Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,

Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa CHADEMA, maana nimenote baadhi ya viongozi, wanachama, wafuasi wamepigwa na butwaa kwa uamuzi wa wanawake mashujaa, mashoka wa CHADEMA, kukataa ujinga wa chama chao and did the right thing.

Kitendo cha CHADEMA kususa kupeleka majina ya Wabunge wa Viti Maalum, ni kufanya kosa, ila kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa. Hili kosa la CHADEMA is a death mistake or a deadly mistake, hivyo CHADEMA hapo ilipo kwenye matokeo ya uchaguzi huu is almost dead, due to such deadly mistakes.

Uamuzi wa kina Halima Mdee kukataa ujinga wa chama chao, ndio the only hope for Chadema survival. Wakiwatimua, its adding an insult to an injury, huku kutakuwa ni kurudia kosa, it's do or die kwa CHADEMA. Warudie kosa wafe, au wakubali matokeo, waendelee kuishi, the choice is theirs.

Kuna wanasiasa wako kwenye siasa, na wametafuta uongozi wa siasa kwa kusaka madaraka tuu, uongozi as a means of livelihoods, lakini kiukweli siasa hawaziwezi, hawazijui wala hawajui uongozi wa umma sio utumishi wa chama ni utumishi wa watu.

Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Kwenye bandiko hili, nilieleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya Tanzania, vyama vya siasa sio mali ya viongozi, sio mali ya wanachama, ni mali ya umma, hivyo maamuzi yoyote ya chama lazima yatangulize mbele maslahi ya umma.

Vyama vya siasa kama vilivyo vyama vya wafanyakazi, vina uhuru wa kugoma, kufanya maandamano na hata kususia jambo lolote, ili mradi kugomea huko au kususa huku, kwa kususa huko kuna something tangible they will achieve. Kususa tuu ili mradi kususa bila ku achieve anything nilikuita ni ujinga.

Leo, nimefarijika sana kusoma haya;
Wabunge Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameanza mchakato wa kusajiliwa Jijini Dodoma.

Majina yao yamewasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA

Wabunge wa viti Maalum CHADEMA wanaoapishwa ni:
1. Halima Mdee
2. Grace Tendeka
3. Ester Matiko
4. Kunti Yusuf
5. Salome Makamba
6. Anatropia Theonest
7. Hawa Mwaifunga
8. Tunza Malapo
9. Nusrat Hanje
10. Agnesta Lambat
11. Sophia Mwakagenda
12. Cecilia Pareso
13. Jesca Kishoa
14. Ester Bulaya
15. Naghenjwa Kaboyoka
16.
17.
18.
19.

HOTUBA FUPI YA HALIMA MDEE KWA NIABA YA WABUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA

Nikishukuru chama changu cha CHADEMA kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe ambao kupitia wao sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu, viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata

"Mh. Spika tumefanya kazi wote kwa miaka zaidi ya 10, tutafanya kazi kwa uaminifu kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa uadilifu mkubwa, tuna vijana wapya sisi kama dada zao tutahakikisha wanafanya kazi nzuri kwa ajili ya Taifa hili

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana, Mh Spika nikushukuru sana, wewe na chama chetu

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana, Mh Spika nikushukuru sana, wewe na chama chetu"

View attachment 1633801
Naunga mkono hoja, hongera sana Mhe. Halima Mdee kwa kukataa ujinga na badala yake kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii, KM wa CHADEMA, J.J Mnyika amesema chama kama chama hakija poleka majina.

Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa CHADEMA, najua mtaitisha kikao cha dharura cha ile Kamati Kuu, na kukaa kama a kangaroo court kama kawaida yenu, kulijadili hili, na kuwatimua, nawashauri, msipoteze muda wala msithubutu kuwatimua as usual kama waasi, kwasababu hapo CHADEMA ilipo is almost dead ikiwatimua, this is a deadly mistake, huu ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa CHADEMA.

