Kufanya siasa yahitaji afya ya akili kubwa, Uongozi wa ACT Wazalendo chini ya Zitto, akili hiyo hawana, ila kutumia frusa wanaweza!

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Wasalaam

Mimi si mwandishi mzuri, lakini twende hivi!

Mbali na kwamba Chadema siipendi hasa kwa tukio la 2015, lakini hawa jamaa wanauongozi wenye watu waliojaliwa kuwa na akili kubwa sana,

Hawa watu, wamepitia mambo magumu mno mbali na kuwa na ushawishi Mkubwa kwa jamii, lakini hakuna madhara ambayo kupitia ushawishi wa chama hiki, wananchi waruhusiwe kuvunja sheria na au kumwaga damu, ila wao wenyewe viongozi ndio wanakuwa wanakinywea kikombe cha uonevu kutoka kwa viongozi wa serikali,

Katika hili, kuna wananchi wengi ambao kupitia mateso makali ya viongozi wa chama hicho, huingia na kuwa wanachama kwa sababu ki kawaida, binadamu tunahuluka ya huruma kwa wanaoonewa na hata kama hawaonewi, lakini kila wakati wanapokuwa wao tuu, lazima watu watanza kuona kuna uonevu, na kupitia uonevu huo, watu wanashawishika kukiunga mkono chama!

Viongozi wa chadema, wanajua kujenga hoja, na wanajua kucheza vema na siasa, uongozi wa awamu ya tano, Chadema ilipitia misukosuko mingi, lakini hutokuta wanapayuka maneno ya hovyo na ya kuwafanya wengine wasiwaunge mkono kama ilivyo kwa chama cha ACT na viongozi wake ijaokuwa baadhi tu ya wafuasi wake ndio hupayuka na kutukana maneno ya hovyo, hii ni kwa sababu nao hawaelewi siasa inavyokwenda, chama Ni watu, hata kama hawana akili,ila tuu hakikisha ndio watakupa kura!

Unapokuwa chama cha upinzani, nachokifahamu, unakuwa ni chama ambacho kitakuwa kikitafuta kuungwa mkono na wananchi wote ikiwezekana,

Penye mnyukano wa chama kinachokuwa madarakani, hiyo huwa ni furusa kwa chama makini cha upinzani kuwavuta wale wanaobagazwa ndani ya chama hicho

Chadema wameweza hili, walitumia vema mpalanganyiko wa 2015 na kujikuta kimekuwa chama kikubwa na kinachoogopeka na chama tawala,

Kuna hili la Wafuasi wa JPM, mbali na kwamba Chadema kinaweza kuwa ni chama ambacho sasa kinaelekea kudumaa kwa sababu mbali mbali, moja wapo ni ya umri wake bila kufikia malengo take, kutokubadili uongozi na kuweka damu changa n.k, lakini bado wanacheza vema karata ya kisiasa, Viongozi wake si wapaukaji kama ilivyo kwa chama kidogo na maskini cha ACT, viongozi wake ni hamnazo wapowapo tuu na hawana mwelekeo na hawajui wanataka nini masikini chini ya baba yao Zitto

Mashabiki wa waliokuwa upande wa JPM ni wengi na huwezi kuwabeza na kuwatukana hovyohovyo ikiwa kweli wewe unatafuta kukuwa kwa chama chako, hiyo ni karata nyingine kwa vyama vya upinzani kutafuta uungwaji mkono na Wafuasi hao

ACT kupitia baba yao Zitto, tayari wameonekana kuwa ni chama ambacho kipo kumpa manufaa zaidi zitto, na si kutaka kuwa chama cha upinzani, kama kiongozi wa chama, huwezi kutoa kauli tata na za kipuuzi kama afanyavyo baba zitto na ACT kusema eti Wafuasi wa JPM wakazikwe naye badal a ya kutumia furusa hiyo kukiongeza chama chake

Kwa haraka haraka, Wafuasi wa JPM, hivi majuzi kunaonekana kuna chama kipya ambacho hata hakijulikani iwapo kweli kina malengo na falisafa kweli za JPM, mamia kwa maelfu ya watu wameanza kukishabikia chama hiko, kwa sababu hakuna chama ambacho kinaonekana kuwavutia ili kupoza Machungu na matusi kutokana na kwa aliyekuwa kiongozi wao waliyekuwa wakimwamini,

Siasa ni kuwa na watu, haijalishi watatokea wapi, ila tu ni kwamba, una wafuasi na wanachama wengi

ACT kinakosa viongozi wenye ushawishi kwa wananchi na wenye akili kubwa

Zitto hawezi, yeye aendelee kuegemea watawala ili wampe atakacho ale ili siku ziende, ila si yeye kutafuta wana chama. Hana uwezo huo, kwenye masuala ya siasa yuko empty mno, na hilo jina chadema ilimsaidia sana umarufu mdogo alionao
 
Alishashtuka kuwa hana watu wenye ushawishi so anatumia fulsa iliyopo kuelekea 2025 asije akakosa hata wawili watatu huku bara.
 
Back
Top Bottom