Kufilisika kwa wafanyabiashara wa maduka ya vyakula 'rejareja' wanakosea wapi?

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
4,137
13,824
Huu ni uchunguzi rasmi ambao nimeufanya, unakuta mtu amepata milioni mbili akaanzisha duka LA vyakula 'rejareja' baada ya miezi 4 duka halina kitu ilihali lilikuwa limejaa na miezi inayofuata unakuta kafunga kabisa yaani hana hata mtaji wa kuanza na Moja.

Ni wachache sana ambao wanafanikiwa katika hii biashara, Je hawa wengi wanakosea wapi kimahesabu kiasi chakushindwa kuendelea tena na hii biashara.

Tuondoe kodi ya pango , TRA na kusema biashara mbaya hakuna wateja, Nataka KIMAHESABU wanakosea wapi?

Najua Kuna wataalamu wa biashara humu mtusaidie!
 
Cha kwanza na kikubwa ni kushindwa kutofautisha kati ya fedha binafsi na fedha za biashara na cha pili ni rekodi mbovu au kutokuwepo kwa rekodi kabisa...
Pia lazima uweke wazi ni vyakula vya kupika ili wateja wavinunue au ni vyakula vikavu au vibichi,Kama ni vikavu mbona magenge ya kaliakoo hayafi miaka nenda miaka rudi.Kwa namna nyingine huenda gharama za uendeshaji na uuzaji zina changamoto,ukikopesha vyakula na wewe ukala hapo na watoto wakakwapua pesa na mama yao akapeleka vikoba,no way.
 
Unapoanza biashara yeyote lazima ujue mambo mengi sana.
Wengi huamua tu kuanza biashara na sio kwetu hata wenzetu pia biashara nyingi hukwama mwaka wa tano.
Lakini kwetu zingine hazivuki mwaka wa kwanza na sababu kuu ni kuwa mtu anaingiza hela zote bila kuangalia kodi na gharama zingine za miezi ijayo.
Hela zote umeingiza kwenye bidhaa halafu unategemea kula humo humo au hela zenyewe mkopo.
 
Fedha binafsi za matumizi ya kila siku na fedha za biashara....watu wengi wanashindwa kutenganisha. Unatakiwa ujilipe mshahara na sio kuchota kila siku kwenye droo linalohifadhi fedha ya mauzo.
 
Huu ni uchunguzi rasmi ambao nimeufanya, unakuta mtu amepata milioni mbili akaanzisha duka LA vyakula 'rejareja' baada ya miezi 4 duka halina kitu ilihali lilikuwa limejaa na miezi inayofuata unakuta kafunga kabisa yaani hana hata mtaji wa kuanza na Moja.

Ni wachache sana ambao wanafanikiwa katika hii biashara, Je hawa wengi wanakosea wapi kimahesabu kiasi chakushindwa kuendelea tena na hii biashara.

Tuondoe kodi ya pango , TRA na kusema biashara mbaya hakuna wateja, Nataka KIMAHESABU wanakosea wapi?

Najua Kuna wataalamu wa biashara humu mtusaidie!
1.Kuanzisha biashara halafu unaitegemea kuishi

2.Poor management ( Utawala na fedha )

3.Poor supervision - Kutojali

4.Siyo wazo lako - Umeambiwa tu biashara fulani inalipa umehemka umefungua tu. Do what you love - A great business idea comes within you !!

5.Mahitaji yote ya nyumbani hununui, unachukua BURE dukani - SI LAKO Bana

FANYA HAYO HATA KAMA UNA CHUMA ULETE LAZIMA UBUME TU !
 
Teh teh hapo bado ndugu wakija unawachotea tu..si lako bana
 
Back
Top Bottom