Kwa vile mule Bungeni hawa ni the minority, hata CHADEMA mkiwatimua kwa kuwafuta uanachama wao kikangaroo, kama mlivyo mfanyia Zitto, kwanza Spika atawalinda as the minority ila pia Watanzania wote wenye akili timamu, hawatawaelewa kabisa CHADEMA, kwasababu, hamtambui matokeo, hamlitambui Bunge, hivyo jikausheni tuu, muendelee kujivutia ruzuku.

Mkiwatimua this will be a very sad ending for what was used to be CHADEMA.

Hapo ilipo tayari CHADEMA is severely and deeply wounded, uchaguzi huu umewaacha with very big injuries, kitendo walichokifanya mashujaa hawa wanawake wa shoka wa CHADEMA, waiongozwa na shujaa Halima Mdee kukataa ujinga wa CHADEMA, ni kitendo cha kishujaa sana, kuwatimua its like adding an insult to an injury.

CHADEMA ikiwatimua, it will no be an instant death, but a slow poisoned death. Waliotimuliwa ndio watasikika, waliowatimua wenzao, ndio wataishia 6ft under kwa kupitia hukumu ya karma.

Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. Kususa kupeleka majina ni kosa, mimi niliuita ni ujinga, kina Halima Mdee wameukataa ujinga huu, kuwatimua ni kurudia kosa.

CHADEMA msifanye death mistake, deadly mistake, mtakufa slow death!

Paskali
 
Executive decision nikuwafukuza wote na yule wa mpanda.

Matumaini, imani na subra za wanachama na watanzania zitadumu. Kinyume chake hakuna ataekuja wakuwaamini cdm na ijiandae kuwa NCCR mageuzi

Heshima na Nidham katika jambo lolote nikuamini, kusimamia nakuishi kile mnachokihubiri. Kinyume chake ni kuanguka.
 
Wewe ni mshamba sana Ila sometime unazuga unajua zaidi alafu tabia ya kuiandama CHADEMA unalipwa we mzee tulia kalee wake zako wawili na watoto wako, naona unaijadili Sana CHADEMA.

Ila uhalisia ni kwamba hata wakifukuzwa CHADEMA haina cha kupoteza maana CHADEMA ni itikadi sio Kama unavyofikili kirahisi, pendekezo langu ni kuwafukuza uanachama ndio Kinga pekee ya kulinda heshima ya CHADEMA.
 
Chadema wameshakuwa na wabunge bungeni sasa kwanini wasiwe na wabunge wa viti maalumu kama hawataki watangaze kufuta chama chao watume barua kwa msajiri
Ninafikiri siasa ni mahesabu. Ukikosea unapotea kwenye ulingo wa siasa.CHADEMA watch out! Safari hii by all standards you may perish miserably in the history of mult party politics. Pelekeni viti maalum msionekane waasi wa katiba na utawala bora kwenye macho ya wananchi.
 
Pascal, hili la viti maalum ilikuwa leverage kwa CHADEMA, ndio maana CCM wakawa wanahaha kila saa hadi kuja na ngonjera kuwa kuna mfumo dume.

CHADEMA kuwa ndani ya bunge sasahivi wanaeffect ndogo kuliko ambavyo wangeendelea kutokuwepo.

For survival ni heri CHADEMA wasiwepo ndani ya bunge ila wakabaki na leverage waliokuwa nayo. Through leverage many things can be accomplished, cause mtu ukiwa na leverage juu ya mtu, hiyo ni silaha.
 
Hongera Sana wanawake wa CHADEMA kwa kutanguliza maslahi ya Taifa mbele acheni Wahuni wa pale ufipa waendelee kuwapigia makelele mwishoe watachoka wataenda kulala.
 
Kama haya yote ni ya kweli na yana baraka za Chadema, bado ni wakati muafaka wa kuchukuwa kadi za CCM na kuhamishia vita ya mabadiliko tukiwa wote ni wana CCM nchi nzima.

Nadhani sasa tuachane na majina ya vyama, huu ni usaliti wa karne kama ni ya kweli haya na uchaguzi ujao ni kura za maoni tu CCM watakaoshinda kura za maoni uchaguzi umeisha.
 
Back
Top Bottom