Kufanya kazi Vijijini ni changamoto kwasababu ya Wanasiasa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,074
42,852
Hakuna watu wabaya kama Wanasiasa, nina ushahidi wa kutosha wa rafiki zangu wawili mmoja yupo kada ya mifugo ni daktari wa kata na mwingine ni msimamizi wa jumuiya za watumia maji CWBOS'C Mkoani Manyara huko Babati. Sasa kuna siku nilimtembelea Kijijini huyu wa maji nikakuta anateseka sana na Visa anafanyiwa na mheshimiwa diwani wa pale.

Mwanzo diwani alikuwa anaiba hela za mafuta ya kuendeshea pump alikuwa hajazi Lita zote karibia Lita kumi anaziuza Sasa huyu jamaa yangu alipopewa mradi akagundua yote Yale ndipo majanga yalipoanza huwezi Amini Diwani anafanya mbinu amuangushe jamaa Hadi kumkatia mabomba maksudi.

Huyu wa mifugo yeye alikuwa akipigwa Sana majungu hapo kijijini kuna mwamko mkubwa wa kisiasa yaani ushidani wa CCM na chadema Sasa diwani wa pale na viongozi wengine wakaanza kuleta majungu kwamba jamaa kapewa nyumba ya afya coz na mke wake ni nurse wa zahanati ya pale mara ooh eti nurse akiamshwa usiku hataki kuamka kumbe ni fitina na uwongo mtupu.

Kiukweli wanasiasa sio watu wazuri na ndo wanafanya watu waone mazingira ya kijijini ni magumu hasa kama ukiwabania maslahi yao kivyovyote.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom