Kufanya vibaya kwa Namungo FC inatokana na ratiba ya ligi kuu Tanzania Bara?

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Namungo Fc ipo nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa imecheza michezo 18 pekee.

Huku wawakilishi wenzao Simba Sc imecheza michezo 20 ya ligi kuu ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.

Namungo Fc ilikuwa na muendelezo mzuri wa kupata matokeo chanya katika ligi kuu na kombe la shirikisho Africa katika hatua za awali lakini baada kuingia kwenye makundi hali imekuwa tofauti kabisa.

Je tuseme ni kwa sababu timu inakosa morali ya kuichezaji na upambanaji kutokana na kukaa mda mrefu bila kucheza mechi kubwa?

Kabla ya mechi ya leo dhidi ya pyramids Fc ambapo namungo amepoteza goli 0-2 ni mechi ya pili mfululizo kwenye hatua ya makundi pia zinatimia siku 7 bila kucheza mechi ya ushindani wakati yupo hapahapa nyumbani.

Au wameridhika walipofika?
 
Yani unahoji kuhusu kufanya vibaya Kwa Namungo kwenye group stage yanye team kama Raja na Pyramid serous?

Anyway jibu jepesi ni kwamba, stage waliyofika saizi wamekutana na team ngumu kuliko stage zilizopita, Namungo hawana cha kupoteza maana group stage wameingia kama zari tu ila wamepangwa kundi gumu hivo mafaniko waliyopata ya kuingia group stage bado ni makubwa Sana kwao na wanahitaji pongezi

Ukitaka ujue kuwa wanahitaji pongezi jiulize club kubwa kama yanga au Azam zimeingia mara ngapi? Na mara ya mwisho Yanga kuingia group stage ya shirikisho alipangwa na hao pyramid wote tunajua nini kilimkuta, kwahiyo kuhusu ratiba lengo ilikuwa ni kuwapa muda zaidi wa kujiandaa na sio ubovu wa ratiba
 
Hilo kundi la kifo Namungo wasisingizie chochote, niliwaambia huku "wazalendo" wakajidai kupiga kelele kama kawaida yao, mpira ni kuwekeza tu sio kelele na kubeba watu migongoni.
 
Namungo hana uwezo hata wa kutoa sare katika hilo kundi yaani atapigwa zote
 
at this stage, namungo ni wa kupongezwa sana... mkumbuke huu ni msimu wake wa kwanza kwenye mashindano haya, na kufika group stage si kazi rahisi... CONGRATS NAMUNGO & AND KEEP IT UP...
 
Hili kundi la Namungo hata ukimtia Simba sc hatoboi kirahisi. Lazima atachezea tu.
Namungo afungwe na Pyramid.. useme sababu ni kutojiandaa..

Sisi Yanga wenyewe Pyramid alitufunga Mwanza kirumba . Na tulivyoenda kwake akatufunga nyingi zaidi...

Kundi la Namungo hata ajiandae vipi hawezi kutoboa sababu lina timu ngumu kuliko Namungo
 
Kwa hapo alipofika ni hatua ya kumpongeza ingawa alipenya kimuujiza kufikia group stages.

Wajipange mwakani watuwakilishe tena
 
Hili kundi la Namungo hata ukimtia Simba sc hatoboi kirahisi. Lazima atachezea tu.
Uko sahihi mkuu, hata mikia wasingefurukuta kwenye hili kundi! Labda kama wangesaidiwa na vipimo vya COVID19......! Jokes
 
Yani unahoji kuhusu kufanya vibaya Kwa Namungo kwenye group stage yanye team kama Raja na Pyramid serous?..
Hivi tanga alitoka na point ngpi mara ya mwisho alipokuwa kwenye makundi kma haya, sijauliza Kwa no a mbaya mkuu, Nataka tu kulijua kma kuweka kumb kumb Sawa...
 
Lengo la namungo ni kufika group stage na walifikia malengo so hawana cha kupoteza.
Sio kidimbwi wao walikuwa wanaenda enda tu hawana malengo kauli mbiu yao eti wana jiita wa kimataifa wana furahia kupanda ndege...dah yaani uto jamani wanachekesha.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
Malengo..au "plans" ni muhimu saaana,huwezi miliki kwa mfano gari kama hukupanga kumiliki gari!
Baada ya malengo ni namna ya kufikia hayo malengo; hapa ndipo penye kazi,lazima jembe liitwe jembe!
Aina ubora wako,kwa dhaati na kweli ya nafsi yako,koz humdanganyi mtu,utakuwa unajidanganya mwenyewe!..then ainisha udhaif wako,kwa dhaaati kabisa ya moyo na nafsi sababu uko mwenyewe,usijiletee kibri mwenyewe hapa,anguko au kupanda ni kwako!...fanyia kazi udhaif na ubora then...with tym mambo yaonekana,ya Simba its obvious! ...kufika nusu fainal ishakuwa sio issue,weka kwenye maisha yako binafsi,inawezekana!
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
Back
Top Bottom