Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,442
- 113,452
Wanabodi,
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kila nipatapo fursa, huwa naendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zina lengo la kukuza uzalendo na kulisaidia taifa letu, kusaidia nchi yetu, kusaidia serikali yetu na kusaidia viongozi wetu waweze kutuongoza vizuri kwa kuangazia maeneo yenye changamoto ili zitatuliwe. Makala ya leo ni hoja na swali.
Hoja ni "Kufanya Kosa Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa", hoja hii inakuja kwasababu hatuongozwi na malaika, tunaongozwa na binadamu, katika kuongoza huko, huweza kufanyika makosa ya hapa na pale. Hivyo hata kukifanyika makosa, kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa.
Hoja hii inakuja kwa tangu rais Samia ashike usukani, juzi ndio amefanya uteuzi wake mkubwa wa kwanza wa viongozi wengi kwa mpigo. Kwenye uteuzi huu, kuna idadi ndogo ya wanawake, na ndipo kwenye swali, "Jee ni kweli Tanzania hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa za uongozi kustahili uteuzi?. Kwa maoni yangu japo uteuzi huu una walakin ya idadi ndogo ya wanawake, yaani gender imbalance, Rais Samia hajafanya kosa, bali akirudia idadi ndogo hivi kwa ma DC, RAS, DED na ma DAS, then, litakuwa ni kosa!.
Lazima tukubali, tukatae, kwenye gender balance kule nyuma, kuna makosa yalifanyika. Sasa ni jukumu letu sisi tuliobahatika kuyaona makosa hayo ya nyuma, ambayo Rais Samia ameyarithi, tumsaidie, rais Samia, kwa kuyaangazia makosa hayo, ili rais Samia asiyarudie makosa ya nyuma kwa spirit ile ile ya kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa, kwenye uteuzi wa maRC kuna kosa la gender balance, kwa vile sasa wanakuja ma RAS, wanakuja ma DED, wanakuja ma DC, wanakuja ma DAS, tumsaidie Tanzanite Lady wetu, Mama Samia, huko mbele, tusirudie makosa!.
Kabla haujasoma hoja za bandiko hili, naomba nikupe homework ndogo ya kusoma bandiko langu hili
Kwenye bandiko hilo nilisema
Uteuzi wa JPM, Kwa mfano idadi ya mawaziri wanawake ni 4 tu kati ya 19, hii ni asilimia 21%. wanaume ni asilimia 79%. Kwenye Baraza la Mawaziri la Samia, lina mawaziri 25, wanawake ni 6 ambao ni asilimia 24% wanaume 19 ambao ni asilimia 76%. Hivyo hapa gender imbalance imeendelezwa!.
Kwenye uteuzi wa Wakuu wa Mikoa, kati ya wakuu wa mikoa 26 wa Magufuli, wanawake ni 4 tu ambao ni asilimia 15% wakati wanaume ni 21 ambao ni asilimia 85%!. Sasa rais Samia anapita mule mule, alikopita JPM kwenye uteuzi wa wakuu wa mikoa wa Samia ameteuwa ma RC wanawake 4 tu kati ya ma RC 25, hii ni asilimia 16% ndio wanawake na wakati wanaume ni 21 ambao wanafanya asilimia 84%!.
Kwenye wakuu wa wilaya, kati ya wakuu wa wilaya 134 wa Magufuli, wanawake ni 25 tu ambao ni asilimia 18%, wakati wanaume ni 109 ambao ni asilimia 82%. Na kwa upande wa Wakurugenzi, kati ya wakurugenzi wa halmashauri na wilaya 185 wa Magufuli, wanawake ni 33 tu!, ambao ni asilimia 17% tuu, wanaume asilimia 83%.
Kwa trend reading, kama ni kweli kabisa Samia ni kama Magufuli, then you know what to expect, kwenye uteuzi wa ma DC na Wakurugenzi. Jameni hili ni kosa, lisiachwe liendelee!, ili tufikie gender balance ya 50/50.
Kwa vile hatukumpangia JPM nini cha kufanya, hivyo nilisisitiza tangu mwanzo, hata Mama Samia, tusimpangie, lakini huku kutompangia hakumaanishi tunyamaze tuu, pale tunapoona mapungufu mahali, au mambo yanakwenda ndivyo sivyo, tunawajibu wa kumshauri ili kumsaidia.
Katika safari ya kuelekea gender balance ya 50/50 katika uongozi, mimi siamini kuwa Tanzania hatuna wanawake wa kutosha hadi uteuzi wa wanawake uwe that low!.
