Kuepuka vifo na Magonjwa ya moyo toa taarifa unaporudi nyumbani

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,404
9,233
Kuna msemo unasema usimuwekee mitego mingi ya kumfumania kama unajua huwezi kumuacha na unaipenda afya yako.

Mtu ulikuwa safari lakini unarudi nyumbani bila kusema Leo narudi , nini lengo ? unataka umfumanie?

Umeenda kazini unarudi hutoi taarifa kuwa uko njiani , nini lengo? unataka ujue alienda wapi?

Hizi 'saplaiz' zimeharibu zaidi ndoa na mahusiano kuliko kujenga na wengine wamekufa kwa presha.

Wazee wetu sio kwamba walikuwa 'hawachit' (sio wote) ila ndoa zilikuwa zinadumu kwasababu Mzee anapokaribia nyumbani alikuwa anatuma mzigo au koti linatangulia kwanza ili kama mama alikuwa sehemu anarudi mbio ili Mzee amkute, au kama aliingiza 'njemba' ndani amtoe haraka na ajiweke katika hali ya kutotiliwa shaka.

Hivyo ndivyo mahusiano yalivyo dumu enzi hizo.

Turudipo kwa wake zetu , tutume ujumbe kuwa "tuko karibu" hii itaondoa hata 'vipigo' kwa wake zetu pindi tunaporudi ghafla halafu hatuwakuti.
 
Back
Top Bottom