GE2025 Kufanyike nini wapiga kura tutoke? Hayo mazoezi ya majeshi yanatutisha, waandamanaji nao vilevile!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

mkulimamiwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
2,440
Reaction score
4,857
Mwaka huu huwenda ukawa ni mwaka mgumu sana kutekeleza haki zetu za kikatiba za mwananchi kwenda kupiga kura

Nchi nzima imetaharuki, sijawahi kuona wanajeshi na majeshi mengine kufanya mazoezi kama ilivyo sasa tena tu ni kwa ajili ya uchaguzi

Ukweli ni kuwa, magwanda ya wenzetu hawa, yanatosha kabisa kutaharukisha wananchi hasa kwetu sisi wa vijijini huku

Mazoezi yanayofanyika sasa tunapoelekea uchaguzi, binafisi yananifanya niogope hata kwenda kupiga kura yenyewe

Jambo hili si kwangu tuu, kijijini kwetu huku, kila mwananchi anahofia jambo hili, mambo haya mawili, ya majeshi kufanya mazoezi na tishio la maandamano, ki ukweli kabisa, serikali ifikirie namna nzuri ya kutoa elimu zaidi ili kuondoa hofu kwetu wapiga kura

Mi nadhani, Jeshi lingefanya mazoezi ya kificho ili wananchi tusijae hofu kama ilivyo sasa

Kwa namna ilivyo sasa, inakuwa ni vigumu sana kujitokeza kwenda kupiga kura, kwa sababu, hofu ya kwanza ni juu yao hawa wanaofanya mazoezi yaani, (Majeshi) na kwambaa, ikitokea hawa waandamanaji wakajitokeza, wataweza kumtambua mtu mwema na muovu? Au tutapigwa wote bila kujali mimi nilienda kupiga kura?
 
1. Unaweza kujitokeza kupiga kura ukakutana na kundi la waandamanaji wakakudhuru
2. Unaweza kujitokeza ukakutana na polisi wanasambaratisha waandamanaji wakakudhuru.
3. Unaweza kutoka kupiga kura, ukapiga zako fresh bila tatizo lolote.

Ushauri.

Kama huna lengo la kuandama bora ukae zako ndani. Maana washindi wanajulikana. Kura yako haina maana yoyote, upige usipige matokeo ni yale yale. Sasa ni kwanini uhatarishe maisha yako kwa kitu kisichokuwa na tija?

Kama umedhalimia kwenda kupiga kura basi sikilizia kwanza, usitoke mapema. Vuta vuta mida yaa saa 5 hivi utakuwa umesha soma ramani ya eneo lako na hali ya usalama.
 
Mwaka huu huwenda ukawa ni mwaka mgumu sana kutekeleza haki zetu za kikatiba za mwananchi kwenda kupiga kura

Nchi nzima imetaharuki, sijawahi kuona wanajeshi na majeshi mengine kufanya mazoezi kama ilivyo sasa tena tu ni kwa ajili ya uchaguzi

Ukweli ni kuwa, magwanda ya wenzetu hawa, yanatosha kabisa kutaharukisha wananchi hasa kwetu sisi wa vijijini huku

Mazoezi yanayofanyika sasa tunapoelekea uchaguzi, binafisi yananifanya niogope hata kwenda kupiga kura yenyewe

Jambo hili si kwangu tuu, kijijini kwetu huku, kila mwananchi anahofia jambo hili, mambo haya mawili, ya majeshi kufanya mazoezi na tishio la maandamano, ki ukweli kabisa, serikali ifikirie namna nzuri ya kutoa elimu zaidi ili kuondoa hofu kwetu wapiga kura

Mi nadhani, Jeshi lingefanya mazoezi ya kificho ili wananchi tusijae hofu kama ilivyo sasa

Kwa namna ilivyo sasa, inakuwa ni vigumu sana kujitokeza kwenda kupiga kura, kwa sababu, hofu ya kwanza ni juu yao hawa wanaofanya mazoezi yaani, (Majeshi) na kwambaa, ikitokea hawa waandamanaji wakajitokeza, wataweza kumtambua mtu mwema na muovu? Au tutapigwa wote bila kujali mimi nilienda kupiga kura?
Hapo ni kupumzika nyumbani tu kwani hiyo kura yako haina maana yoyote matokeo tayari yako kwenye server za INEC.
 
Kwamimi ambaye SITIKI majeshi labda yaje yaung'oe mlango wangu lakini nitakuwa nayacheki tu kupitia dirishani.
 
Back
Top Bottom