KUFIMA na KUBEDU

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Watanzania tumejiwekea utaratibu(japo siyo rasmi) wa kuwaenzi viongozi wetu kwa michango yao kwa taifa letu kwa kutoa majina ya viongozi hao kwa baadhi ya maeneo kama vile barabara, viwanja vya michezo, taasisi za elimu ya juu, majengo, madaraja nakadhalika. Kwa mfano:

Nyerere
The Mwalimu nyerere International airpot
The Mwalimu nyerere memorial academy pale kigamboni
Mwalimu nyerere road

Mwinyi
Ali hassani mwinyi road
Ali Hassan Mwinyi stadium Tabora

Mkapa
Benjamini William Mkapa Economic Processing Zone EPZ(Mabibo)
Mkapa bridge (daraja la mkapa)
Benjamini William Mkapa tower(mafuta house)

Na kulikuwa na tetesi kwamba uwanja mpya wa taifa walitaka uitwe Mkapa stadium na chuo kikuu cha dodoma walitaka kiitwe Benjamini William Mkapa university lakini ikapendekezwa isiwe hivyo maana ingekuwa too much

Tukiachia mbali majina ya shule za secondary kama
Ali hassani mwinyi Elite schools
Kambarage secondary school
Mkapa High School(City High School)

Binafsi naona kama mda unazidi kuisha jina la Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete linaweza lisitumike kabisa katika eneo lolote lenye hadhi, na kwasababu vyuo kama CBE na IFM kwasasa watakuwa wakitoa degree badala ya advanced diploma nadhani utakuwa ni mda muafaka kuitumia nafasi hii pia kubadilisha majina yao, kwa mfano IFM yaweza kuitwa Kikwete University of Finance Management(KUFIMA) au CBE ikaitwa Kikwete University of Business Education(KUBEDU). Ni mapendekezo tuu kama ikionekana hastahili hata kwa hilo basi japo napenda sana jina la kikwete litumike mahala fulani panye hadhi na binafsi nina Bar ya kichovu pale tegeta naogopa kuiita jina lake.
 
Ni kweli kabisa anastahili kuenziwa lakini, kwasababu mda bado upo na bado yupo madarakani mpaka miaka minne ijayo yatapatikana maeneo ya kutoa jina lake, kwa mfano hivi sasa ana mpango wa kujenga madaraja ya juu pale Ubungo, Tazara, na fire moja kati ya hayo yaweza kuitwa Kikwete fly over!!
 
sidhani kama ndani ya muda uliobaki atakua amefanya jambo lolote la maana,maana kipato cha serikali ni kwa ajili ya mishahara na posho na kuhudumia ma land cruiser v8.barabara ya msata-bagamoyo itaitwa kikwete road nadhani inatosha!
 
Kama ni lazima sana basi " Bagamoyo Collage of Arts" kiwe "Kikwete Collage of Arts" (chuo cha Sanaa cha Kikwete)Kikwete University Of Finance Management!!!! with all these public funds mismanagement!! really no way.
 
mi nakushauri hyo bar yako uiite tu kwa jina lake,inaweza ikawa ''kikwete bar & nyama choma''
 
Taabu moja ya majina iwe ndani ya jamii (familia) au penginepo huwa yana-tabia ya kurithi na mwenendo wa lilipotoka jina hilo.

Inakuwa na itakuwa heri iwapo mtu huyo lilipotoka jina ana tabia njema, vinginevyo jamii yote itakayopita kwenye hiyo taasisi watakuwa Rotten.

Pengine ndo sababu hadi leo bado kimya hii huenda imeonyesha hofu mahali fulani!!
 
nadhani hii thread ingeenda kwenye jukwaa la jokes/utani maana inachekesha sana ukisoma comments za magreat thinkers unafurahi na kucheka sana, zinafurahisha sana.
 
Back
Top Bottom