Kufuata sheria ni unyanyasaji kwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufuata sheria ni unyanyasaji kwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zhu, Jan 7, 2011.

 1. Z

  Zhu Senior Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nchi yetu kwa sasa imekuwa kawaida kwa kuto kufaata sheria. Ukianzia kwa mabasi. Basi likikamatwa ni unyanyasaji. Ukikamatwa kwa kutupa taka ni unyanyasaji. Ukidaiwa kodi na TRA ni unyanyasaji. Ukiandamana bila sheria ni unyanyasaji. Nchi yetu kwa sasa inakosa viongozi wanaoweza kutoa amri ya kufuata sheria za nchi. Jf yenyewe inatumia matusi sana ikifungiwa ni unyanyasaji. Lazima sasa tuangalie both side the rules and the ruled. Utaona wengi tunapenda kuyafanya yale tuyotaka kwa muda huo bila kujali athari zake kwetu binafsi au kwa taifa. Naamini mambo yako hivi kwa vile no one who is serious. Umeya ni wa madiwani but uongozi wa kitaifa wa siasa they make it an issue. Hii haijatulia. Wananchi lazima tuangalie hoja inakuja kwa manufaa ya vyama au wananchi. Porojo za wanasiasa zitatumaliza. Nchi za magharibi have managed us. We have to be think on our own mind. Politics is going to finish Africa while the western country have reluxed.
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Zhu hivi kwanini unaninyanyasa na hizi post zako....?
   
 3. Z

  Zhu Senior Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Great thinker
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Thanks Zhu
  "We Birds of a Feather Flock Together" ila usipende kuninyanyasa, we are all Tanzanians, Human Beings Fresh & Blood.
   
 5. Z

  Zhu Senior Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimegundua Jf ni sehemu ya kujadili 'News' au kupokea 'news'. Habari nyingi zinazopostiwa utakuta ni kutoka kwa gazeti, redio au Tv. Lakini hoja za kushirikishana wengi wanakwepa. Nafikiri hii pia inachangiwa na uelewa mdogo tulionao katika mambo mengi yanayotuzunguka katika maisha. Unachangia news then. Toja hoja.
   
 6. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  usifanye hivyo Zhu ebu nieleweshe na mimi tachangia..... usiwe mkali pole pole tunaeleweshana. Tusaidiane kukuza uelewa wetu.
   
 7. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  ZHU Lazima ufikirie kwanza ndipo ulete hoja usilete hoja ambayo wewe mwenyewe huielewi na huna uhakika nayo. JAMBO LA MSINGI NI LAZIMA UJUE NI KWANINI WATANZANIA WANAONA UNYANYASAJI KWA HAYO YOTE ULIYOYASEMA.JIBU NI KUWA ASILIMIA KUBWA YA VIONGOZI WA TANZANIA HAWA TEKELEZI HAYO, NA WAO NI DIRA, JE MWANANCHI ITAKUWAJE. Pia watu wanalipa kodi kwa maendeleo, mafisadi wanakula.JE WEWE IKIWA NI MTOAJI UTATOA WAKATI UNAFAHAMU ukitoa mtu anakula bure bure! Sasa unakuta uzembe na ujinga wa viongozi unaleta hasara kwa nchi na kusababisha wananchi kuwa na tabia mbovu. PIA UWE NA AKILI WEWE UNAPOLETA HOJA,maandamano ni haki ya mtu/kundi kuyafanya kwa amani, lakini Tanzania hakuna demokrasia na utawala wa sheria hivyo maandamano si haki kwa sababu madudu mengi hivyo wakiruhusu maandamano yatakuwa nchi nzima kutokana na hali halisi. LA KUTUKANWA,hivi mtu mjinga kama wewe ZHU itakuwaje usitukanwe kwa hoja zako za kipuuzi?
   
 8. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Viongozi wenyewe ndo wamekuwa mahiri katika kukiuka sheria na taratibu!! Unataka kusema sheria zetu haziruhusu watu kukusanyika, kupeana taarifa na kuonesha misimamo yao????? TRA wangekua wanafuata sheria watu wasingelalamika!! Huko nako ni uonevu mtupu?? Wanaotakiwa kulipa kodi hawalipi!!!! Walala hoi ndo tunakamulia!!! Serikali inakusanya mahali ambako haikutawanya na kuvuna mahali ambako haikupanda!!! Wewe unamkamata mtu anatupa taka Je umemuwekea miundo mbinu madhubuti ya kukusanya taka????? Miji yenyewe inaachwa inajengwa hovyo bila mipango!!! Kwani kazi ya Serikali ni nini? Si kuratibu yote hayo?? Badala yake Serikali inakaa na kufanya kazi ya kulazimisha DOWANS walipwe!!! CHICKEN SHIT!!!
   
 9. Z

  Zhu Senior Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninakubali kuitwa mjinga and what ever name you give. Ukweli ni kwamba kwa nchi hii
  ni vigumu kuendelea kwa akili zetu za kuto jali sheria. Iwe ni viongozi au wananchi kwa sasa sheria imekuwa ni kuonea wananchi. Kwa mfano swala la Dowansi. Ikumbukwe kuwa bunge ndio lilishinikiza mkataba uvunjwe. Kuna wanasheria walisema kuvunja mkataba kuna gharama zake. Wanasiasa walipinga kwa nguvu. Sasa leo serikali imeshindwa kesi inatakiwa kulipa wanasiasa hao hao wanajifanya hawajui kama kuna sheria za mikataba.
   
 10. m

  mzambia JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ikija katiba mpya ndoulete hoja yako ya unyanyasaji mi nitachangia.

  Kuhusu kodi mi nakatwa kny mshahara, mazao, biashara yangu , bidhaa nazonunua bila kuangalia nimelipa kodi tayari ya paye, lazima nijione nanyanyasika maana sioni maendeleo kila siku nakaa gizani na umeme nimeweka nyumbani kwangu na ninalipia kodi huko kny luku je kwako wewe zhu si manyanyaso hayo?
   
 11. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ni unyanyasaji ndio kwa sababu sheria lazima ifatwe na watu wote. Sisi wananchi tunapoona sheria inavunjwa na viongozi na sisi ndipo tunapoamua kufanya tunayoyataka sisi.
  Hata katika ngazi ya familia ukiona kuna matatizo ujue baba/mama au wote wameshindwa kuwajibika effectively as heads of family.
  Wewe huwezi kunikataza kitu wakati wewe nakuona unakifanya na unabenefit.
  Siasa inatumaliza kweli. Hofu kwa vizazi vya kesho maana watakuta nchi nyeupe resource zote zishatafunwa na hata zile renewable zitakuwa katika hali mbaya zaidi.
   
Loading...