Kufeli huku ni janga la taifa si suala la Wakristu vs Waislamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufeli huku ni janga la taifa si suala la Wakristu vs Waislamu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzito Kabwela, Feb 16, 2012.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Lula wa Ndali Mwananzela


  WAKATI mwingine natamani ningekuwa na uwezo wa kuwatia bakora baadhi ya watu wanaozungumzia suala la maelfu ya wanafunzi kufeli vibaya katika mtihani wa kidato cha nne.
  Watu wanaoniudhi na kunikera ni wale ambao wanayaangalia matokeo haya ya mtihani kama ni suala la ubora wa shule za “Kikristu” kulinganisha na shule za “Kiislamu” au wale wanaoona “kupendelewa kwa Wakristu” na “mfumo Kristu”.
  Mwitikio wa baadhi ya watu kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne kwa kweli unanifanya nijiulize kama udini umezama kati yetu kiasi kwamba hatuoni kilichotokea na kinachotokea katika elimu ni nini.
  Ndugu zangu, kuna janga katika sekta ya elimu ambalo linasababisha maelfu ya watoto wetu, wadogo zetu, ndugu zetu kuachwa nje ya elimu! Jamani, hawa maelfu wanaofanya vibaya si Waislamu, si Wakristu, si Wapagani hawa ni Watanzania!
  Kwa upande wa Wakristu
  Kuna baadhi ya Wakristu ambao wanapoangalia matokeo ya mitihani wanajisikia vizuri kwamba watoto wenye majina ya Kikristu wanaonekana kuwa wamefanya vizuri.
  Tena wengine wanajisikia vizuri wanapoona majina ya shule zilizofanya vizuri mengi yanahusiana na Wakristu na hivyo kuthibitisha ile imani kwamba shule za Kikristu ni bora. Sasa, jambo moja liko wazi sana kwamba shule za Kikatoliki – si shule za majina ya Kikristu tu -karibu sehemu zote duniani zinatoa elimu ya kipekee na bora zaidi.
  Hilo ni kweli India, China, Pakistani, Uingereza, Marekani na hata Indonesia. Kuna sababu ya hilo na si kusudio langu kuingia kwa undani kwenye sababu hizo. Sasa huu ni ubora unaotokana na mfumo wa elimu ya Kikatoliki pote duniani na hili halikuanza jana au juzi. Kanisa Katoliki lina historia ya muda mrefu katika masuala ya elimu mbalimbali huko Ulaya na baadaye katika makoloni ambayo yalichukuliwa na nchi za Ulaya.
  Nimesema hili ili kusiwe na hisia kuwa ni shule za Kikatoliki za Tanzania ndizo zinafanya vizuri zaidi. Wale wanaowaaminisha watu kuwa shule za Kikatoliki za Tanzania zinafanya vizuri zaidi kwa sababu “zinapendelewa” hawawatendei haki wasikilizaji wao.
  Mtu anaweza kwenda Kenya, Zambia, Uganda, Nigeria au nchi yoyote ambayo ina mfumo wa shule za Kikatoliki na ataona kuwa shule hizi zinafanya vizuri zaidi na mara nyingi kuliko shule nyingine binafsi au za serikali.
  Lakini si watoto wote wa Kikristu wanasoma shule za Kikristu! Si Wakatoliki wote hupeleka watoto wao kwenye shule za Wakatoliki kwanza kwa sababu zina gharama ya juu na vile vile kwa sababu ni chache na zina uchaguzi wa hali ya juu sana.
  Hii ina maana ya kwamba bado kuna Wakristu (Wakatoliki na wengine) ambao wanapeleka watoto wao kwenye shule hizi hizi za umma. Maelfu ya hao waliofeli kwa mara nyingine ni Wakristu vile vile na hivyo huku si kufeli kwa watoto wa Kiislamu peke yake kama watu wengine wanavyochukulia.
  Kwa Waislamu
  Wale Waislamu ambao wanaangalia suala hili kama ni mashindano ya “sisi dhidi ya nyinyi” hawawatendei haki watoto wa Kiislamu nchini. Kuwaambia au kuwafanya watoto waamini kuwa wamefeli kwa sababu ni Waislamu ni kuwaonea, kwani hao watoto wanajua – kama wanatazama vizuri – kwenye shule hiyo hiyo waliyofeli wao watoto wengine mamia wa Kikristu nao walifeli!
  Hawa Waislamu wanaofikiria kuwa Wakristu wote nchini wanapata elimu nzuri, wanapata kazi nzuri na wanaishi maisha yenye utu na kuwa Waislamu wote hawajasoma na hawana nafasi yoyote ya maana na kuwa hakuna Waislamu wengine wanaofanya vizuri kwenye mitihani, hawautendei haki ukweli.
  Sote tunajua wapo Waislamu ambao wamefanikia na wanaendelea kufanikiwa kwa kila kipimo; wapo wafanyabiashara, wasomi, walimu, madaktari n.k ambao ni Waislamu ambao wamesoma kwenye elimu hii ambayo Wakristu wengine wanapata. Sasa kufeli kwa baadhi ya shule za Kiislamu ni lazima kutafutiwe maelezo ya kisayansi kama vile kufeli kwa shule za Kata au shule nyingine binafsi kunavyohitaji maelezo.
  Nitoe mifano kidogo
  St. Mary ya Mbalizi huko Mbeya ni shule inayoonekana ina jina la Kikristu na sijui kama ni ya kanisa au mtu binafsi. Mtu mwingine anaweza kufikiria labda shule hiyo imefanya vizuri. Matokeo ya mtihani shule hiyo yanaonyesha kuwa waliopata daraja la 1 ni 0 waliopata daraja la 2 ni 0 waliopata daraja la tatu ni 1 na waliopata daraja la nne ni 38 huku 34 wakifeli. Huo mfumo Kristu umeshindwa vipi kuwasaidia hawa?
