Kufilisika kisiasa kwa CHADEMA: Wanataka kumfukuza diwani aliyehudhuria maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
Diwani wa viti maalum CHADEMA jimbo la Tarime vijijini, Mh Philomena Tontora yuko hatarini kufukuzwa uanachama wa chama hicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuhudhuria maandamano ya kumpongeza Mh Rais Magufuli na serikali yake ktk jitihada za kupigania maslahi ya watanzania kunufaika na sekta ya madini nchini.

Mipango na shinikizo hilo linaandaliwa na ofisi ya mbunge jimbo la Tarime vijijini, kwa mtazamo wa ofisi hiyo inaonekana Philomena alikiuka shinikizo la ofisi hiyo ambayo toka mwanzo ilipinga na hata kujaribu kukwamisha tukio hilo kwa kuwashawishi wananchi na wadau wasijitokeze. Hata hivyo mpango wao wa kukwamisha ulishindwa kwasababu maandamano hayo ulikuwa ni uamuzi wa wananchi na wadau wa sekta ya madini bila kujali itikadi zao.

JE KTK KAULI ZA DIWANI KUNA MAHALI ALIKOSEA?

Diwani Philomena alipopoewa nafasi ya kuzungumza ktk maandamano hayo kama kiongozi alisema aliomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufika Nyamongo Tarime ili kusikiliza kilio chao ktk changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ucheleweshaji wa fidia na utatuzi wa wanachi wanaoishi mita 200 kutoka mgodi wa ACACIA uliopo Nyamongo.Kwa maelezo hayo utaona kuwa diwani huyu hakwenda kinyume na kile ambacho wananchi wanataka, japo anaweza kuwa amekiuka amri ya ofisi ya mbunge

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG] Katika hili Chadema inakosea sana, hata kama ofisi ya mbunge inashinikiza diwani huyu kuchukuliwa hatua za kinidhamu, hakuna mahala ktk hotuba yake alipokikosea chama chake. Nimeitazama video ya huyu diwani akizungumza, na kiuhalisia Mh Philomena amewakilisha mawazo na maoni ya wananyamongo wengi.

Natumai mkisoma andiko hili mtajitafakari, binafsi ningefurahi sana kuona mkifukuzana kwa usaliti, lakini huyu mama alifanya kazi kubwa ya kiuwakilishi kwa kufikisha mawazo na maoni ya watu anaowaongoza, kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na Mbunge ambaye ofisi yake ilisusa na badala yake ofisi ikaandika waraka kuwadhihaki wote waliohudhuria maandamano hayo kuwa ni vibaraka.

Magoiga SN
 
4e99ebb87415ed58f2e40b76c1c5df11.jpg
 
Kitendo cha CCM kuanza harakati za kumpigania humu kwa mtandao ni wazi mnajua alikosea , kwanini CCM ndio mnakuwa wa kwanza kulalamika kuwa CHADEMA inataka kumchukulia hatua Diwani wake ? CCM ambayo leo ukituhumiwa kwa Rushwa unapandishwa cheo , hakika ndio CCM Mpya hiii ya Polepole...........
 
Ukitaka kuwafatilia vigeugeu chadema unaweza kupasuka kichwa.Hao ni sikio la kufa.
Sasa hivi zitto amekua hero wa chadema.
Laana ya kumtukana Slaa,inawatafuna mpaka wamuombe msamaha
 
Hivi ni nani ambaye hataki kulipa fidia kwa walioumizwa ? DC anamwelekeza nani kulipa fidia ? Hivi huyu Mwakilishi wa Rais Magufuli anampelekea ujumbe gani boss wake ? Kwamba serikali ya Magufuli inakandamiza wananchi wake mpaka wanaandamana ? Hivi kumbe hii sio serikali ya wanyonge kama inavyosemwa?
 
Unafahamu maana ya kuwa Mpinzani?

Ukishaitwa mpinzani wewe ni mpinzani wa Serikali uko kwa ajili ya kuichallenge serikali na sio kuisifia au kuipongeza Serikali.

Huyo afukuzwe tu hakuna namna.
 
Hivi ni nani ambaye hataki kulipa fidia kwa walioumizwa ? DC anamwelekeza nani kulipa fidia ? Hivi huyu Mwakilishi wa Rais Magufuli anampelekea ujumbe gani boss wake ? Kwamba serikali ya Magufuli inakandamiza wananchi wake mpaka wanaandamana ? Hivi kumbe hii sio serikali ya wanyonge kama inavyosemwa?
Chadema phorbia?
 
Diwani wa viti maalum CHADEMA jimbo la Tarime vijijini, Mh Philomena Tontora yuko hatarini kufukuzwa uanachama wa chama hicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuhudhuria maandamano ya kumpongeza Mh Rais Magufuli na serikali yake ktk jitihada za kupigania maslahi ya watanzania kunufaika na sekta ya madini nchini.

Mipango na shinikizo hilo linaandaliwa na ofisi ya mbunge jimbo la Tarime vijijini, kwa mtazamo wa ofisi hiyo inaonekana Philomena alikiuka shinikizo la ofisi hiyo ambayo toka mwanzo ilipinga na hata kujaribu kukwamisha tukio hilo kwa kuwashawishi wananchi na wadau wasijitokeze. Hata hivyo mpango wao wa kukwamisha ulishindwa kwasababu maandamano hayo ulikuwa ni uamuzi wa wananchi na wadau wa sekta ya madini bila kujali itikadi zao.

JE KTK KAULI ZA DIWANI KUNA MAHALI ALIKOSEA?

Diwani Philomena alipopoewa nafasi ya kuzungumza ktk maandamano hayo kama kiongozi alisema aliomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufika Nyamongo Tarime ili kusikiliza kilio chao ktk changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ucheleweshaji wa fidia na utatuzi wa wanachi wanaoishi mita 200 kutoka mgodi wa ACACIA uliopo Nyamongo.Kwa maelezo hayo utaona kuwa diwani huyu hakwenda kinyume na kile ambacho wananchi wanataka, japo anaweza kuwa amekiuka amri ya ofisi ya mbunge

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG] Katika hili Chadema inakosea sana, hata kama ofisi ya mbunge inashinikiza diwani huyu kuchukuliwa hatua za kinidhamu, hakuna mahala ktk hotuba yake alipokikosea chama chake. Nimeitazama video ya huyu diwani akizungumza, na kiuhalisia Mh Philomena amewakilisha mawazo na maoni ya wananyamongo wengi.

Natumai mkisoma andiko hili mtajitafakari, binafsi ningefurahi sana kuona mkifukuzana kwa usaliti, lakini huyu mama alifanya kazi kubwa ya kiuwakilishi kwa kufikisha mawazo na maoni ya watu anaowaongoza, kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na Mbunge ambaye ofisi yake ilisusa na badala yake ofisi ikaandika waraka kuwadhihaki wote waliohudhuria maandamano hayo kuwa ni vibaraka.

Magoiga SN
Maandamano yepi tena hayo jamani? Si nilisikia maandamano,mikutano ya adhara marufuku hadi mwaka 2020
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom