Kufanya kazi na watu wanaoielewa dunia ni raha sana

Kuna hiyo nyumba house girl anapiga deki mara tatu kwa siku nyumba nzima (bonge la nyumba ) asubuhi baada ya chai, mchana baada ya lunch na usiku wenye nyumba na watoto wakiingia kulala.

Mshahara 40k kwa mwezi

Maza house wengi wa kibongo ni watesaji..
Dada anatakiwa kupata job description kabla ya ajira, tena wastaarabu wengine una deki nyumba mara moja kwa wiki. Anaishi yeye na mke wake tu watoto wako boarding sachool.
 
Na wengine kuajiri vitoto vidogo jamani.
Kutokana na hali halisi ya maisha hii sekta inategemewa na wengi kuleta kipato. Kama kungekua na system nzuri unapomuona mtoto kwenye ajira unampeleka kwenye nyumba ya kulelea watoto.
 
Ndio apate sasa nyumba za kishua na penyewe mama mwenye nyumba awe mzungu ila kama ni kama hawa ambao mfanyakazi akionekana amekaa anapewa kazi hata ya kutoa vyombo vyote stoo kisha asafishe na kuvirudisha eti kisa amepumzika tu baada ya kumaliza majukumu yake ya muhimu kwa siku husika basi we have a long way to go!

Wabongo tuna roho za kinyanyasaji sana hakyamungu!
Ndio maana na sie tunanyanyaswa na Wahindi na Waarabu eeh fair game mamaye.
 
Back
Top Bottom