Kufanikiwa Maandamano ya CDM ni kufeli kwa Mkakati wa CCM Bungeni

Wingi wa watu sio upigaji kura , rejea ya Mrema nk ! wengi hawajajiandikisha sasa sijui watapigaje kura
\

Acha porojo mazee na urejee takwimu za NEC kuhusu waliojinadnikisha dhidi ya Wapiga kura! Hujiulizi? Hushangai? Waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 19, waliopiga kura milioni 8! Wewe hujiulizi hao milioni 11 ambao hawakupiga kura walienda wapi? UCHAKACHUAJI uliofeli! Hata JK mwenyewe confidence yake kwishney!
 
Mengi yamesemwa kuhusu CCM, wanakosolewa lakini hawasikii. Sikio la kufa halisikii dawa.

Jamii forums imelaumiwa kwa kuikosoa CCM na serikali yake, badala ya Kuishukuru JF eti wanailaumu. Kwa muda wote ambao CCM wamekuwa wakikosolewa, wangejirekebisha leo wangekuwa na unafuu, OOOOOHH Hoi CCM poleni. Msiilaumu JF. Hata mie sina chama ila sijaridhishwa na utendaji wa serikali, serikali ya kuwanyonya wananchi kwa kukusanya kodi nyingi na kufanya matumizi ya anasa kama mashangingi na bilion 30 za chai na billion 25 za fenicha kila mwaka.

Wengi wa wachangiaji huku ni watu huru wasio na vyama ila hawaridhishwi na utendaji wa serikali, serikali ya ccm ni kandamizi. Wafanyakazi serikalini wengi wao ni wavivu, hawawajibiki. Askofu Kilaini hajakosea. Wanaingia ofisini wanasign wanakoroga chai wanakunywa siku imeisha.

kwa mfano ukiandika barua katika wizara haijibiwi, sijui wanatakaje? Wanataka kila mtu aende wizarani? Ni tija kweli mtu atoke mbeya au kigoma au Lindi aende dar wakati anaweza kujibiwa kwa email au barua?

Hata ukienda wizarani hutapata information, mpaka utoe kitu kidogo. Tanzania government is sleeping.

Wenzetu Kenya na Rwanda wanaendelea sana, wanakimbia while we are sleeping.

We just talk too much without actions, hakuna watendaji.

OOh poor ccm, poor serikali ya Tanzania
 
maandamano ya jana mbeya ilikuwa ishara tosha ya wananchi kuchoshwa na magamba!tukifanikiwa kupata tume huru ya uchaguzi tutatambua tatizo liko wapi.kama ni uelewa wa wananchi (ili waeleweshwe) ama kama kuna majini yanayokula kura (kama alivyowahi kulalamika mzee wa mapesa)

Huku Arusha tunasubiri maandamano mengine ya kupinga uchakachuaji wa Meya, yaani CDM wakipanga maandamano mengine huku Arusha nchi itataharuki kwa umati utakaojili; wana-Arusha hawatakubali tena upuuzi ule waliofanyiwa na Polisi wakati wa mauaji na itabidi Polis watoe ushirikiano wa hali ya juu kufanikisha mandamano hayo.
 
Wingi wa watu sio upigaji kura , rejea ya Mrema nk ! wengi hawajajiandikisha sasa sijui watapigaje kura

Mlitumia msemo mawazo hayo kuiba kura za wananchi nadhani mtaproof 2015
 
Back
Top Bottom