  Shule nyingine inaitwa St. Margareti ya wasichana. Sasa kwa jina na kwa vile ni ya wasichana tena wengi wana majina ya Kikristu watetezi wa hoja ya “mfumo Kristu” wangeweza kutuonyesha kuwa shule hiyo wanafunzi wake wameshinda kwa kiwango cha seminari za kiume. Hakukuwa na mtoto yeyote aliyepata daraja la kwanza, la pili wala la tatu! Walikuwepo 27 wa daraja la nne na 28 wakifeli kabisa!
  Shule nyingine ni St. Paul ambayo nayo kwa kuangalia haraka haraka tunaweza kuamini kuwa ni shule ya Kikristu na hivyo ingependelewa na mfumo “Kristu”. Wanafunzi wengi wana majina ya Kikristu lakini katika shule hiyo hakuna hata mmoja aliyepata daraja la kwanza, la pili au la tatu!
  Sasa hii ni mifano michache tena ya haraka haraka tu kuonyesha kuwa wanaofeli si watoto wa Kiislamu tu na si katika shule zenye majina ya Kiislamu tu! Wanaojaribu kuelezea kufeli huku kwa misingi ya kidini hutawasikia wakiwapigania watoto hawa wa Kitanzania! Wao wameng’ang’ania “mfumo Kristu, mfumo Kristu” na hawa watoto walilie nini? Rais Muislamu? Makamu Muislamu? Ndipo maelezo ya kufeli kwao yatapatikana?
  Tuvuke mpaka wa udini na kuliangalia tatizo letu kama letu sote
  Ndugu zangu, muda wa kubebesha lawama za kidini tena za kijinga umepita. Watoto wetu wanafeli kila mwaka na sisi watu wazima tumekaa kama washirikina kukwepa kuelezea mambo yanayoelezeka kisayansi na badala yake tunatafuta maelezo mepesi yasiyoweza hata kushawishi akili za mtoto mdogo.
  Wazazi wa Tanzania ni lazima wakasirike kuwa watoto wao wengi wanafeli na wanapoteza nafasi. Hivi tumewahi kujiuliza hawa watoto wote wanaofeli kila mwaka na wakakosa nafasi ya kuendelea mbele huwa wanaenda wapi? Hivi, tunafikiria wote wanaenda kwenye shughuli gani hasa? Hawa watoto wa kike ambao walijizuia na majaribu mbalimbali ili angalau wapate elimu ya sekondari wanapofeli nani anajali!?
  Binafsi naomba niwe wa kwanza kutaka uongozi wote wa Baraza la Mitihani kujiuzulu na pamoja nao kufumuliwa kwa uongozi wa Wizara ya Elimu. Hizi sera za CCM zimekuwa janga la kudumu sasa na watu wetu hawachoki na hawakomi! Leo hii vile ambavyo vimekuwa aibu na fedheha kwa familia nyingi vimekuwa navyo ni aibu hadi Ikulu! Nani atatusadia?
  Makundi ya Waislamu wanadai Wakristu wanapendelewa; Wakristu wanasema Waislamu hawapendi elimu. Lakini ukweli unabakia kuwa wanaofeli na kupoteza nafasi nyingi ni watoto wa Kitanzania, Waislamu, Wakristu, Wapagani na wasioamini kabisa!
  Tufanye nini? Well, wapo wanaoangalia CCM na serikali yake kutafuta majibu. Hatuamini kuwa tunavuna tulichopanda; hatutaki kukubali kuwa haya ni matokeo ya kushindwa kwa sera za elimu pamoja na mipango yake yote!
  Tunatumia mabilioni ya shilingi kila mwaka lakini tunazidi kufelisha kama tuna wazimu au tunashindana. Hadi inafika wakati watoto wanaandika mashairi ya bongo flava kwenye mitihani na watu bado wako na ofisi zao wakisubiri mwaka mwingine, hakuna hasira, hakuna kukerwa, hakuna kuchukizwa, inashangaza!
  Hivi walimu na wenyewe kwa nini wasigome hadi mabadiliko ya kweli yaanze? Walimu wanaweza na wanapata wapi ujasiri wa kwenda darasani na kukuta shule isiyo na milango, madawati, vitabu na watoto ambao wamekosa chakula? Mwalimu anaweza kufundisha vipi mahali ambapo mtoto akirudi nyumbani hana cha kufanya zaidi ya kujipanga kucheza “Hakunaga”?
  Hawa wazazi wanaoshabikia mtoto “anavyojua kucheza sana” wanafikiria watoto watafaulu kwa kuombea au kwa kuonea? Wazazi wangapi wanauliza kama mtoto kamaliza kazi na kufuatilia kuona amefanya kazi yake vizuri? Wazazi wenyewe ni nani anawasaidia kuweza kuwasaidia watoto maana si wazazi wote nao wana uwezo wa kusaidia watoto wao linapokuja suala la shule. Kama mzazi hakupata elimu yeye mwenyewe anaweza vipi kufuatilia elimu ya mtoto wake?
  Labda sasa inabidi tufikirie kitu kingine nje ya CCM, nje ya sera hizi zilizoshindwa na nje ya watu hawa hawa. Tufanye nini? Tusaidie vipi? Au tukubali tu na kuombea labda mwaka ujao tutafaulisha zaidi kidogo. Twende tukaombee na kwenda kwa waganga tuone ni nani anatuloga! Maana kama hatutaki kutumia vichwa vyetu na uwezo wetu tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu kubadilisha maisha yetu hivyo ni bora tuanze kutumia uganga wa kienyeji!?
  Vinginevyo, kuna kitu cha haraka, cha makusudi na kikali kinahitajika kufanyika ili kuokoa elimu ya watoto wetu. Lakini ili tuweze kufika ni lazima kwanza tukasirike. Mimi nimekasirika na nimekerwa. Sijui wewe mwenzangu unajisikiaje? Kama hujisikii hasira yoyote au kukerwa kwa namna yoyote, nina uhakika wewe ni sehemu ya tatizo!


