Kufuatia historia ya Mkapa yafanyike maboresho mukubwa katika Elimu

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Nimekuwa impressed na safari ya maisha ya marehemu Rais Mstaafu mzee Mkapa

Alianza shule ya msingi kijijini Lupaso miaka hiyo ya 1940s. Akasoma Ndanda na Kigonsera. Alisoma kwa taabu nyingi ikiwemo kutembea peku kwa kilometa nyingi. Lakini mwisho tumeona kile alicho archive, CV yake inatosha

Najiuliza hivi ubora wa elimu ile ya Tanzania hasa Shule za msingi uliishia wapi? Mbona mzee mkapa kafanya makubwa sana duniani kwa elimu ya Tanzania tena ya miaka karibia 80 iliyopita ?

Nashauri wizara ya elimu ichukue hii kama changamoto elimu yetu ipigwe msasa shule ziwe bora, kusiwe na haja ya kupeleka mtoto shule ya kulipia mamilioni viwango viwe sawa au zaidi ya private schools jambo linaloonekana kufanikiwa huko nyuma

Tuache Siasa kwenye Elimu ikiwa ni pamoja na île fikra ati ya kuachana na utumiaji wa Lugha ya kingereza,tumeona jinsi mzee mkapa alivyofanya vizuri katika lugha ya kiingereza ambapo msingi wa Mwanzo aliupata huko Lupaso, nadhani juhudi na uwezo wake ndio ulimfanya hadi kufikia kushiriki kwa ukamilifu katika maswala mengi ya kimataifa hadi kualikwa na viongozi wa mataifa mukubwa duniani jukwaa la world economic forum, kusuluhisha migogoro, ubalozi na majukumu mengi hata baada ya kustaafu hapo ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na english medium School ikibidi shule zote za serikali zitumie english kama lugha ya kufundishia.

Rais amefaulu kuifanikisha elimu bure sasa ni wakati wa wizara husika kuifanya kuwa Quality kwa kuhakikisha vyumba vya madarasa, ratio ya Mwalimu na idadi ya wanafunzi darasani, vifaa, viti madawati walimu wazuri pamoja na stahiki zao ziboreshwe vizuri

Nadhani tukiutafuta ubora tutafanikiwa kwani zamani tuliweza vipi? Kusiwepo tofauti za mbinu na mazingira ya ufundishaji kati ya government na private Schools

Apumzike kwa amani mzee wetu BWM.
 
Lugha zote mbili zitumike, halafu Kiswahili kizidi kupewa kipaumbele kikubwa zaidi. Masomo sekondari yafundishwe kwa Kiswahili. Wengi wanashindwa, siyo kwa sababu hawana akili, ila lugha ndiyo huwa changamoto kwao.

cc: mama D
Asante mkuu

Serikali inakuja na mpango mzuri na makini sana. Hatuwezi kuwa duniani karne halafu tukashindwa kuwasliana sababu hatujui lugha

Serikali ya John Pombe Magufuli haitashindwa hili

Kama ilivyo kwa watoto wa wenye vipato vya juu kupata elimu bora ikiwa ni pamoja na kuijua lugha ya kimataifa ya kiingereza watoto wa maskini nao watapata hivyohivyo

Mungu ibariki Tanzania
 
Asante mkuu

Serikali inakuja na mpango mzuri na makini sana. Hatuwezi kuwa duniani karne halafu tukashindwa kuwasliana sababu hatujui lugha

Serikali ya John Pombe Magufuli haitashindwa haitahili

Kama ilivyo kwa watoto wa wenye vipato vya juu kupata elimu bora ikiwa ni pamoja na kuijua lugha ya kimataifa ya kiingereza watoto wa maskini nao watapata hivyohivyo

Mungu ibariki Tanzania
Kuna mtu anajifungia sandukuni, hataki kutoka nje, lugha iko letaring shida mingimingi.
 
Somo la kiingereza lipo shule za msingi miaka na miaka ila tatizo ni namna linavyofundishwa

Kama lingefundishwa vizuri kusingekuwa na maPhd wasiojua kuongea kiingereza
 
Binafsi naona mfumo wa Elimu ungejikita kumuandaa mwanafunzi kuwa mbunifu na mvumbuzi wa vitu au mambo kuliko ilivyo sasa iliyojikita ktk kukalili,aidha iwaandae wahitimu kujiajiri na siyo kuajiriwa.
 
Binafsi naona mfumo wa Elimu ungejikita kumuandaa mwanafunzi kuwa mbunifu na mvumbuzi wa vitu au mambo kuliko ilivyo sasa iliyojikita ktk kukalili,aidha iwaandae wahitimu kujiajiri na siyo kuajiriwa.
Kuajiriwa na kujiajiri ni dhana ileile; no essential difference. Kitu cha msingi ni kujenga na kuimarisha elimu ya kujitegemea kimawazo, kifikra. Wasomi wanaowaza na kutamani kila kukicha wapewe misaada ya Wazungu wana ulemavu kichwani. Anayekulisha lazima akutumikishe. "No free lunch!"
 
Mkuu Kujiajiri na kuajiriwa haiwezi kuwa dhana moja,kwasababu anayejiajiri lazima awe Committed kwenye field husika,lazima awe creative,Risk taker,etc wakati anayeajiriwa yeye anaenda tu kutumikishwa na mara nyingi skills zake zipo kwenye makaratasi zaidi kuliko kwenye vitendo.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom