Kufanikiwa Maandamano ya CDM ni kufeli kwa Mkakati wa CCM Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufanikiwa Maandamano ya CDM ni kufeli kwa Mkakati wa CCM Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Feb 26, 2011.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Katika Bunge lililopita, CCM kwa makusudi na kimkakati kwa kushirikiana na Chama Tawala Kishiriki Zanzibar yaani CUF kwa kuwatia mfukoni NCCR na John Cheyo walikukihujumu Chama Kikuu cha Upinzania Tanzania CHADEMA kwa kuja na tafsiri mpya ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambayo ilibuniwa na CUF na kusimamiwa kikamilifu na Spika wa Bunge na Naibu wake John Ndugai kufanikisha hujuma dhidi ya Demokrasia kwa kuwalazimisha CHADEMA kufunga ndoa ya mkeka na Vyama vingine vya upinzani.

  Tundu Lisu au Tundi Lisu kama inavyotamkwa na Spika Makinda alisema waziwazi kuwa sheria za Tanzania zinaruhusu ndoa ya wake wengi, lakini haitambui ndoa ya waume wengi akimaanisha kuwa CUF haiwezi kuolewa na CCM kule Zanzibar na papo hapo kuwa na ndoa nyingine na CHADEMA.

  Tafsiri mpya ya Kambi rasmi iliyoasisiwa na CUF na kuthibitishwa na CCM kwa kungwa mkono na Cheyo, Mrema na NCCR ililenga kuvunja nguvu ya CHADEMA Bungeni na nchini kwa ujumla. Sote tunakumbuka hoja ya Hamad Rashid wakati akichangia tafsiri mpya ya Kambi Rasmi ya Upinzani jinsi ilivyochochea malumbano baina ya CHADEMA dhidi ya CCM na Vyama vingine vya Upinzani. Hata pale Mh. Lisu alipomuomba Spika amuamuru Hamad Rashid kufuta maneno ya kuudhi; kwa unafiki wa hali ya juu Spika Makinda alimtaka Hamad Rashid afute kauli yake lakini Spika pasi aibu wala woga na kwa kutumia madaraka yake vibaya akabandika neno lake lakini message sent, kauli ambayo iliongeza munkari kwa wachangiaji waliofuata na kugeuza Bunge kuwa sehemu ya kashfa na matusi na kuanika udhaifu mkubwa wa kiuongozi wa Spika Makinda kwa kubali kuwa sehemu ya malumbano yale. Wengi tunakubali kuwa ule ulikuwa mkakati wa kuimaliza CDM ambao waliamua kutoka nje kuonyesha kutokubaliana na tafsri mpya ya Kambi rasmi ya upinzania iliyokuwa njiani.

  KURUHUSIWA KWA MAANDAMANO YA CHADEMA KANDA YA ZIWA NA KUFELI KWA MKAKATI WA CCM NA 'WAPINZANI' VIBARAKA


  Bila shaka Wadau mtakubaliana nami kuwa wa uzoefu wa upinzani hapa nchini huwa si rahisi Vyama vya upinzani kuruhusiwa kirahisi kufanya maandamano. Rejea maandamano ya rasimu ya Katiba ya CUF Dar na Maandamano ya CHADEMA Arusha.

  Kwa hiyo naamini kabisa kuwa kuruhusiwa kirahisi kwa CHADEMA kufanya Maandamano kule Mwanza na Musoma bila Polisi kuleta sababu za 'kiintelejensia' za kuzuia Maandamano hayo ni mbinu ya CCM na Serikali yake kupima kama Mkakati wao wa Kifisadi dhidi ya CHADEMA Bungeni ulifanikiwa au la.

  Maandamano ya Kihistoria ya CHADEMA Mwanza na Musoma yamethibitisha kuwa kinyume kabisa na matarajio ya CCM na CUF. Watanzania ndio kwanza wamezidi kuonyesha kuiunga mkono CHADEMA na kuwaonyesha CCM kuwa WAtanzania sasa wamegundua michezo michafu ya CCM na wanasonga mbele kwa kuonyesha imani ya hali ya juu kwa CHADEMA.