  Source: Raia Mwema | Kufeli huku ni janga la taifa si suala la Wakristu vs Waislamu


   
 2. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kuna thread nilileta hapa wiki jana nikinukuu Sheikh Bassalleh aliyesema "Necta imesheheni mfumo Kristu ndiyo sababu ya wanafunzi waislamu kufeli" Nashukuru Lula wa Wanzali amemjibu na amelieleza kwa ufasaha sana. Kwa bahati mbaya wasikilizaji wengi wa sheikh Bassalleh katika kipindi chake cha kila jumapili ndani ya radio kheri nahisi si wasomaji wa gazeti kama Raia Mwema na huenda ujumbe huu muhimu usiwafikie.
   
 3. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Vipi kuhusu wabudha ,wahindu na wanaotambika na kuabudu masanamu shule zao zimeperfom vipi? laiti mgalijua Mungu wa wakristo sio Mungu wa waislam,kila imani ina Mungu wake,inategemea uwezo wa Mungu wa imani husika ktk kutatua matatizo.Ngoja wenye mapovu waje
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni sayansi tu itatupa majibu sahihi kuliko porojo la akina Malaria Sugu na wenzake.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wanaosahihisha mitihani wanakutana na namba za watahiniwa tu wakati wa kusahihisha si jambo rahisi kupendelea.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Vijana watatu wakristo katika kumi bora kitaifa wametoka Feza boys ambao ni shule ya kiislamu. Nafikiri sayansi ndio jibu badala ya majibu mepesi kwenye swali gumu.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mwaka jana Baraza la mitihani limewafutia mtihani wanafunzi zaidi ya 9000.
  Je, hawa ni wakristo au waislamu. Jibu sahihi ni dini mchanganyiko.
  Dini ipi ilionewa kutokana na uamuzi huu? jibu ni hakuna dini ilibaguliwa bali nchi imepata hasara.

  Taifa hili litaangamia kama tutaendelea kukosa majawabu ya maswali magumu.
   
 8. p

  petrol JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Lula wa Ndali Mwananzela umenena; sijui tuongeze nini. Tatizo ni la kimfumo. Dawa ni kukasirika na kusema basi inatosha. Tumewahi kusikia na hata watu kutunga kitabu cha viongozi wenye sifa/shahada zenye utata. Hakuna aliyeshituka . Sasa tunashangaa nini wakati watoto wetu wanafeli kiasi hicho, kiasi cha asilimia 10 ndio wamepata div 1-3. Binafsi div 4 ni kufeli tu - yaani watoto tisa kati ya kumi wamefeli.

