Kufa na kufufuka upya kwa vyama vya siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufa na kufufuka upya kwa vyama vya siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, Jul 31, 2011.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Mdahalo wa katiba uliofanyika ubungo plaza jana umekuwa tofauti na midahalo ya hapo kabla ile iliyotawaliwa na hisia za vyama vya siasa, kipindi kile hakuna kilichofanikiwa zaidi ya watu kuzomeana na kusodoana tu.

  Leo hali ilikuwa tofauti sana, kwani washiriki walikuwa watulivu na walipeana nafasi na kila aliyebahatika kupata nasafi ya kuchangia alitoa mawazo yake kwa uhuru tofauti na awli ilivyokuwa.

  MAWAZO YALIYONIGUSA NA MAPYA KWANGU NA NINAYOYAUNGA MKONO NI HAYA YAFUATAYO
  :-

  1. Dada anaeitwa Agnes alitoa mawazo yake kuhusu VITI maalum, alisema viti maalum vinarahisisha wanawake kutawaliwa na hata wanapofika bungeni hawana jeuri ya kutoa mawazo huru, kwani ni lazima waendelee kujipendekeza na kuwaabudu waliowawezesha (waliowazawadia)kupata nafasi hizo

  MY TAKE.

  Hii ni dhahili sana kwani hata mifano ipo wazi, sio wazo zuri kuwapata wabunge hawa kwa mfumo unaotumiwa wa vyama vya siasa kuwaweka watu wao, nyumba ndogo zao, wake zao, dada zao na ndio sababu hata leo utamsikia VITI maalum akijitambulisha kuwa ni mbunge kivuli wa jimbo fulani analoliota, na sio mbunge wa viti maalum wanaona aibu na hawana uhuru kwa kuhofia kuwakera waliowazawadia nafasi hizo n.k.

  Ushauri wangu kwenye katiba mpya hizi nafasi za makundi maalum, zisipatikane kupitia vyama vya siasa, ili makundi haya ya wanawake na walemavu, yawakilishwe bila upendeleo na bila itikadi za kisiasa.

  BABU ALIYETOA MFANO WA KINYONGA.
  Babu mzee sana alitoa unabii kama uliwahi kutolewa na Nabii katika injili ya luka, kuwa hatakufa mpaka atakapomuona Yesu, na mzee huyu leo ametoa unabii huo kwa kusema kuwa hatakufa kabla ccm haijafa, akatoa mifano mingi ya kuwataka viongozi wawe waadilifu na akashangiliwa sana.

  Mfano alioutoa Babu wa kinyonga kufa akiwa tayari amefikia term(yaani miezi ya kujifungua)au kinyonga dume kukubali kutafunwa na jike ili waweze kuzaa, ni mifano dhahili akilenga ccm ni lazima ife ili mfumo wa vyama vingi uwe huru na wa haki, hapa sio tu kwa ccm bali hata vyama vya siasa vina jukumu la kufa kiitikadi kiimani na kimienendo na hata kisera/kiorganisation, ili viweze kuwa na mitazamo imara na ya dhati, na ili viweze kudumu mioyoni mwa wananchi na viweke misingi ya kudumu ya kujiendesha kimgawanyiko wa kiutendaji.

  Ndio tafasiri ya kufa na kufufuka upya, kufa pia kuna maana ya kuwaweka watendaji wenye sifa katika ngazi husika na sio kama ilivyo kwa vyama vyetu hapa tz, vyenye viongozi wanaotumia nafasi zao kuwateua watu kwa vigezo wajuavyo wenyewe na sio uwezo wala sifa dhahili,hakutatokea mabadiliko ya kiutawala kama viongozi wa vyama hawatajikana nafsi zao wenyewe,bila kujali mtu bali wajali uwezo na utashi, hapa bila kukubali kuliwa na kufa ili vifufuke upya, hatutaona kipya i swear!!


  NIWATAKIE MATAZMIO MEMA YA KATIBA MPYA...
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  By 75%,nakuunga mkono kamanda...kwenye biblia kuna mstari unasema kwa kuwakaribisha watu wengine walijikuta wanawakaribisha malaika pasipo kujua,amini usiamini yule mzee aweza kuwa ni mwanadamu lakini aliongea kwa niaba ya roho mtakatifu na ni ajabu kuamini japo huo waweza kuwa ndo ukweli wenyewe
   
Loading...