Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,264
- 33,867
Wakati Tanzania tukijipanga kuongeza Idadi ya ndege zetu ili kuendelea kulijenga upya shirika letu la ndege, Duniani kote inaonekana ni kama vile biashara ya uendeshaji mashirika ya ndege inazidi kuwa ngumu.
Habari za karibuni kabisa ni kufilisika kwa shirika la Ndege la "Thomas Cook" na kusababisha zaidi ya abiria wake 155,000 kukwamba kusafiri.
Kinachonishangaza ni kwamba hayo mashirika yanayosemwa kwamba yamefilisika si kwamba hayana ndege, hapana. Yana ndege nyingi sana tena sio mbovu bali ni nzima na zenye ubora wa kuaminika. Kwa mfano mpaka shirika la ndege la Thomas Cook linafilisika lilikuwa na ndege zaidi ya 34.
Jee kufilisika kwa mashirika ya ndege ni Uzembe wa wanayoyaendesha mashirika hayo?
CC: barafu