Kufanyike nini sasa ili Hayati Magufuli achukiwe na wote? Naona waliokuwa wanamchukia wanabaki kuwa walewale

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Tusifichane,

Imebaki kuwa wale wale wenye chuki na Hayati JPM, tena ni wale wale ambao yeye aliwaita wakwamishaji wa maendeleo ya nchi, na aliwashughurikia kisawasawa

Waliokuwa wakila pesa za walipakodi Kwa mgongo wa wafanyakazi hewa, ndio hao hao wana chuki naye mpaka leo, kwa sababu mirija yao ilizibwa!

Wenzangu na Mimi waiba majina ya watu ili tu waajiriwe bila kupita shule, ndio hao hao wameendelea kumchukia, lakini majuzi kuna rafiki yangu mmoja alimshukuru JPM baada ya yeye kutimliwa akiwa na cheti feki kipindi hiko, aliamua kuingia shule kwa hasira, amehitim majuzijuzi na akaajiriwa idara ya Maji Dawasa, alimshukuru saana JPM kwa kumfanya awe na elimu bora.

Wale waliokuwa wakishirikiana na mabeberu ili kukwamisha ujenzi wa Bwawa la Umeme Rufiji na mazungumzo ya wamiliki wa migodi mbalimbali nchini ndio hao kila leo kelele na bahati mbaya wako mpaka huko juu, na ndiyo maana hata mradi huo hauendi utadhani anayekomolewa ni JPM, kumbe tunakomolewa wananchi! Hizo hasira zingine hazifai bhana.

Mashoga wenyewe wanajulikana, bishara zao walizifanya kwa taaabu mno kiasi kwamba wakaingia kinyongo na JPM.

Hata hivyo, Raia wema na wapenda nchi, wote walimwelewa huyu mwamba na bado wako upande wake lije jua au inyeshe Mvua, wataendelea kumtetea kila kunapotokea uhuni.

Na cha kushangaza, hao hao 2025 wataomba kura kwa kutumia jina na mifano yake ya uchapa kazi!
 
Mimi namkubali mpaka kufa ila sema Kuna eneo dogo tu alifanya nijione mbwa tu na degree yangu mpaka natumwa kuomba chumvi kwajirani maana Sinamchango wowote na degree ya ualimu toka 2015. Naomba mama aupige mwingi niajiriwe huu mwaka Ili nimchukie mwendazake.
 
Mungu akuone mkuu, naamini katika majira sahihi ya Mungu!
 
Mimi namkubali mpaka kufa ila sema Kuna eneo dogo tu alifanya nijione mbwa tu na degree yangu mpaka natumwa kuomba chumvi kwajirani maana Sinamchango wowote na degree ya ualimu toka 2015. Naomba mama aupige mwingi niajiriwe huu mwaka Ili nimchukie mwendazake.
Basi hutaaliwa kamweee kabisa
 
Kweli mkuu, ukiangalia hata humu wanaomchukia, utagundua kuwa ni wale wale walioshikiwa akili na kulishwa matango pori na wanasiasa uchwara toka 2016. Kazi za wanasiasa hao ni kuchumia matumbo yao na familia zao.
 
Unamchukia mfu ili iweje?

Tunaweza kuzungumza hoja, sera, dhana, siasa, uchumi bila ku personalize mambo?

Tunaweza kuongelea matatizo ya kimfumo bila kujikita sana kwenye watu binafsi?

JPM alikuwa na makosa mengi sana ambayo wengi hatukuyapenda.

JPM amekufa, tukipewa JPM mwingine kwa sababu kuna matatizo ya kimfumo, chuki yako dhidi ya JPM itakusaidia nini?
 
Mkuu, kuna watu humu wanamchukia yeye personally, japo hayupo nasi (rip rip JPM). Wanajua hawawezi kupambana na sera, utendaji kazi wake, uthubutu wake, nk, wanajua hivyo vitawasuta, kwa hiyo kitu rahisi kwao ni kumtukana yeye mwenyewe mchana kutwa usiku kucha. Hao watamchukia mpaka siku wanakufa.
 
Hao watu ni wa kuwapuuza tu sababu kiuhalisia haijawahi tokea Binadamu yeyote kupendwa na kila Mtu hata kama hajakwazwa naye.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom