Kufika hapa tulipo mh. Rais ni lazima achukue hatua hizi......! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufika hapa tulipo mh. Rais ni lazima achukue hatua hizi......!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Analyst, Mar 12, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kwa ufupi hali ya nchi yetu imefikia mahala pabaya sana.
  1. Wanaoelewa na kutafakari, hawaiamini tena serikali (isipokuwa pale wanapokuwa na maslahi binafsi katika kufanya hivyo).
  2. Serikali haiko organised kiasi ambacho haijawahi kutokea katika historia. Haijulikani nani ni yupi na yupi ni nani. Mwanyekiti wa kamati anataka kutoa maamuzi na kutekeleza kazi za waziri. Kauli za serikali zinatolewa na watu tofauti na kwa mtazamo tofauti bila kujali matokeo ya kauli zao. Mfano ni juu ya maandamano ya Chadema. Mmoja anatishia kutumia nguvu kuyazuia, mwingine anasema wana haki ya kuikosoa serikali na wa mwisho anasema wamepewa fedha kuivuruga nchi... kwa maslahi ya nani?... hajasema na wote hawa ni Mawaziri wa Serikali moja. Waziri Magufuli anataka majengo yabomolewe kupisha upanuzi wa barabara, Waziri mkuu anasema mpaka Baraza la Mawaziri likae ndo iamuliwe kama majengo hayo yavunjwe au la.....
  3. Rais analalamika Chadema wanataka kumtoa madarakani bure wakati yeye amechaguliwa kikatiba. Kweli (anakubali) hali ya nchi kiuchumi ni ngumu lakini yeye si Mungu kwa hiyo aliikuta hivyo na ataiacha ikiwa na matatizo. "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania" hayawezekani hadi mtoa ahadi hiyo awe Mungu.... Atakuwa Mungu lini?... Hakuna anayejua.
  4. Chuki za kidini zinapoanzishwa na kupaliliwa na viongozi wakubwa kabisa kwa kuwa tu wanahisi au kujiaminisha kwamba malalamiko yaliyopo si kwa sababu ya ufisadi na hali ngumu ya maisha tu, ila kuna jambo zaidi....jambo gani?...dini. Wananchi wenye uelewa mdogo wameivalia njuga issue ya udini kama sababu pekee ya watu wengi kulalamikia. Ufisadi?.... Mbona wizi mwingi umetokea katika awamu iliyopita na hawakusema?...ndiyo utetezi wa hoja. UTACHOKA!!
  5. Watuhumiwa wahalifu wakubwa wanasamehewa hata kabla hawajafikishwa Mahakamani wakati wengine wanaozea Magereza kwa vifungo vya kesi za kubambikiwa. Mifano ni kashfa ya EPA na mambo mengi yanayoendelea kuitafuna nchi. Mh. Rais anataka warejeshe fedha vinginevyo watapelekwa mahakamani. Walioiba nyingi zaidi wanasamehewa na walioiba chache wapo mahakamani. Kituko!
  6. Siku hizi hakuna hata kauli za kujilinganisha na nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Kwa nini..?... Who cares...?...Tutaungana kuunda shirikisho!
  7. nk..nk...nk...
  Orodha hiyo inaweza kujaza server nzima kama itaendelezwa lakini kwa ufupi mambo yanayoendelea katika uongozi wa nchi hii yanatia aibu na yanatuua wanyonge.  Kwa nini tuko hapa?
  1. Rais hana kauli juu ya lolote linaloiumiza nchi kwa kuwa yeye ni mmoja, tena muhimu, katika watu walioamua kujali maslahi ya mtu mmoja ama wachache na kusahau kinachoumia ni nchi nzima. Na kuna wajinga wachache wanaamini rais anafanya vizuri kwa hayo yanayoendelea. RA kwa mfano kala za EPA kupitia Kagoda (Inadaiwa kati ya bil.40 alizokwapua chama kiliambulia 10 tu) na Richmond/Dowans. Ipo wazi kwamba baadhi ya wezi wakubwa ni ama marafiki zake au wafadhili wakubwa katika siasa zake. Hawa jamaa wataendelea hivi mpaka lini?