  Kwa vile tunawekeza sana kwenye mambo ya shughuli hivyo tusishangae na tukubali kupokea hayo mavuno ya hovyo. Wajanja wachache ndio wanatupeleka kwenye udini kwa lengo la kutupotosha na hivyo kupotea njia kwa sababu tusipojikita kwenye tofauti za kiimani, tutafunguka macho na kuanza kuhoji kwa nguvu zote wapi wanaotuongoza wanakotupeleka. Tuhoji kwa nguvu zote mfumo uliopo, vinginevyo tubakie kusali na kwenda kwenye waganga wa kienyeji kutafuta mchawi! lakini kwa Wakristo wanaelewa kuwa Mwenyezi Mungu atamsaidia mwenye kujisaidia. Hakuna miujiza
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, wangekuwa wanaandika majina tungeweza kuzungumza mengine lakini kwa namba hata mimi nakuunga mkono!
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Katika masuala ya utaifa hebu tuondoe hizi fikira za udini tubaki kuwa wote ni watanzania na imani zetu zisitugombanishe.
   
 11. comson

  comson JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  "serikali yetu imepiga hatua kubwa katika suala la elimu, na hatua kubwa kama hiyo haijawahi kutokea katika nchi nyingi za AFRICA (shule za kata), so hatua kubwa kama hiyo inweza kuwa na impacts mbaya au nzuri watz tuwe tayari kwa lolote" maneno ya mtu mmoja bungeni........
  hv shule za kata ni hatua ya kufurahia..............?
  zamani ilikuwa unafaulu halafu unakosa nafasi (hauchaguliwi), ila sasa unafeli then unapata nafasi....... watz tunatoka wapi tunaenda wapi..........?
   
 12. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Mtu yeyote aliyefilisika kifikra hukimbilia udini kuhalalisha hoja zake za kichovu.
   
 13. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Wenzetu walidhani shule zinafaulisha kwa kuwa na neno Seminary, Wakabadilisha majina ya shule zao na kuziita ....... Seminary. Angalia hizo shule performance zake zinatisha.
  Nilisema kitu kimoja "Kama mtoto wa Rais na Waziri wa Elimu wanasoma
   
 14. k

  kanjanja Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na nyinyi ndugu zetu waislam mmezidi kulalamikia v2 vilivyo wazi kabisa.., hebu boresheni shule zenu msitulilie maana kama mmeamua kusoma juzuu bila elimu dunia, hayo ni matatizo yenu!!! ss tunasoma vyote ; elimu dunia na elimu ahera na ndio siri kuu ya kufanikiwa maana kwa elimu tunaongaza. SS tunasoma shule zote ziwe za ki-kristu, kiislam na za serikali na number ya wasomi wakristu ucpime!!!! kama hamtabadilika na kutuiga mtazidi kulia kila siku!! kwani hamuoni hata Kikwete alikosoma? tena mumshukuru NYERERE kwa uamuzi wa kutaifisha shule zetu ili na nyinyi walau msome coz sasa hivi mngekuwa mnalia na kutoa makamasi, achaneni na juu bila mipango coz imesha- prove failure!!!!
   
 15. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hakuna sababu ya kuwalaumu wanaohusisha matokeo na udini. niwataarifu tu kuwa hii ni phase 2 ya PROJECT 2010. Na kwa sasa inafahamika kama PROJECT 2015. Msijidanganye kuwa itazuiwa na vimakala vya akina Lula. Ni project inayopokea mabilioni ya shilingi kila mwaka. Mnashangaa redio! Mtaziona tv nyingi za project kabla ya 2015. Mnamlaumu Basalehe! Mtawaona na kuwasikia wengi kabla ya 2015. Tegeni masikio na fumbueni macho, but FYI, PROJECT 2015 itashinda.
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  zanzibar shule zote za makanisa hazikuguswa
   
 17. e

  eddy JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,370
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Mcechuru Ndalichako sio mnyarwanda kweli? isijekuwa anatukorogea elimu kwa makusudi!
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  una moyo safi ndio maana uwaasa wadini
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni kwa sababu hujui majukumu ya katibu wa baraza la Mitihani sio yeye anayesahihisha mitihani. wanaosahihisha mitihani ni waislamu, wakristo, wapagani na wa dini zingine wakiwa wamepewa namba tu za watahiniwa ili kuondoa upendeleo. hapo utajuaje kuwa huyu ninayesahihisha karatasi lake ni wa dini fulani?
   
 20. e

  eddy JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,370
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni watoto kuchanganyiwa mitaala inawezekana anafanya makusudi au anavuta cha juu kwa akina Nyangwine auze makabrasha yao, haiwezekani kila mwaka mitaala ibadilike! watoto waende chaka!
   
Loading...