Kufa kwa intelijensia ya CHADEMA

Kama mnakumbuka CHADEMA ilikuwa ni chama kinara wa kudaka taarifa za kiintelijensia zikiwemo za kuhujumu chama na ufisadi.

Mifano ipo mingi, intelijensia ilimnyaka Zitto akisaidiana na CCM kukiua chama. Kina Shonza na wenzie walinaswa kabla hawajaleta madhara nk

Lakini leo hii hali ni tofauti kabisa, CHADEMA kimekuwa chama kisichojua chochote kuhusu usalama wa watumishi wake,hakijua alipo Ben Saanane, hata kujua tu ni kina nani wamefanya haya.

CHADEMA ilikuwa chama cha kuwahi kabla hakijawahiwa. Zitto tulimuwahi, Shonza na wenzake walizimwa kabla na mapema. Lakini leo hii hata madiwani washamba kabisa wanashindwa kujjlikana mapema hujuma zao na kufukuzwa kabla ya kujiuzuru.Hovyo kabisa.

Lazima tukubaliane Dr. Mashinji kazubaa sana.
Chadema haikuwa na intelijensia wala ushuzi.Alichokuwa akifanya slaa ni kupata tip tu,na hao waliokuwa wakimpa tip wote wamepelekwa mbele ya haki,kwa sasa chadema hawajui pa kuanzia na utawala huu wa Magufuli umepiga pini sehemu zote nyeti ukigundulika tu umetoa siri huna kazi siku hiyo hiyo
Lakini nakubaliana na wewe Mashinji ni bomu.Uchaguzi wa 2019 mtamtimua kwa bakora huyo masinji.
 
Nakuunga mkono hoja yako mkuu umeandika point Chadema waliwahi kubaini madiwani wake wanne ambayo walipewa milioni 70 kwa ajili kuzijiulu udiwani wakafukuzwa kwenye chama .Hili la Arumeru ushahidi upo lakini chama wapo kimya wameshindwa hata kuchukua mapema kuna nini?
Lakini leo hii hali ni tofauti kabisa,CHADEMA kimekuwa chama kisichojua chochote kuhusu usalama wa watumishi wake,hakijua alipo Ben Saanane,hata kujua tu ni kina nani wamefanya haya.
Nakubaliga point zako kama hii ya leo, pale palipo na ukweli unasema, cyo wengine wanaokuwa wafa chama wanaogopa ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makamanda tunaelewana,tunaongea lugha moja hata kama ni kinzani

Sidhani kama Upo Sawa, tumezoea kuona hivyo kule CCM ambapo kuna kupishana Kwa akina Nape, Makonda, Aeshi, Dr. Kafumu, MSUKUMA, Kigwangala, nk na bado wanabaki kitu kimoja

Huku kwingine mtu akiwa na mawazo tofauti kidogo tu basi majina Yote mabaya ni Yake, atapchikwa kununuliwa, njaa, usaliti n.k
 
Lumumba mna ngano za zamani sana. Mlichobaki ni kula rambirambi na kukaa mabarazani kutafuta Leo Chadema wako wapi tuwakamate tuwaweke ndani.

Mmebaki kuwaota watu badala ya kufanya kazi. Kichaa wenu amebaki kuwatukana waliompa kura akidhani ndiyo stail ya kuwawin. I am telling this "Time will tell"
 
Ukitaka kujua umuhimu wa matako kalia kichwa.

Naona pengo la Dr Slaa limeanza kuonekana lakini mnashindwa kuusema huo ukweli mchungu mnaishia kujibaraguza.
 
Back
Top Bottom