  2. Rais hana mamlaka tena juu ya mawaziri wake ndiyo maana Kombani na AG walisema No Katiba Mpya yeye mwenyewe kaja na Yes. Kwa maana nyingine wanahitilafiana. Dowans lazima walipwe kauli zimetolewa na baadhi ya mawaziri na mwisho rais anasema hata yeye asingependa walipwe (ktk hili simwamini). Kina Sitta ndo basi tena. Ni kama Rais hawezi kuwaambia kitu kwa kuwa alijifanya kuwatenga katika ulaji.
  3. Upinzani unazidi kukua na kunawiri kwa kuwa sasa hivi hakuna mtu mwenye uwezo mzuri kwa kuchambua hali ya siasa na kuwapanga CCM. Walichokimbilia, badala ya kuwajenga, kinawabomoa zaidi. Sitta aliwapa uhuru wabunge kuikosoa serikali mwisho rais akaishia kupata 60% (Uchakachuzi Inclusive). Kwa kukosa mwelekeo RA katafuta House Girl amtunzie nyumba muhimu kwake, naye H/Girl kawa jeuri analazimisha kuzima moto ndani ya nyumba wakati tayari paa linawaka moto. CDM haoooooo...!!!!!! wanawamaliza nje ya Bunge, tena kwa hoja za msingi. Walivyo wagumu kujifunza sasa wanadai ni kuiondoa serikali kwa nguvu. Upumbavu mkubwa! Mikutano ya CDM inataja machungu mengi ya wananchi nao wanaguswa, wao(JK, RA na wenzao) badala ya kutafuta utatuzi wanajaribu kujenga PR kwa kusingizia mapinduzi... kwa nini hawawakamati basi ili wawapeleke mahakamani kwa kutaka kupindua serikali?
  4. nk...nk...nk...
  Orodha hii pia si fupi lakini ninachoshauri ni Mh. Rais kuchukua hatua zifuatazo:
  1. Akae kimya tu (and so is the Cabinet of his). Wajifanye hawajui kinachoendelea ili CDM wafanye kazi yao. Mwisho wa hatua hii si mzuri sana kwa taifa lakini unaweza kuwa mzuri kwa heshima ya serikali iliyojaa rushwa maana, kila mtu atajua nia yao na kuishia kujilaumu kwa nini aliwashabikia wakati wanagawa jezi za Yanga. Inajulikana wazi hawezi kuwakemea mafisadi wakubwa kwa kuwa naye ana maslahi yake katika ufisadi huo. Tutayajua yote sikua akitoka madarakani. Ya KIWIRA yalijulikana vipi kwani?..
  2. Aamue kuwa muungwana. Kama alivyokiri kushindwa kutatua matatizo ya nchi na aseme swala la ufisadi limekuwa gumu kwa kuwa baadhi ya watuhumiwa wakubwa ndo hasa wenye mamlaka ya urais na Katiba inasema wazi kwamba mtu yeyote atakayekuwa na mamlaka hayo hashtakiwi.
  3. Rais akiri wazi kwamba hapakuwa na swala la udini katika kupungua mvuto wake kwa wapiga kura isipokuwa kushindwa kwa serikali yake kutimiza ahadi. Awatake radhi wananchi wenye uelewa mdogo waliokwishaamini kwamba anapigwa vita kwa sababu ya dini ili kuiokoa nchi yetu na mzozo mkubwa siku wananchi watakapoamua kumchukulia hatua za kisheria yeye, maswahiba zake, mtangulizi wake nk.
  4. Kwa kuwa ameshatusababishia machungu makubwa, aamue moja kati ya haya mawili; ama kumtema RA na kuacha sheria ifuate mkondo wake na sisi wanyonge tumlinde ili awe huru kufanya kazi pasipo kuwaogopa RA na kundi lake au aamue kuachia ngazi ili ampishe mtu mwingine (hata kama ni wa CCM) mwenye uadilifu ili ajaribu kutusafishia nchi.
  5. Kwa gharama zozote zile namwomba JK asithubutu kujiingiza katika kutumia nguvu kuzuia demonstrations za watanzania wanyonge kabla hajafanya juhudi za wazi wazi za kutatua matatizo makubwa yanayolalamikiwa. Yeye mwenyewe kwa ahadi zake tamutamu, ilhali akijua yeye si Mungu, aliwapa watanzania wanyonge matumaini makubwa na wakamuunga mkono. Leo kageuka kijakazi wa mafisadi anataka wasilalamike. Hiyo si haki!
  PLEASE! PLEASE! DON'T KILL ANY INNOCENT CITIZEN....endapo watachoka maana wanalilia matatizo ya msingi wewe na kabineti yako mnazungumza vitu tofauti. Watu wanojazana ktk mikutano ya CDM wana machungu yao waulizeni ni yapi ili myatatue na si kujibu kama mipasho.
   
