Kufanya biashara kipindi hiki ni kigumu kuliko kwenye madaftari

monga farm

Member
Jun 25, 2021
84
152
Habari za leo ndugu,natumaini u mzima.

Aisee kwa mimi kufanya biashara kipindi hiki naona ngumu sana tofauti na tulivyodhania kwamba pesa itaonekana mtaani, jambo lililopo ni pesa inaonekana ila vitu vipo juu sana kiasi kwamba unabaki kushangaa nchi inaenda wapi na viongozi wanafanya nini zaidi ya kuongeza malipo kila leo.

Hivi mfano mimi ni mfugaji ila leo tunaamka chakula kimepanda bei na vifaranga vipo juu uliona wapi? Tangu kuanza kufuga kwangu sijawahi una na viongozi wapo kimya hivi hizi mambo ndo unataka tuwachague tena hapo baadae mtakapopita na sare zenu?

Safari hii hatutaki sare kama kazi hukufanya inavyotakiwa uongozi bye bye. Inaumiza sana mtu kuona unapambana halafu kila leo viongozi wanasema vijana kwa wazee tujiongeze kwenye kutafuta mkate huku wao wanaongeza bei za vitu.

Hebu tupia kwenye sekta yako nini kimeongezeka labda Mama hajui akipitia huku JF apate mwangaza.

Mpaka sasa wafanyabiashara 0-Serikali 4
 
Back
Top Bottom