Kufagiliwa kwa JK na New African ni Uswahiba au Mshiko?

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Ukisoma New African Toleo la June 2008, Makala kuhusu Tanzania Riding High, na kama hujui Tanzania unaweza uamini kuwa Watanzania wanaishi katika anga la saba, hawana shida ya maisha na kila kitu ni shwari, ni kama vile maisha Bora kwa kila majakazi yamefikiwa.

Mwanadada Regina Jere - Malanda anamsifu Kikwete kwa kazi nzuri na hata anamtaja waziri wa fedha kuwa ni Zakhia Meghji. Wakati uchumi kwenye makaratasi unaonesha kuwa umepanda, hali halisi ni tofauti kwani Wabongo wanaishi nusu Jehanamu, mfumuko wa bei unaodaiwa kudhibitiwa katika hali halisi unatisha kama kivuli cha shetani, ukichenji shilingi 10,000 noti nyekundu haipo tena na vitu vinapanda mno. lakini mwadada huyu haya hakuyaona.

hakuona hata janga la mafisadi ama mwafaka wa kisanii wa zanzibar, kwake kila kitu ni shwari mno. Mhh huu kweli siyo mshikooooooooooo! ama ni uswahiba tuuu!
 
Hapa mimi ndo nashindwa kuwaelewa.. hawa wanaojiita "experts on African issues". Yaani awe mzungu au mwaafrika aliyeishia huko diaspora..wanaandika nadharia sana. Na naamini ndo ugonjwa ambao IMF na WB wamewaambukiza. wanaangalia uchumi wa makaratasi na statistics. Economy is growing 7%, blah blah.( kwa data zinazopikwa huko Washington).lakini reality ni kwamba hakuna kitu kabisa..watu hata mafuta ya taa ni issue iliyo beyond their reach.

Swali, ni je, hawa so called experts wanatufanyia makusudi kwa kuandika nadharia zao..au ni genuine ignorance (kwa kuangalia tunavyosifika nje na Bush, IMF, ziara za wakubwa..nk?) sielewi..what makes these folks think that Tanzania is doing better..wakati tumeshindwa kumtia pingu fisadi hata mmoja ambaye amehusika na upotevu wa mabillion ambayo kama yangetumika vyema yangetusongesha mbele!! All in all, I can say..wazungu na "elites" wenzetu waafrika hawataki waafrica tusonge mbele, maana the current situation benefits them a great deal.
 
Mimi nimeona hili gazeti bomu toka waliokuwa wakifanya kila jitihada kumfagilia Mugabe. Hao ndugu zetu kutoka magharibi ya bara letu naona hawatutakii mema! Au ndio biashara yenyewe?
 
alikuwa anamaanisha uchumi wa serikali ya kifisadi umekuwa lakini si uchumi wa Watanzania uchumi wa kweli utakuwa baada ya karne mmoja ijayo kwasababu hatutaki kuyavulia maji nguo...wamelikoroga na kulinywa hawataki
 
Waswahili twasema, "asifuye mvua imemnyeshea", Natumai umenipata vizuri hapo.
 
Hilo gazeti halina mpya na nnadhani bado wangependa sana ile Africa ya 60's, cold wars, Southern Africa liberation iendelee ili waendelee kuvuna mapesa. Just imagine Mugabe is reported to have paid over US$1.6 million to this London-based magazine "New African"
to counter bad publicity emanating from the 11 March 2006 oposition party (MDC)beatings.

Kwa hiyo usije ukashangaa hata muungwana labda ametoa kidogodogo na labda siye lakini wizara kama ya mambo ya nje au hata mafisadi kwa kujipendekeza wakafanya hivyo.
 
Unajua kuna jamaa mmoja ni mghana ni editor kama sikosei wa hilo gazeti...ni spin master nadhani wa viongozi madikteta wa Africa..anaitwa ANKOMAH..jamaa anajifanya ni mzalendo wa kiafrica anaibondea West..lakini huyo huyo hafungi virago na kurudi kwao Ghana akaangalie na kufeel policies za hawa viongozi anaowatetea...zilipotufikisha. Jamaa anamtetea Mugabe kwamba there is no problem in Zimbabwe.. only whites ndo wanamatatizo..., but he is in London enjoying the fruits of the wazungus anaowabondea, watoto wake wakipata elimu safi...yaani aise..nakwambia waafrica sisi..kazi ipo..... What I know ofcourse Mugabe alimpa mipesa kibao kuwa spin master wake against opposition. I respect his right to write and express himself, but I detest the way he construes facts and fictions. Jamaa naweza kusema ni spin master namba moja na opportunist!
 
Sawasawa mkuu Masanja, huyu jamaa anaitwa Baffour Ankomah, imagine hata jina lake analiforce force lionekane la kidhungu. And he is what? Son of Africa......... safari bado ndefu mkuu!!!!!!!!
 
Ukisoma New African Toleo la June 2008, Makala kuhusu Tanzania Riding High, na kama hujui Tanzania unaweza uamini kuwa Watanzania wanaishi katika anga la saba, hawana shida ya maisha na kila kitu ni shwari, ni kama vile maisha Bora kwa kila majakazi yamefikiwa.

Mwanadada Regina Jere - Malanda anamsifu Kikwete kwa kazi nzuri na hata anamtaja waziri wa fedha kuwa ni Zakhia Meghji. Wakati uchumi kwenye makaratasi unaonesha kuwa umepanda, hali halisi ni tofauti kwani Wabongo wanaishi nusu Jehanamu, mfumuko wa bei unaodaiwa kudhibitiwa katika hali halisi unatisha kama kivuli cha shetani, ukichenji shilingi 10,000 noti nyekundu haipo tena na vitu vinapanda mno. lakini mwadada huyu haya hakuyaona.

hakuona hata janga la mafisadi ama mwafaka wa kisanii wa zanzibar, kwake kila kitu ni shwari mno. Mhh huu kweli siyo mshikooooooooooo! ama ni uswahiba tuuu!

Mwandikie mpe picha halisi naumuulize kaandika kama mwandishi mchambuzi na mchunguzi ama kwa kaandika msukumo wa mulungula ?
 
...ile New African Special Edition ..zimbabwe Hata Mimi Ninalo Na Hadi Leo Huwa Narudia Kulisoma ...siamini Kama Yule Mwandishi Was Serious Au That Issue Was Just The Advertisers Column Au Alilipwa Na Jongwe!!!!.....tangu Hapo Nimeacha Ku Subscribe Issue Za New African.........issue Iliyotangulia Ile Ya Zimbabwe Pia Kikwete Alifanyiwa Special Interview Na Huyo Kuffour.....nadhani Hiyo Issue Uliyoona Last Month It Will Be Another Interview.....

For Sure I Will Not Buy That Again....though I Liked That Newspaper Since Was Very Young......pamoja Na Lile African Now!!!
 
hawa hawa wangeandika kukandia serikali ya kikwete wangeonekana mashujaa na kupambwa kwa kila aina.

ama kweli watu humu wa na majibu yao ukija kivingine wewe utakuwa huna maana
 
hawa hawa wangeandika kukandia serikali ya kikwete wangeonekana mashujaa na kupambwa kwa kila aina.

ama kweli watu humu wa na majibu yao ukija kivingine wewe utakuwa huna maana

Hapana, Mkuu! Si wote wenye mtazamo huo. Hili gazeti kwa wengine wetu limekosa credibility kwa kumfagilia mno Mugabe na other despots wa Afrika kwa kisingizio cha kutetea uAfrika. Kwa hali hiyo, wakimsifia Kikwete, panakuwa na shaka hata kama pana ukweli.
 
Back
Top Bottom