 2. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,555
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Na jana limeongezeka lingine!Waziri wa afya mponda juzi alitangaza kusitishwa mara moja kwa huduma za mchungaji Mwasapile alafu jana waziri wa sera uratibu na bunge William Lukuvi ametangaza kuwa serikali haiwezi kujiingiza kwenye masuala ya kiimani hivyo haina ubaya kwa huduma kuendelea!Hawa wanatumikia serikali moja lakini wanatoa kauli tofauti kila mtu akitoa msimamo wa serikali yake!Umesema vema sana Analyst,hii serikali ya awamu ya nne hasa hii ya kipindi cha pili imejaa vioja.Na sababu kubwa ni udhaifu wa mkulu.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280

  Thanks Analyst for your good and interesting post;

  Pamoja na mabaya unayoyaona au kuyasikia ya CCM, bado kwa tunaotaka mabadiliko kazi ni kubwa mno kuliko tunavyodhani

  1. Bado wabunge wengi ni CCM, hili halina ubishi kuwa wabunge wa upinzani bado hawajafanya kitu mbadala cha kuvuta hisia za watanzania. Mfano mzuri LEO hii Dr. Slaa anaweza kuongea lolote lile na likaeleweka sio kwa sababu ni Dr. bali kwa matendo yake alichukia malipo makubwa bungeni! hii inamweka kuwa mtu wa tofauti katika hilo. Wabunge wa upinzani karibu wote ni CCM typical, malengo yao, matendo yao wengi ni wajasiriamali na jobsearchers...UPINZANI ulikuwa na nafasi kubwa bungeni kuteka wananchi wote kwa matendo yao CUF zanzibar walifanikiwa hili na kivumbi chake tulikiona mpaka leo hii, itakuwa hadithi ya alinacha au ndoto kufikiri kuwa wananchi hawalioni hili. I repeat semeni msemalo wabunge wengi ndio nafasi za kutokea swala la wananchi na matatizo yao sahau!

  2. Umesema pia kuwa CCM , inaogopa, ni kweli imechanganyikiwa na nguvu kidogo ya wapinzani ambayo HAIPO ndiyo iliyokosekana, wapinzani wetu bado wanawaza evolution katika zama hizi za revolution, wapinzani wanapenda ku-compromise na hali halisi, wapinzani hawa ambao ni wanasiasa wengi hawana muda na taifa hili na kushindwa kukabili hili tatizo ndio ucheleweshwaji wa mapinduzi

  Sioni tatizo leo hii watu wakiandamana kupinga mwelekeo wa CUF-bara, TLP,NCCR, n.k ambavyo haviko wala havina mpango kwa maslahi ya TAIFA NA BELIEVE ME KUWA NAO HAWA KWENYE UPINZANI KUNACHAFUA WAPINZANI WAZURI! Sioni shida pia ya kuipa-challenge CDM na kuwaamsha hili wasilale na wajue kuna watu wanawaanagalia, bahati mbaya hili huwa halipokelewi positively na wana JF wengi achilia mbali na baadhi ya viongozi! wengi huwa hawachukulii changamoto ni MTAJI! BELIEVE ME TUNAWEZA KUVIFUTA VYAMA VYOTE UCHWARA we can do that even kesho!! hawa wanafiki wanaleta taswira wapinzani ni 'wale wale tu'

  HAAMINIKI MTU KUSHIKA TAIFA HILI MPAKA APITIE VIGEZO VYA KILA MTU!! hii ndio siasa ya kweli! hata washindi wa kura huwa hivi..

