Kufuatia Kanusho la TAKUKURU, magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE yashughulikiwe ipasavyo!

Nje ya mada:

Nilichojifunza JF siku hizi sio mahala pa majadiliano ya maslahi mapana ya taifa. Unaweza kuta mada nzuri imeanzishwa ila utakuta imejaa
1-uchama bila kujali maslahi ya tanzania kwa ujumla
2-Personal attacks kwa watoa mada
3-Dhihaka
4-Ujuaji mwingi kwenye kada zisizo zetu. Utakuta hata mimi geologist nabishana na mwanasheria au daktari kwenye kada zao.

Ni aibu sana
kweli ni nje ya mada , lakini lengo la wewe kuandika hii kwenye uzi huu lilikuwa nini ?
 
Swali fikirishi je hayo mgazeti hayapewi rushwa kuandika upotoshwaji na je km hupewa rushwa ili kuandika upotoshwaji TAKUKURU wanashindwa nini kuwakamata
Imagine. TAKUKURU wana “jeshi” na wao huwa wanakamata, wanahoji, wanatesa na kutupa lupango. Ila sasa na wao eti wanalialia hapa badala ya kuchukua hatua mathubuti
 
we si mwanasheria nenda mahakamani ukashtaki, sijui kama kuna kesi hata moja umewahi kuisimamia au wewe ni mwanasheria wa mitandaoni? acha ukanjanja
sasa hapo kuna tatizo gani limepelekea wewe kutoa povu kiasi hicho? au nawe ni mbia wa hivyo vijarida? hivyo vijarida visikiage tuu, mnavyovilea vitajawashida kubeba! chekea nguruwe kwenye shamba la mihogo!!
 
Mkuu Mselewa, kwani taarifa kusainiwa na mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU ndiyo ushahidi tosha kwako kuwa hao maofisa hawakupokea rushwa? Kama anawatetea wenzake wasije wakapoteza kibarua chao?

Hao maofisa ni akina nani mpaka uwatetee kuwa hawawezi kupokea rushwa?
To me, ingeundwa tume huru ili ichunguze hizo tuhuma zilizoandikwa katika magazeti hayo na siyo kuishia kukanusha kuwa ni upotoshaji.

Pindi ushahidi utakapopatikana kuhusu hizo tuhuma itabidi sheria ichukue mkondo wake.

Kwa vile watanzania ni watu wa kupuuzia hakika hata hizi tuhuma watazipuuzia.
Kama hawajapokea rushwa kwanini wasifungue kesi mahakamani kwa sababu wamechafuliwa?

Let's think beyond the box.
 
Boss Petro E. Mselewa Sio kwa Jamhuri na Serikali hii, Kuna Issue na Mambo mengine hayaitaji Akili kubwa kuyajua na kuyaelewa. Mubasi yupo tu kama Chambo.

Mimi binafsi nafikiri Jamaa anatumika kuvunja Makundi ndani ya Chama. Anaandaa njia 2019 na 2020.

Leo asubuhi, nimesoma humu JamiiForums Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka TAKUKURU ikikanusha taarifa za upotoshaji zilizoandikwa na magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE zikiwahusisha Maafisa mbalimbali wa TAKUKURU na tuhuma za kupokea rushwa. Kutokana na uzito wa Taarifa husika za kukanusha, taarifa hiyo imesainiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

TAKUKURU ni moja ya Taasisi nyeti za kiserikali. Kimajukumu, TAKUKURU ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wakati nchi ikiwa kwenye vita kubwa ya kutokomeza rushwa nchini, tuhuma dhidi ya wenye jukumu la kutokomeza rushwa si tuhuma ndogo. Ni tuhuma kubwa na zinazopaswa kufanyiwa kazi haraka-kama ilivyotolewa Taarifa ya kukanusha. Uchunguzi zaidi pia unapaswa kufanyika juu ya tuhuma hizo, hasa kwa aliyezitoa ili kujua lengo na nia ya upotoshaji wake.

