AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Diwani wa viti maalum CHADEMA jimbo la Tarime vijijini, Mh Philomena Tontora yuko hatarini kufukuzwa uanachama wa chama hicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuhudhuria maandamano ya kumpongeza Mh Rais Magufuli na serikali yake ktk jitihada za kupigania maslahi ya watanzania kunufaika na sekta ya madini nchini.
Mipango na shinikizo hilo linaandaliwa na ofisi ya mbunge jimbo la Tarime vijijini, kwa mtazamo wa ofisi hiyo inaonekana Philomena alikiuka shinikizo la ofisi hiyo ambayo toka mwanzo ilipinga na hata kujaribu kukwamisha tukio hilo kwa kuwashawishi wananchi na wadau wasijitokeze. Hata hivyo mpango wao wa kukwamisha ulishindwa kwasababu maandamano hayo ulikuwa ni uamuzi wa wananchi na wadau wa sekta ya madini bila kujali itikadi zao.
JE KTK KAULI ZA DIWANI KUNA MAHALI ALIKOSEA?
Diwani Philomena alipopoewa nafasi ya kuzungumza ktk maandamano hayo kama kiongozi alisema aliomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufika Nyamongo Tarime ili kusikiliza kilio chao ktk changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ucheleweshaji wa fidia na utatuzi wa wanachi wanaoishi mita 200 kutoka mgodi wa ACACIA uliopo Nyamongo.Kwa maelezo hayo utaona kuwa diwani huyu hakwenda kinyume na kile ambacho wananchi wanataka, japo anaweza kuwa amekiuka amri ya ofisi ya mbunge
[HASHTAG]#Note[/HASHTAG] Katika hili Chadema inakosea sana, hata kama ofisi ya mbunge inashinikiza diwani huyu kuchukuliwa hatua za kinidhamu, hakuna mahala ktk hotuba yake alipokikosea chama chake. Nimeitazama video ya huyu diwani akizungumza, na kiuhalisia Mh Philomena amewakilisha mawazo na maoni ya wananyamongo wengi.
Natumai mkisoma andiko hili mtajitafakari, binafsi ningefurahi sana kuona mkifukuzana kwa usaliti, lakini huyu mama alifanya kazi kubwa ya kiuwakilishi kwa kufikisha mawazo na maoni ya watu anaowaongoza, kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na Mbunge ambaye ofisi yake ilisusa na badala yake ofisi ikaandika waraka kuwadhihaki wote waliohudhuria maandamano hayo kuwa ni vibaraka.
Magoiga SN