Seif Kazige Mbambizi
Senior Member
- May 7, 2016
- 135
- 92
Suala la matamshi katika lugha sio jambo tunaloweza kulifanya mjadala katika nchi kama hii ambayo bado inasumbuliwa na shida nyingi. Isitoshe tatizo la kuelewa au kutokuelewa lugha flani ni suala binafsi sana ambalo hatupaswi kulifanya kama mada ya siku au mjadala wa kitaifa kwasababu kiongozi anaeongoza Tanzania ni mswahili na lugha ya taifa ni kiswahili hivyo akitumia lugha ya kigeni kufikisha ujumbe kwa wahusika ni wazi kwamba watauelewa tu kwasababu wanajua watanzania lugha yao kuu ni kiswahili. Ukiacha kiingereza wapo viongozi wengine hawafahamu lugha ya Kiswahili, kichina, kifaransa, kihindi, kiarabu, kigiriki, kihosa, kingoni, kichaga, kizigua, kihaya n.k hata wakija hapa nchini wanajitahidi kuongea kiswahili lakini kwa makosa na bado tunaelewa nini walitaka kutuambia. Tuache fikra potofu kwamba kujua kuandika au kuongea kingereza ni ufahari sana.
Lugha yoyote ya kigeni ni njia tu ya mawasiliano sio sifa ya mtu flani kuwa kiongozi mzuri.
Lugha yoyote ya kigeni ni njia tu ya mawasiliano sio sifa ya mtu flani kuwa kiongozi mzuri.