Ujumbe wa jumla wa Taarifa ya TAKUKURU ni kuwa tuhuma za FAHARI YETU na TANZANITE si za kweli na za kupotosha. Ndiyo kusema, magazeti hayo yameandika habari zisizo za kweli na za kupotosha ambazo zinaweza kusababisha sintofahamu kwenye jamii. Kinachofuata hapo, kwa mujibu wa Sheria, kuwashughulikia wasemauongo na wapotoshaji hao. Katika muktadha huu, magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE yashughulikiwe na kudhibitiwa ipasavyo.

Roporopo huweza kuleta madhara makubwa!
 
Walikwishasema ambaye anaona Magazeti hayo yanamkera Akayashtaki hakuna kuyafungia
 
tumefikia pazuri kama takukuru hawawezi kumgusa (walau kumuita na kumuhoji) mmiliki wa magazeti...nani ataweza.......kwa mamlaka waliyonayo wameshndwa hata kutafuta udhaifu wenye mianya ya rushwa kwenye kampuni inayomiliki magazeti hayo ili wawaadabishe
 
Nje ya mada:

Nilichojifunza JF siku hizi sio mahala pa majadiliano ya maslahi mapana ya taifa. Unaweza kuta mada nzuri imeanzishwa ila utakuta imejaa
1-uchama bila kujali maslahi ya tanzania kwa ujumla
2-Personal attacks kwa watoa mada
3-Dhihaka
4-Ujuaji mwingi kwenye kada zisizo zetu. Utakuta hata mimi geologist nabishana na mwanasheria au daktari kwenye kada zao.

Ni aibu sana
Shida ni hao the so called MATAGA wapo wwngi sana mitandaoni, lengo ni kumpamba na kumlinda Meko.
 
Leo asubuhi, nimesoma humu JamiiForums Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka TAKUKURU ikikanusha taarifa za upotoshaji zilizoandikwa na magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE zikiwahusisha Maafisa mbalimbali wa TAKUKURU na tuhuma za kupokea rushwa. Kutokana na uzito wa Taarifa husika za kukanusha, taarifa hiyo imesainiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

TAKUKURU ni moja ya Taasisi nyeti za kiserikali. Kimajukumu, TAKUKURU ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wakati nchi ikiwa kwenye vita kubwa ya kutokomeza rushwa nchini, tuhuma dhidi ya wenye jukumu la kutokomeza rushwa si tuhuma ndogo. Ni tuhuma kubwa na zinazopaswa kufanyiwa kazi haraka-kama ilivyotolewa Taarifa ya kukanusha. Uchunguzi zaidi pia unapaswa kufanyika juu ya tuhuma hizo, hasa kwa aliyezitoa ili kujua lengo na nia ya upotoshaji wake.

Ujumbe wa jumla wa Taarifa ya TAKUKURU ni kuwa tuhuma za FAHARI YETU na TANZANITE si za kweli na za kupotosha. Ndiyo kusema, magazeti hayo yameandika habari zisizo za kweli na za kupotosha ambazo zinaweza kusababisha sintofahamu kwenye jamii. Kinachofuata hapo, kwa mujibu wa Sheria, kuwashughulikia wasemauongo na wapotoshaji hao. Katika muktadha huu, magazeti ya FAHARI YETU na TANZANITE yashughulikiwe na kudhibitiwa ipasavyo.

Roporopo huweza kuleta madhara makubwa!
Takukuru hawa bana?
Hakuna taasisi yoyote isiyo na waovu na wahalifu.
Mbona wanawasaka watumishi wao wenyewe kwa rushwa na ubadhilifu na habari ziko hapa JF na magazetini?
 
Hapo serikali watavuta miguu sana. Mwakyembe atakuambia yule aliyeona amekerwa au kuumizwa na hizo taarifa aende mahakamani akafungue kesi. huo ndio uchumi wa kati
Huyo naye alitolewa pale jalalani usitegemee lolote la maana toka kwake
 
1130612

Nani atakaethubutu kulinyoshea kidole, au kulikemea gazeti linalohaririwa magogoni..?
 
Back
Top Bottom