  Naamini hili laweza kuwatia kiwewe CCM na huenda wakaanza tena kuitumia Polisi kuleta sababu za 'kiintelejensia' ili kuwazuia CHADEMA kuandamana. Nawaambia wasijaribu kucheza na nguvu ya umma!

  OMBI LANGU KWA CHADEMA
  Mimi nasuburi maandamno mengine ya CHADEMA Arusha na nawashauri waje tena na maandamano yale yale ya kupinga mchezo mchafu uliofanywa na CCM na Serikali kutusimamishia Meya bila kushrikisha Vyama vingine, kupinga DUWANZI na Kupanda gharama za umeme na maisha kwa ujumla. Arusha hapatatosha na Maandamano ya Mwanza yatakuwa chamtoto!
   
 2. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Na bado mkuu!! Watasema tu, yanakuja ya warabu!!
   
 3. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  kamanda uyasemayo hapa yote yanatija, CCM waliweka mtego usiyo kuwa na malengo, ila kufanikiwa kwa CHADEMA ni salamu kwa ccm kuanza kujiuliza walipo toka walipo na wanapo kwenda sasa
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hayo uliyo sema ni kweli kabisa mkuu, nakumbuka Maria Hewa (MB) alisema bungeni kuwa watu wa Mwanza walikosea wakaati wa uchaguzi kuchagua, Maandamano hayo pia yatakuwa majibu kwa mbunge huyo wa viti maalumu kuwa Mwanza hawakukosea/hawajakosea bali walitimiza wajibu na wamemuonesha kuwa aliyosema bungeni ni pumba tu hawayajali. HONGERENI WANA WA MWANZA KEEP IT UP! Mpaka tuwazibe sehemu za kupumulia hao sisiem (Jiji njemu)
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  CCM wanajaribu kutumia kila intelijensia iliyopo kuyazodoa maandamano ya CDM na kuwarrubuni baadhi ya watu kuwa ni kupoteza muda.

  Lakini kama wangalikuwa na UFAHAMU wasingelala juu ya kitu kinachofanyika sasa hivi ndani ya CDM...Hakuna siku inayopita bila cdm kutajwa kwenye Media, na picha kuonyeshwa, huku neno CCM likizidi kuyoyoma na kudharaulika machoni mwa watu.

  Hadhara niliyoionA kwenye maandamano pale MUSOMA leo nimepigwa na butwaa!...Nimeambiwa na Mheshimiwa Mbunge mmoja wa CDM ambaye yupo kwenye kazi hii maalum, kuwa ameshuhudia wafanyakazi wakiacha ofisi zao wazi na kuungana msafara ili watembee japo kilomita moja, na kisha kurudi maofisini kwao...si jambo la mzaha hata kidogo.

  Lau kama hawa ccm wangelikuwa na jicho la 3, wangeliona kuwa HUJUMA zote wanazofanya Bungeni dhidi ya cdm ni mfano wa petroli inayomwagwa juu ya moto...na bahati mbaya vyombo vingi vya habari viliweka wazi kuwa Mama Anna Makinda ni zao la kifisadi, hivyo hata kama ataongea ukweli gani, lazima upande wa pili wahoji mno.
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Trust me,....
  kwa sasa hivi hakuna sehemu wata zuia maandamano na wafanye kama Arusha kule.

  Macho ya dunia nzima yako Africa,Jk na serikali yake hawataki kuonekana kuwa wananyima wananchi haki ya kukusanyika au kuandamana!
  Wanajua/walijua kabisa kwamba wange zuia maandamano kule mwanza nk basi chadema wangefanya kwa kulazimisha, na kama wangetumia nguvu kama kule Arusha tena (kwa sasa hivi) naamini unge msikia Ban kin moon akikemea mauaji Tanzania!

  Kwa sababu hiyo basi,viongozi wetu ambao ni watalii katika dunia hii,hawataki kujichafulia muonekano wao kwa wakubwa (UN)
   
 7. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mpaka kieleweke
   
 8. B

  Bolivar JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  CHANGAMOTO!

