Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Nakumbuka miongo kadhaa imepita tangu kutokee mtafaruku wa viongozi wawili mkoani Ruvuma kati ya Askofu na Mkuu wa mkoa. Askofu kilichomponza ni kumtaka Mkuu wa Mkoa kufuata maadili ya dini yake. Mkuu wa Mkoa alitaka aheshimiwe na Askofu kama Kiongozi asiyeguswa hata akienda kinyume cha maadili na miiko ya dini yake.
Mtafaruku huu ulipelekea mkuu wa mkoa kuonyesha mamlaka yake ya kidunia kwa kufunga hospitali kuu iliyokuwa ndio pekee mwambao wa ziwa nyasa huko Lituhi. Hakuishia hapo ila kuwahamisha wakazi wote wa hapo kwa kisingizio kwamba wako kando ya mto Ruhuhu ili kuwanusuru na mafuriko. Hata hivyo wachunguzi wa mambo walishangaa hoja hiyo kwa vile sehemu hiyo ni ya mwinuko na wengi tunavyojua mazingira kando ya ziwa nyasa yalivyo. Hayo yalitokea kipindi Cha Rais Mwinyi. Kitendo hicho kilimwuma sana Askofu huyo na waumini wa Mwambao na hata wakazi wengi wa Mkoa Ruvuma licha ya mkuu wa mkoa huyo kujenga jina zuri kwa mengi aliyotenda mkoani humo katika suala la maendeleo ya jumla.
Kwa waliokuwa karibu na askofu huyo walimsikia akisema, Mkuu wa mkoa aliyofanya bila kujali watu wake na huduma ya kanisa kwa kuwahamisha watu kwa lengo la kuonyesha mamlaka yake katika himaya yake kisiasa, kamwe hatakuwa na mafanikio makubwa kisiasa. Askofu huyo alifariki siku ambayo kulikuwa na sherehe za kitaifa Songea ambapo alialikwa kuwa mmoja wa wageni mashuhuri. Alisalimiana na Rais Mwinyi, kisha na mkuu wa Mkoa na jioni yake tulipata habari za mshtuko kwa Askofu huyo amefariki na kuacha simanzi kubwa kwa kuwa viongozi wengi kitaifa walikuwapo Songea. Amini usiamini, hayo yalitokea, kwani mkuu wa mkoa huyo alibaki kuhamishwa hamishwa na cheo cha juu alichojaribu kushika mambo hayakumwendea vema, hadi mauti yalipokumta hana cheo cho chote. Wengi walimlilia kwa maendeleo mbalimbali aliyofanya katika uhai wake licha ya kumwendea baba wa milele wakati bado nguvu za kimwili na kiakili zilikuwa zinahitajika kujenga taifa lake.
Yanayotokea Arusha si ya kudharau, maana ya hapa duniani yanapita, na hawa manabii wanachoongea ni sauti ya Mungu licha ya kuwa binadamu wenzetu. Tujue kwamba wametwaliwa kati ya watu ili wawahudumie watu katika mambo yamhusuyo Mungu. Tunapojibu kitu kwa hawa viongozi wa dini lets double check, or overlook what you going to respond to them. Usimjibu kama mwanasiasa mwezako kwa sababu kauli yako inaweza kuakisi maudhui yaliyo kinyume cha uadilifu katika maisha. Tukitanguliza heshima ya mtu ni bora kuliko onyesho la mamlaka ya tuliyo nayo ambayo yanapita na pengine yanaweza kutuharibia future yatu machoni mwa tunaowatumikia.