Kufikisha ujumbe wa ukombozi wa Mtanzania vijijini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufikisha ujumbe wa ukombozi wa Mtanzania vijijini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Aug 31, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Inaelekea kuwa ccm inafanya juu chini kukwamisha ujumbe wa kumkomboa Mtanzania kufika vijijini. Natumaini kuwa sote ambao tu wazalendo na tunaelewa ni kitu gani kinachoondelea, tuna ndugu, marafiki na jamaa zetu huko vijijini.

  Tuna bahati kubwa kwamba tunaishi katika wakati ambapo teknolojia imepiga hatua kubwa, tofauti na miaka ya zamani. Teknolojia ambayo imesambaa sasa nchi nzima ni ile ya simu za mikononi na uwezo wa kutuma sms.

  Kwa mantiki hiyo basi, ninatoa ushauri kwa wazalendo wote wanaochukia ufisadi, kusambaza ujumbe wa kumkomboa Mtanzania, kwa kila ndugu, jamaa na rafiki anayeishi vijijini, (huko ambapo mafisadi wanasema wananchi hawawezi kupata habari za upinzani) ili wapige kura kwa kujua ni nani atakayewafaa na ni nani anawadanganya.

  Mimi binafsi nimeshaanza hivyo kwa kutuma sms,na hata pale inapowezekana kupiga simu na kuwaeleza hali halisi. Kutokana na maongezi yangu hayo, nimeweza kuwaelimisha jamaa zangu juu ya hali halisi iliyopo nchini mwetu, ufisadi unaondelea ambao unasimamiwa na kuendelezwa na chama tawala. Wengi wameelewa uhusiaono kati ya ufisadi huo na hali mbaya inayowasibu huko vijijini. Kutokana na juhudi zangu hizo, hao nilioongea nao wameamua kuchagua kwa busara zaidi katika uchaguzi ujao. Kwa kifupi, hawadanganyiki tena.

  Kwa pamoja tunaweza.
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli wa vijijini hata baadhi ya wa mijini pia bado hawajaupata ipasavyo ujumbe wa ukombozi! Inabidi infanyike kazi kubwa ya ziada ili kuweza kubadili mawazo mgando ya baadhi ya walio mijini ambao wameishakata tamaa wakidhani hakuna jipya wanaona bora liende lilivyo.

  Kwa mawazo yangu, ili kuweza kuwapata watu wa vijijini Dr. Slaa akaze uzi kusisitiza na kuwaambia wananchi jinsi CCM ya sasa ilivyokengeuka na kuacha kufuata misingi yote ya ile CCM aliyoiongoza Mwalimu Nyerere ambayo uongozi ulikuwa haununuliwi kwa vijizawadi vya msimu, uongozi ulipatikana kwa mgombea kujieleza jukwaani na wananchi kumkubali bila kutoa hata senti tano!

  Dr. Slaa aeleze kinaga ubaga kwamba yeye anataka kuendeleza pale Mwalimu Nyerere alipoachia katika kuwatendea wananchi mema wanayostahili yatakayowaletea wananchi maendeleo. Mkazo uwe kwenye upatikanaji wa maji safi, elimu bora na bure kwa wote, na afya. Haya ni mambo ambayo yanawagharimu wananchi fedha na wale wasio na fedha kama za kuweza kupata tiba za uhakika wanapoteza maisha yao kutokana na sera a kwenye makaratasi za CCM na viongozi wake ambao wameacha kabisa kujali maisha na uhai wa wananchi wenye kipato duni, na kuruhusu kundi la wachache kujinufaisha.
   
 3. s

  skeleton Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kumshukuru saana ndugu Dingswayo for his constructive idea. Nadiriki kusema ni constructive idea kwani iko action oriented. Nimeona ideas nyingi ambazo zinachangiwa na majority wa members wa hii forum ni constructive pia.

  Lakini at this critical moment ambapo uchaguzi uko mlangoni itakuwa ni busara pamoja na ku-identify na kukemea maovu yanayofanywa na CCM, tuweze pia kutoa constructive ideas ambazo ziko more focused on actions by WE members of this forum.

  Michango yetu haitakuwa na positive impact kama na sisi members hatutatoa ideas ambazo ni action oriented zitakazokuwa implemented na SISI wenyewe members apart from other Tanzanians. Tusikae tu tukiwa watazamaji na kumwambia Dr Slaa na CHADEMA wafanye hivi au vile. Nasisi wenyewe tupeane ideas zitakazosaidia kuing'oa CCM madarakani kwani haba na haba hujaza kibaba.

  Kama Dingswayo alivyosema mitandao inasaidia kuwaelimisha watu wa vijijjini lakini pia tusiishie vijijini. Hii mbinu ya mitandao na nyinginezo itumike kuwaelimisha na hata watu wa mjini pia.

  Mimi binafsi nitaanza kuwaelimisha wana familia wenzangu and then marafiki na watu wangu wa karibu (especially waliojiandikisha kupiga kura) mpaka waelewe somo langu la, "KWANINI USIIPIGIE KURA CCM UCHAGUZI HUU?" mpaka wakate shauri na pia siku ya kura tuandamane kwenye kura au niwahimize wakapige kura kama wako mbali nami.

  Naamini pia na wana JF wenzangu mnaopinga ufisadi mkifanya hivi mtakuwa mmemrahisishia Dr Slaa, CHADEMA na wagombea wengine wa upinzani wasio waovu katika kuing'oa CCM, kwani umoja ni nguvu na muda hata kama ni wa majeruhi una count kwani haba na haba hujaza kibaba. Though i'm daydreaming, you never know, Dr Slaa might be the next president of Tanzania na Tanzania inaweza kuwa ufisadi free country yenye maisha bora kwa kila raia wake.
   
Loading...