi sio mahala pa majadiliano ya maslahi mapana ya taifa. Unaweza kuta mada nzuri imeanzishwa ila utakuta imejaa
1-uchama bila kujali maslahi ya tanzania kwa ujumla
2-Personal attacks kwa watoa mada
3-Dhihaka
4-Ujuaji mwingi kwenye kada zisizo zetu. Utakuta hata mimi geologist nabishana na mwanasheria au daktari kwenye kada zao.

Ni aibu sana

Mkuu pole sana, inaonekana ww ndio umepitwa na wakati, hivi sasa wapotoshaji ni hao wenye kada zao kwa maslahi ya matumbo yao. Na haya unayoyaona humu jukwaani ndio picha halisi ya nje ya mitandao. Hivi siku hizi huoni upotoshaji wa wazi ukifanywa na polisi au taasisi nyingine za kimamlaka? Huoni huko mahakamani ni jinsi gani mahakama zinatoa hukumu zinazoonyesha kabisa ni nje ya weledi? Huoni tume ya uchaguzi wanachofanya kwenye uchaguzi? Hizo taasisi ziko na watu wenye weledi lakini ndio zinazoongoza kwa upotoshaji kwa manufaa ya kisiasa.
 
... hivi vijarida vimeandika upumbavu mwingi kwa muda mrefu sana lakini vipo tu vinadunda! Sijui nani anavilinda hivi vitakataka. Ingekuwa magazeti mengine yameandika hayo, jana ile ile Dr. Abbas angeshaitisha press conference kutoa msimamo wa Serikali na kutangaza kuyafuta rasmi kwa muda usiojulikana. Lakini hivi vijarida vyenyewe vipo tu pamoja na kuwachafua watu wengi na kusambaza upotoshaji mwingi!
Kama hujui nani anawalinda, basi rudi usingizini.

Ingekuwa Tanzania Daima, ama mwanahalisi ndio yaliyoandika basi yangrshafungiwa asubuhi na mapema.
 
Leo asubuhi, nimesoma humu JamiiForums Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka TAKUKURU ikikanusha taarifa za upotoshaji zilizoandikwa na magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE zikiwahusisha Maafisa mbalimbali wa TAKUKURU na tuhuma za kupokea rushwa. Kutokana na uzito wa Taarifa husika za kukanusha, taarifa hiyo imesainiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

TAKUKURU ni moja ya Taasisi nyeti za kiserikali. Kimajukumu, TAKUKURU ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wakati nchi ikiwa kwenye vita kubwa ya kutokomeza rushwa nchini, tuhuma dhidi ya wenye jukumu la kutokomeza rushwa si tuhuma ndogo. Ni tuhuma kubwa na zinazopaswa kufanyiwa kazi haraka-kama ilivyotolewa Taarifa ya kukanusha. Uchunguzi zaidi pia unapaswa kufanyika juu ya tuhuma hizo, hasa kwa aliyezitoa ili kujua lengo na nia ya upotoshaji wake.

Ujumbe wa jumla wa Taarifa ya TAKUKURU ni kuwa tuhuma za FAHARI YETU na TANZANITE si za kweli na za kupotosha. Ndiyo kusema, magazeti hayo yameandika habari zisizo za kweli na za kupotosha ambazo zinaweza kusababisha sintofahamu kwenye jamii. Kinachofuata hapo, kwa mujibu wa Sheria, kuwashughulikia wasemauongo na wapotoshaji hao. Katika muktadha huu, magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE yashughulikiwe na kudhibitiwa ipasavyo.

Roporopo huweza kuleta madhara makubwa!
To buttress your point, I would borrow the words of the House of Lords, in DERBYSHIRE CC V TIMES NEWSPAPERS LTD (1992), The decision was explained by LordKeith in these terms:;

It is of the highest public importance that a democratically electedGovernmental body, or indeed "ANY GOVERNMENTAL BODY," should be open touninhibited public criticism. The threat of a civil action for defamation mustinevitably have an inhibiting effect on freedom of speech."

"...... to allow a local authority to sue for libel
would greatly inhibit freedom of speech"

"....Individual officers of a local authority would be able to sue in their own right for libel, and local authorities are at present able to bring an action for criminal libel"
 
Much obliged Counsel!
 
Ndo mnaamka Leo kisa imeguswa TAKU KULA RUSHWA?
mbuyu ushakomaa huo kuukata unaweza kuondoka na mtu
 
Leo asubuhi, nimesoma humu JamiiForums Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka TAKUKURU ikikanusha taarifa za upotoshaji zilizoandikwa na magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE zikiwahusisha Maafisa mbalimbali wa TAKUKURU na tuhuma za kupokea rushwa. Kutokana na uzito wa Taarifa husika za kukanusha, taarifa hiyo imesainiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

TAKUKURU ni moja ya Taasisi nyeti za kiserikali. Kimajukumu, TAKUKURU ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wakati nchi ikiwa kwenye vita kubwa ya kutokomeza rushwa nchini, tuhuma dhidi ya wenye jukumu la kutokomeza rushwa si tuhuma ndogo. Ni tuhuma kubwa na zinazopaswa kufanyiwa kazi haraka-kama ilivyotolewa Taarifa ya kukanusha. Uchunguzi zaidi pia unapaswa kufanyika juu ya tuhuma hizo, hasa kwa aliyezitoa ili kujua lengo na nia ya upotoshaji wake.

Ujumbe wa jumla wa Taarifa ya TAKUKURU ni kuwa tuhuma za FAHARI YETU na TANZANITE si za kweli na za kupotosha. Ndiyo kusema, magazeti hayo yameandika habari zisizo za kweli na za kupotosha ambazo zinaweza kusababisha sintofahamu kwenye jamii. Kinachofuata hapo, kwa mujibu wa Sheria, kuwashughulikia wasemauongo na wapotoshaji hao. Katika muktadha huu, magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE yashughulikiwe na kudhibitiwa ipasavyo.

Roporopo huweza kuleta madhara makubwa!
Pamoja na kuwa hivyo vijarida na waandishi/wamiliki wake hawaaminiki, lakini hata TAKUKURU yenyewe pia si kwamba ipo immune kwenye rushwa! Rushwa ni suala la attitude ya jamii yetu zaidi, na hawa TAKUKURU wanatoka miongoni mwa jamii yetu. Kwa hivyo yamkini (probability) kuwa nao wanakula rushwa sio NIL.

Hivi ile kesi ya yule aliyekuwa mhasibu wa TAKUKURU (kama nakumbuka vema) iliishia wapi?
 
we si mwanasheria nenda mahakamani ukashtaki, sijui kama kuna kesi hata moja umewahi kuisimamia au wewe ni mwanasheria wa mitandaoni? acha ukanjanja
Mkuu huyo ni msanii tu,mwanasheria makini huwa hakurupuki
Badala ya kuhimiza waathirika wakimbilie mahakamani,katoa mishipa ya shingo kutaka magazeti yafungiwe
 
Hayo ni magazeti ya Musiba a third person after Mkulubilanga. Akianza Mkukubilanga, anafuata BASHITE kisha mmiliki wa hayo magazeti.
Magazeti yenyewe yanachapiahwa mbweni kwenye asasi nyeti kuliko zote nchini.
Hamna mwenye uwezo wa kumuwajibisha
IMG-20190618-WA0046.jpeg
 
Natumaini Mh Mwakyembe amekusikia ngoja sasa tuone anachukua hatua gani. Binafsisimsubiri Mwakyembe kufanya lolote ili kuyaadibisha magazeti hayo, isipokuwa kama atapata maelekezo toka juu!
 
Back
Top Bottom