  Lets think of post CCM Tanzania,

  CCM ni tatizo japo si tatizo pekee, kuna mambo sharti tuanze kuyatazama ili tusije kuiondoa CCM lakini matatizo ya ufisadi na kutokuwajibika yakabaki pale pale.
   
 9. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Chadema oyeeeeeeeeeeeee, ccm magambaaaaaaaaaaa
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  good idea.japo hata kama chama tawala kitakachofuatia kitaendeleza kutokuwajibika nao tutawatoa!sisi watz wa kawaida tunataka kuona maendeleo na tija kwenye maisha ya kila siku!hata waje ccu ama ccp,wakileta longolongo tupa kulee!then wanasiasa watajifunza kuwajibika automatically.
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  maandamano ya jana mbeya ilikuwa ishara tosha ya wananchi kuchoshwa na magamba!tukifanikiwa kupata tume huru ya uchaguzi tutatambua tatizo liko wapi.kama ni uelewa wa wananchi (ili waeleweshwe) ama kama kuna majini yanayokula kura (kama alivyowahi kulalamika mzee wa mapesa)
   
 12. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thats just the beginning,nia yetu ni mpaka kieleweke!wajua hakuna serikali dhalimu na yenye kuika haki za binadamu km ya ccm haiwezi kubali maandamano ambayo yanafanywa na umma,ndo maana nguvu nyingi zinatumika,eg hapa Arachuga,lakin msimamo wetu kama wana cdm uko palepale,kuwaelimisha jamii kwakutumia mikutano ya hadhara!mwanzo mwisho mpaka kieleweke!CDM TWANGA KOTEKOTE
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mwendo mdundo with constant velocity towards 2015!
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Yote nimeyakubali. Ila mleta mada umenkumbusha kitu hapa,ivi chama kilichokuwa kinaitwa CUF kilienda wapi? Mara ya mwisho nlimsikia mtatiro kwenye kongamano la katiba udsm kisha kimya,au CUF walikuwa na hoja moja katiba? Jaman mitaani wamesahaulika wamebaki kwenye media!
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  the velocity increases with time mzee
   
 16. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Peoplesss Powerrrrr!!!!wakubali wakatae Chadema itasonga mbele tu.Ktk kikao cha Bunge kilichopita wakati Tindu Lisu anawasilisha mapendekezo ya baadhi ya vipengele ndani ya mahakama zetu alisema"msiniangalie mimi Kama Tindu Lisu au Kama Chadema bali changieni kwa faida ya Watanzania wote"lkn wabunge wa magamba kwa upeo wao mfupi wa akili pmj na kujali matumbo yao(njaa)hawakukubaliana na chochote.Binafsi nilitamani kuwa mchawi niwaue wabunge wote wa ccm kwa kushabikia ujinga(kuweka maslahi yao mbele)Viva Chadema na 2015 wale wote waliohujumu uchumi wa Watanzania wataenda kuanzisha timu ya mpira magereza
   
 17. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Ccm na anguko kuu............sasa wakati ni huu wa kuinyanyasa ccm na ccm-b
   
 18. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Kdogo jana kwenye taharifa ya habari ITV saa3:30 usiku waliirusha maandamano ya Mby ,duh! Kama ccm hawajuhi kufa basi mda wao umejiri, wakaangalie wenyewe wanachowafanya CDM ni kufuru kwa wenye ngozi za magamba

  nilifurahi sana,wanambeya wako mguu kwa mguu na Cdm kila kona ya mji,twanga KoTeKoTe jamani 2015 haiko mbali,CCM walitubip sasa hv tunawapigia wanaingia uvunguni,na CDM daima hatuna gia ya rivasi katika hili mpaka2015 tutakapoingia magogoni,PIIPOOOOOOOOOOOOOOOOO
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hebu nikumbushe wenyeviti wa kamati za bunge za hesabu za serikali za mitaa, na serikali kuu ni wakina nani vile ?
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wingi wa watu sio upigaji kura , rejea ya Mrema nk ! wengi hawajajiandikisha sasa sijui watapigaje kura
   
Loading...