  3. Kumbuka kuwa kugeuza umma wa watanzania ni kitendo cha dakika 3 tu! unaowaona leo wako Upinzani kesho wanaweza wakawa washabiki wazuri sana wa CCM, ndio maana tunasema time will tell,lakini kazi kubwa ipo maana hili ni game, KUONA KIKWETE akitetemeka ni kuwa yeye mwenyewe bado hajui siasa, anajua taarabu, lakini believe me in CCM kun wanasiasa wazuri kwa maana ya wanasiasa wenye uwezo wa kugeuza upepo muda wowote, we need to face this challenge and reality! Sipati picha leo hii CCM wakisema Sita anakuwa waziri mkuu! sipati picha CCM wakisema magufuli anakuwa mgombea urais! sipati picha wakimweka Mwakyembe kuwa mgombea mwenza!!! NIMESEMA MFANO ILI UJUE JAMII YETU JAPO INAICHUKIA CCM lakini IMESHINDWA KUBAINI CCM NI WATU SI GARI, NA KATIKA HAO CCM KUNA WATU WAMEPEWA SIFA YA USAFI NA UPIGANAJI!! BAHATI MBAYA KOSA HILI LINAFANYWA HATA NA WAPINZANI WAZURI SANA! WE HAVE NO CLEAR AND DIFINED GOAL YA KUIONDOA CCM...leo CCM ikisema ishughulikie tranparently issues za IPTL, EPA,Kagoda, watu watabweteka na kusema bora CCM iendelee!!! NDIO MAANA NIMESEMA CREW YA SASA YA CCM HAINA AKILI , ILA NDANI YA CCM KUNA CREW NYINGINE AMBAZO NI HATARI NA WANAWEZA KUZIKA UPINZANI IN MINUTES WAKIAMUA KUFANYA KWELI NDANI YA CCM, sidhani kama hili haliwezekaniki. KUTAKA KUINDOA CCM hili hali kusifia baadhi ya walindani ya CCM nikichekesho cha KARNE! CCM YOTE IMEOZA na kila aliye ndani yake siasa ya tofauti na hapo NI UJANJA WA WACHACHE TUNAOWAJUA WASIOANGALIA MZIZI WA TATIZO, TUACHE KUPUMBAZWA NA KUPUMBUZIKA, kufuata mikumbo kwa kila kitu ni hatari sana, kuna wenye nia zao tofauti na wengine!

  4. Wakati nafanya utafiti ni kwa jinsi gani DSM haijaamka..Nikagundua moja ya vitu ni kuwa DSM ni kitovu cha biashara, wengi DSM maisha yao ni afadhali,WENGI NI WA KUJA NA WAMEKUJA KUTAFUTA!, hawako tayari ku-risk biashara zao kwa mapinduzi, ,machafuko, maandamano n.k ILA WENGI NI WAONGEAJI SANA WAKIONGOZWA NA WASOMI. Hivyo basi mfano sera za nyumba tano tano ile ya CDM inatakiwasana kwa miji kama ya DSM, DSM realy need very different and well researched move! mikoani upinzani ni WAO TU, siku zote wako tayari

  5. Nguvu anayoitumia JK kwa sasa ni dini, ukabila, na ujinga wa watu wengi.......asionekane ameshindwa, still wapinzani wana wajibu kuondoa doubt zote ambazo zitapelekea maadui kusema kitu. Hili ni crucial kwani inapofika muda wa kura mathalani TUHUMA ZA UWONGO ZIMEWEZA KUWAONDOA VIONGOZI WALIOWAZURI..ballot box has got no eyes !

