Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,358
- 6,077
Utaratibu huu ambao umeibuka wa kuwapeleka wanajeshi wetu kwenda kufanya usafi wa barabarani, kuzibua mitaro, kuzoa takataka na kufyeka majani ni kama kuwadhalilisha walinzi hawa wa mipaka ya nchi yetu.
Mimi binafsi nakerwa mno, sijui kwa Watanzania wenzangu, naona kama hii fani ya jeshi inadhalilishwa sana. Naamini tunapaswa kuwapa heshima wanajeshi wetu hasa kutokana na majukumu mazito waliyonayo ya kulinda mipaka ya nchi yetu. Jeshi ni lazima liheshimike na siyo kulipangia kufanya majukumu ambayo yalipaswa kufanywa na wafungwa!
Kazi za kufagia mabarabarani, kuzoa takataka, kufyeka majani mitaani, na kuzibua mitaro michafu ni kazi ambazo zilipaswa kufanywa na wafungwa waliojazana kwenye magereza zetu nchi nzima. Haiingii akili hata kidogo kuona wafungwa wanakaa tu bure magerezani, halafu wanajeshi wetu wanachukuliwa na kwenda kufanyakazi za usafi mitaani. Kwakweli haipendezi hata kidogo.
Mimi ningeshauri, wafungwa ndiyo wawe wanafagia barabarani, kuzoa takataka na kuzibua mitaro michafu, hata kama ni mara moja kwa wiki, na wanajeshi wetu wapewe jukumu la kuwasimamia tu hawa wafungwa ili kuongeza ulinzi wasije wakatoroka.
Hata kama jeshi linaadhimisha tukio fulani, lakini siyo sahihi hata kidogo kuwafanyisha walinzi wetu kazi zenye kudhalilisha na kufedhehesha mbele ya jamii. Tunalivunjia sana jeshi letu heshima mbele ya jamii na hata mbele ya mataifa mengine.
Mheshimiwa Rais Magufuli, ukiwa kama Amiri Jeshi Mkuu, tafadhali sana tafakari hili swala na ubadilishe utaratibu huu kwani haupendezi hata kidogo. Sidhani kama mawaziri wako na wabunge au makatibu wakuu wa wizara, watafurahia ukiwaambia wakafagie barabara na kuzibua mitaro michafu.