Kwa maoni yangu, naamini uteuzi huu wa ma RC ni mama Samia, ameendelea kubeba some luggages na baggages za mtangulizi wake. Hilo ni kosa!. Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa!. JPM alifanya kosa kwenye gender balance.
Gender balance kwenye baraza la mawaziri hatuwezi kulaumu, kwasababu ili mtu uwe waziri ni lazima kwanza uwe mbunge, ikitokea hakuna wanawake wa kutosha kujaza nafasi za kufikia kiwango cha 50/50, hili litaeleweka, kwasababu Mama Samia, ameingia na kuwakuta wabunge tayari wapo, ikitokea wabunge wote hadi wa viti maalum, hawana sifa za uwaziri, hatuwezi kulaumu, kwasababu sio kosa lake. Huwezi tuu kujiteulia watu hawana sifa ili tuu kutimiza gender balance. Lakini kwenye ma RC, ma DC , ma RAS, ma DAS ns na DED, yaani Wakurugenzi, haiwezekani Tanzania ndani ya hii milioni 60, wakakosekana wanawake wenye sifa.
Hitimisho
Naamini rais Samia, kaletewa majina na kuongeza wachache tuu, hivyo sasa tunamuomba, kwenye ma DC, ma RAS, ma DED na ma DAS, awatendee haki wanawake wa Tanzania.
Nisimalize bila kumpongeza Mama Samia kwanza kwa ku heal the nation kwa kutenda haki, na pili ni pongezi kwa kuyaishi maneno yake ya kuteua yoyote hata kutoka upinzani.
Tanzania ni yetu sote,
Mungu mbariki Mama Samia.
Mungu ibariki Tanzania.
Paskali
Update
Hoja za bandiko hili, zimejibiwa jana na Rais, Mama Samia wakati akiapisha majaji, amesema ataongeza nafasi za wanawake kwenye teuzi zote zijazo
Hii ni habari njema, hivyo mabandiko kama haya, yanasaidia.
P

Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa!
Wanabodi, Nimeona mijadala mbalimbali kumlaumu rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuteua wabunge wanaume 6 na Wanawake 2, kati nafasi zake 10 za uteuzi. Naomba kukiri nimehamasika kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana JF huyu Mkuu Learned brother Petro Mselewa. Kwanza...
www.jamiiforums.com
Kwenye bandiko hilo nilisema
Kwa vile Mama Samia amejitanabaisha wazi yeye ni kama JPM, kwenye upande wa uteuzi wa JPM, we had gender problem, Mama Samia, asiiendeleze.Sasa kwa vile wanawake hao wenye sifa na vigezo hivyo vya kuteuliwa hawako wa kutosha, then rais hawezi kujiteulia tuu wanawake just kwa vile ni wanawake hata wasio na sifa na vigezo, ili tuu kutimiza takwa la usawa wa kijinsia kwenye katiba, eti kwa sababu tuu katiba imeshauri, no way!, kwani Katiba ni nini?, hata ikibidi kuweka pembeni katiba, then Magufuli, weka tuu pembeni katiba, kama ulivyofanya kwenye mikutano ya kisiasa, endelea kupiga kazi!.
Naendelea kumshauri rais wetu mpendwa, angalia nchi inataka nini, fanya kile kitu nchi inataka na aendelee tuu kuchapa kazi na kuteua watu wenye sifa na vigezo kwa nafasi mbili zilizobaki, kama hakuna wanawake wenye sifa na vigezo, teua tuu wanaume, kwa sababu sote tunaishuhudia performance ya hao wanawake wawili aliosha wateua, kwa maoni yangu wanatosha sana, maana kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa, kuliko kufanya makosa tena, teua tuu wanaume hata nafasi zote za uteuzi, kwa sababu Tanzania wanawake wenye sifa na vigezo bado hawatoshi, ila wakitosha, wateue!.
Wanabodi na haswa wanawake, naombeni sana msinielewe vibaya, kwa sababu wanawake ni mama zetu, wake zetu, wapenzi wetu, dada zetu, shangazi zetu, shemeji zetu, watoto wetu, samahanini sana kwa kuwaambia kuwa hamna sifa na vigezo vya kutosha kuteuliwa ili kufikia lengo la 50/50 kwa sababu huu ndio ukweli wenyewe japo ni ukweli mchungu, kwa sababu kama mgekuwa na sifa na vigezo, mngeteuliwa!.
Uthibitisho kuwa Tanzania hatuna wanawake wa kutosha kujaza nafasi stahiki za uongozi sio kwenye ubunge tuu hata teuzi nyingine.
Kwa