  6. Ni ukweli pamoja na kujiridhisha kwa mafanikio bado Tanzania haina shiiiiida saaaaaaana kiasi cha kuwafanya watu waingine barabarani, sisemi shida ziwepo nguvu za ziada, hoja nzuri, na convicing power zinatakiwa ziwaondoe watu kwenye lindi raha ya ASILI! ikifikia muda asilimia 90 wakashindwa fedha ya nauli, au asilimia 80 wakalala njaa UKOMBOZI ndio ulipom TUSIFIKE HUKO! matusi hayawabadilishi wasiowaza mbali !!!

  7. Natamani ifikie muda watu kila mmoja wetu aulize jirani au mtu yeyote njiani kuhusu hali ya sasa na apate majibu! Twende field na kuwaza in realistic zaidi na tusipeane moyo. UKILAZA WA JK ndio umemuharibia angepatikana mwneye akili pale CCM inaweza isishikike na hapo ndipo penye KAZI KUBWA KWETU.

   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Sina uhakika kama CCM haijui inachofanya?
   
 5. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Thanks Mkuu Waberoya,
  Nakubaliana na wewe kwamba nchi yetu inaweza kunufaika zaidi kwa kuwa na Wabunge wengi wa Upinzani (makini na wenye nia ya dhati kuondoa matatizo yanayotukabili) pengine hata kuliko kuwa na utawala mpya kabisa ambao pia unaweza kuingia na matatizo yake. Nachelea kusema kuwa hata CDM, ukiondoa Slaa ambaye falsafa zake zinaelekea kuwa wazi zaidi bado sijaweza kuthububutu kumshabikia mwanasiasa mwingine katika hao wazito kitaifa kwa kuwa wengine wanaonekana kama si tofauti sana na JK katika pitapita zao.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Swali gumu sana hili mkuu!

  Mkuu kwa sasa CCM imechanganyikiwa, lakini naamaini wale wanaoweza siasa za hoja sio kundi la JK wako kimya na wanaangalia mambo, wakipewa nafasi waweke mtu wao utaona wananvyobadilika.

  Makundi yamekiua hiki chama na JK na wenzake wameshindwa kuhimili mikikimikiki! ilitakiwa pressure zaidi kipindi hiki, CCM wakipumua na kufufuka kuna hatari kubwa ya tunaotaka iondoke kuwa kwenye wakati mgumu wa kutafuta style nyingine.

  I believe the long strategy ni kuhamasisha na kuwaaminisha watu filosofi zaidi na sio ushabiki zaidi, mtu akijawa na filosofi huwa hapeperushwi na upepo wa mpito!
   
 7. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tuna safari ndefu, ... haya yanayoelezwa hapa yanatoa taswira ya jamii yenyewe ya Wabongo, kutaka kwenda peponi pasipo kuweka juhudi za kutosha kufanya hivyo.

  ... na tuwakamate wezi/mafisadi, wote waishie magerezani; tena na kazi ngumu juu yake! Hayati Sokoine aliwahi kujaribu miaka 28 iliyopita na wanyonge wote walikuwa nyuma yake lakini tatizo letu lilibaki palepale; kutotaka kujituma KUFANYA KAZI!
   
 8. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Kinachotuunganisha hapa ni vita dhidi ya UFISADI, tukaendelea na moto huu inawezekana sana JK na sisiemu yake wakaangushwa!

  Baada ya hapo tutatazamana wenyewe kwa wenyewe; wengine ni WAHFIDHINA, wengine ni WAJAMAA ASILIA, wengine ni MAFISADI waliokosa, na wengi wetu ni Wabongo wa kawaida wanopenda kupata mshahara mzuri pasipo kufanya kazi na wale wanaoishi kwa ujanjaujanja na mishen tauni maofisini kwetu huku tukiishi juu ya kipato chetu halisi.

  Watch this space, naamini JF itaishi kushuhudia kimbembe hicho!
   
 9. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  I agree with you 100%. Unakumbuka hata ilivyokuwa kabla Zitto hajaingia katika Tume ya Rais ya kufuatilia mikataba ya madini? CDM walionekana wamoja kuliko imagination leo nguvu imeongezeka na fedha zimeongezeka mifukoni mwa baadhi yao mambo yamekuwa mambo.
   
Loading...